Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri na kunyambulisha mambo. Kama ndio akili mliyonayo graduate wetu wa kisasa pole sana mkuu. Soma vizuri comment yangu nadhani hujaielewa vizuri. UTAJIONA WEWE NDIYE UMEKOSA AKILI MARA 2
Umeandika madudu ndo Mana nimekujibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba? Tunakwama wapi?
Tunakwama hapa kwenye mawazo kwamba ukimaliza degree, lazima uajiriwe ofisini kufanya kazi na kulipwa mshahara. Elimu yetu 98% haifundishi ujasiriamali bali kuja kuajiriwa tu.

Ndio maana ni rahisi sana kumkuta mtu ana diploma/degree ya "project planning and management" au Masters in Business Administration ila hana a,b,c za kuanzisha wala kumanage business
 
Mtazame Mustafa Hassanal, aligeukia ubunifu wa mavazi na mitindo licha ya kuwa tabibu sasa ni mbunifu nguli barani Africa, mpwao kaona mbali sana, ushonaji ni kiwanda kikubwa anaanza taratibu
 

Hapo kwenye ufundi anakuwa anawashonea watu pia, koneksheni ni popote.
 
Atavyoanza kukushonea suti zako kwa laki saba uje tena uanze kulialia, acheni dharau sio mafundi wote ni washona viraka.
 
Hamna cha kukwama. Kwa taarifa yako, kama ameelimika kwa degree yake, akishajua ushonaji huyo mwalimu wake wa la saba atashangaa, kwa sababu atakavyoifanya hiyo biashara/kazi itakwenda sanjari na degree yake.
 
Wewe umeitumia elimu yako kutawala mazingira? Usikute umeajiriwa ila unavunga kutotambua masaibu wanayopitia wenzako.

Halafu issue kama ni kutawala mazingira basi elimu ya darasa la 7 inatosha sana. Wale jamaa wa Old Stone Age hawakuhitaji kupita shule ili wayatawale mazingira yao, instincts tu zilitosha kuwaongoza wafanyeje kupata chakula, malazi, mavazi, n.k.

Mtu anasomea Udaktari, kwa kuwa hawezi kujiajiri maana hana mtaji wa kununulia vifaa tiba, anajikuta anarudi kijijini kuchoma mkaa. What a wastage of time, resources and knowledge/skills!
 
Mimi Nina digree Nne,
Sasa hivi nimejikita kwenye TASNIA ya UDOBI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye udobi mtu hawezi kunishawishi. Watu wafanye mambo yao kwenye mashuka halafu niletewe nifue? Na degree zangu? Naheshimu kazi lakini hii hapana, unless uniambie nitalipwa mara 100 ya bei ya kawaida.
 
Kwenye udobi mtu hawezi kunishawishi. Watu wafanye mambo yao kwenye mashuka halafu niletwe nifue? Na degree zangu? Naheshimu kazi lakini hii hapana, unless uniambie nitalipwa mara 100 ya bei ya kawaida.
Ulipwe mara 100 ya bei ya kawaida kwa sababu wewe ni nani?

Una add value gani tofauti na madobi wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…