Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Kwa hiyo degree ulitaka aende wapi?
 
Nina jamaa yangu ana Masters lakini kaila wekeend unamkuta anaendesha maharusi mjini hapa.
 
The sad part hata ushauri mzuri anaopata kutoka humu JF unaishia kwenye makabati,hata huu uzi utapita na kubaki kwenye archives za Jamii Forums..sio bure kuna tatizo la kusikia ama kuona kwa viongozi wetu lol
 

Elimu inaweza kumsaidia mtu alieyeipata aweze kutumia mazingira yake kama fursa ya kujipatia rizki yake ya kila siku ikiwa tu elimu hiyo imempa uwezo mhitimu wa kuyamudu mazingira yake, jambo ambalo halipo katika nchi zetu za ulimwengu wa tatu.
Mi nafikiri na ninaamini kwamba ni wakati muafaka sasa elimu yetu kuanzia msingi, sekondari, vyuo vya kati na vya juu imuandae mhitimu ambae atatumia maarifa aliyoyapata kuwa mzalishaji na sio mtoa huduma kama ilivyosasa ambapo taifa linazalisha walimu, wanasheria, wahasibu, madaktari, maafisa utumishi n.k ambao wote hawa ili waweze kuishi kwa kutegemea elimu waliyoipata ni lazima waajiriwe ili waweze kuhudumia, vinginevyo itawabidi kufanya kazi nje ya taaluma zao, kazi ambazo kimsingi angeweza kufanya hata asingeenda shule.
Hivi sasa sio ajabu kuona mhitimu wa chuo kikuu akiuza juice ya miwa, mitumba, mihogo, kupiga debe, dereva wa bodaboda, mama ntilie n.k.
Kimsingi kama taifa kuna haja ya kupitia upya aina ya elimu tunayotoa kwa vijana wetu kwa maslahi yao binafsi, familia zao na taifa kwa ujumla. "HAKUNA TAIFA DUNIANI LILILOPIGA HATUA KIMAENDELEO KWAKUA NA ELIMU INAYOZALISHA WAHUDUMU WENGI KULIKO WAZALISHAJI"
 
Mkuu umegusia kitu cha msingi sana,shukrani sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye ufundi anakuwa anawashonea watu pia, koneksheni ni popote.
it depend anashonea wapi ila vigumu sana fundi mshona nguo kuwa na connection kubwa zaidi atakuwa mtuma salam radioni na mtoa maoni kwenye vipindi vya leo tena clouds fm
 

asante kwa ushauri ila tz wanasiasa ndio wanatuangusha na ndio hao unaosema hawana elimu ila wanamafanikio ndio wanaoshindwa kuweka mazingira bora kwa vijana kuweza kwenda na ushindani wa soko la ajira elimu yetu ipo ipo tu uyu kijana kana kushona angejifunzia kipindi yupo shule

Kuna ugumu gani kijana alikiwa shule ya msingi darasa la sita akafanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na akifika sekondari baada ya kidato cha nne basi elimu ya ufundi iwe lazima kwa wahitimu wote baada ya hapo ndio vijana wajiunge na vyuo
 
Pamoja na bandiko lako lenye mrengo wa ki 'enzi za nyerere', embu tutolee mfano sasa ambao unaona ni njia sahihi ya msomi wa aina ya mwipwao kufanya hasa hizi za kujiajiri, maana 'white colour job' hazikamatiki.

Ulitegemea kazi za ujasiriamali mtaani zinafundishwa na ma profesa?

Ungelikuwa umepitia angalau Jkt, ungelielewa maana ya mkufunzi na mwanafunzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
We umesema nn na he hichi ili chia dola ndo ukichosomea?
 
Hili linaonesha pengo kubwa katika elimu yetu.

Nchi zilizoendelea kwenye elimu hata ushonaji una degree yake. Inaheshimika.

Tuseme mtu anayependa kushona anataka kusomea kushona mpaka level ya degree.

Kwa Tanzania atasoma chuo gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humu kuna watu twawaita ma GT ila ni wapumbavu kiasili na hawataki kuelewa ku ni wapumbavu.

kuna ubaya gani kufunzwa kazi na drs la 7, mimi nimefunzwa kazi na drs la 7 taasisi flani.Badae nikapewa kuwa msimamizi wao (wakati naenda pale wanajamii hasa marafiki walikuwa wananibeza badae tukikutana wananisifia bora kazi ndogo kuliko kukaa bure)

nimetoka pale nikachukuliwa na taasisi nyingine (inayo fanya kazi sawa na ile ya mwanzo wakanipa kitengo)

la saba ama asiyesoma kukufunza kazi ni kawaida sana,kazi inabaki kwako kujiongeza, kufanya kwa malengo na kujitoa pale.
 
Mimi nimeapa mwanangu nitamsomesha mpaka form 4 tu baada ya hapo namtafutia akasome ujuzi wowote hizi takataka za degree ni upuuzi mtupu hazina impact yoyote mtaani ili utengeneze pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…