Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri na kunyambulisha mambo. Kama ndio akili mliyonayo graduate wetu wa kisasa pole sana mkuu. Soma vizuri comment yangu nadhani hujaielewa vizuri. UTAJIONA WEWE NDIYE UMEKOSA AKILI MARA 2
Umeandika madudu ndo Mana nimekujibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba? Tunakwama wapi?
Tunakwama hapa kwenye mawazo kwamba ukimaliza degree, lazima uajiriwe ofisini kufanya kazi na kulipwa mshahara. Elimu yetu 98% haifundishi ujasiriamali bali kuja kuajiriwa tu.

Ndio maana ni rahisi sana kumkuta mtu ana diploma/degree ya "project planning and management" au Masters in Business Administration ila hana a,b,c za kuanzisha wala kumanage business
 
Mtazame Mustafa Hassanal, aligeukia ubunifu wa mavazi na mitindo licha ya kuwa tabibu sasa ni mbunifu nguli barani Africa, mpwao kaona mbali sana, ushonaji ni kiwanda kikubwa anaanza taratibu
 
Kumbuka mpwa kakosa connection akipata connection in three or two year anakuwa na ukwasi au mali zaidi ya uyo fundi ila uyo fundu kitu kupata connection akabadili game faster kama mpwa pengine abet au ashinde tatu mzuka

Kwaiyo usimdharau mpwa ni mapito tu sema mpwa naye yupo porini sana nini si aendeshe hata boda boda afungue milango ya connection kwa kukutana na watu yani umesoma unatafuta kazi alafu unaenda kufanya kazi ya kukaa ukutani na wadau inatakiwa ajichanganye akapige hata vibarua vya ujenzi uko, au kupiga debe stand yani mixing style

Hapo kwenye ufundi anakuwa anawashonea watu pia, koneksheni ni popote.
 
Atavyoanza kukushonea suti zako kwa laki saba uje tena uanze kulialia, acheni dharau sio mafundi wote ni washona viraka.
 
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?
Hamna cha kukwama. Kwa taarifa yako, kama ameelimika kwa degree yake, akishajua ushonaji huyo mwalimu wake wa la saba atashangaa, kwa sababu atakavyoifanya hiyo biashara/kazi itakwenda sanjari na degree yake.
 
Nafikiri tatizo si elimu ila tatizo ni mpwa kuitumia Hiyo elimu

Elimu haikuanzishwa ili Watu waajililiwe ila ilanzishwa ili Watu waweze kutawala mazingira yao vizuri kwa uarahisi

Tunapokwama tunachukulia elimu ni kama njia ya kuajiliwa badala kuchulia kama njia ya kutufungua ufahamu wa kutawala mazingira
Wewe umeitumia elimu yako kutawala mazingira? Usikute umeajiriwa ila unavunga kutotambua masaibu wanayopitia wenzako.

Halafu issue kama ni kutawala mazingira basi elimu ya darasa la 7 inatosha sana. Wale jamaa wa Old Stone Age hawakuhitaji kupita shule ili wayatawale mazingira yao, instincts tu zilitosha kuwaongoza wafanyeje kupata chakula, malazi, mavazi, n.k.

Mtu anasomea Udaktari, kwa kuwa hawezi kujiajiri maana hana mtaji wa kununulia vifaa tiba, anajikuta anarudi kijijini kuchoma mkaa. What a wastage of time, resources and knowledge/skills!
 
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?
Mimi Nina digree Nne,
Sasa hivi nimejikita kwenye TASNIA ya UDOBI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye udobi mtu hawezi kunishawishi. Watu wafanye mambo yao kwenye mashuka halafu niletewe nifue? Na degree zangu? Naheshimu kazi lakini hii hapana, unless uniambie nitalipwa mara 100 ya bei ya kawaida.
 
Kwenye udobi mtu hawezi kunishawishi. Watu wafanye mambo yao kwenye mashuka halafu niletwe nifue? Na degree zangu? Naheshimu kazi lakini hii hapana, unless uniambie nitalipwa mara 100 ya bei ya kawaida.
Ulipwe mara 100 ya bei ya kawaida kwa sababu wewe ni nani?

Una add value gani tofauti na madobi wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom