Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Wapi ilipoandikwa kwamba mtu akiwa na degree lazima aajiriwe?
Wazazi wengi bado tuna mindset za kuwasomesha watoto wetu ili baadae waje waajiriwe.Ajira sasa hvi ni tatizo la dunia nzima. Hivyo kujiajiri ndiyo itasaidia kupunguza hilo tatizo. Na wakati mwingine kujiajiri hakuangalii una elimu gani na umesomea fani gani, ingawa naamini mtu aliyesoma anaweza kujiajiri na nkufanya vizuri zaidi kama atakuwa serious.

Kama huyo kijana ana passion ya kushona nguo anaweza akajiendeleza mdogo mdogo baadae akaja kuwa hata na kiwanda kidogo cha kushona nguo na hata akaajiri vijana wengine. MAISHA HAYANA FORMULA!
Mimi nashangaa sana watu kama wewe huwa mnakosa akili kichwani . Mfano watu 40000 wameliza vyuo katika fani mbalimbali Tz nzima na ktk hao kumi elfu wakawa wameajiliwa na thelathini elfu wakawa hawana ajira na wakaenda kuanzisha ujasiriamali . Nani atamuhuzia mwenzake .

Mfano 2.
Umemaliza course ya engineering hafu wote mkaenda kufungua construction company miaka miatu ujapata tenda utalipa Nini ada crb na kodi.
Kumbuka crb imedelete compuni nyingi sana mwaka huu kwa kushinda kulipa ada na zingine zimekufa kwa kukosa tenda .

Na compuni nyingi hazina mtaji wa kushika hata tenda za milioni Mia moja na zinaenda kwa kampuni za kigeni.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi na degree zangu mbili ni fundi seremala.
Tatizo lenu ujinga mwingi kwani fundi selemala au cherehani hajasoma? Unaweza kuwa seremala au fundi cherehani bila kusomea? Kwani Wewe na wenzio akiwemo mleta mara mnadhani uselemala na cherehani hausomewi Kama hausomewi kwa Nini mnaenda kufundishwa? Fundi cherehani kasoma .Elimu yake kasomea ufundi cherehani huyo meingine kasoma kasomea mambo ya community development.
Mleta mada kichwa Chako kibovu .
 
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?
Ifike mahali watu wakubali kuwa degree siyo guarantee ya kutoboa maisha. Ujuzi binafsi ni muhimu kuliko hayo madegree ya kukariri
 
Kwanza nimpongeze mpwa wako wa kuiona fursa. Hapo naweza kusema mpwao ndio ameanza kuitumia vyema elimu yake.

Mkuu, mpwa wako anaweza kujifunza ushonaji kibarazani akawa fundi mzuri akafungua ofisi kubwa tu na ikibidi ata kampuni ya ushonaji akatoa ajira kwa wengine lakini pia akalipa kodi na kulijenga taifa.

Kiongozi huyo fundi wa darasa la saba anayeshonea kibarazani kuna vitu anavikosa lakini huyo mpwa wako anaweza kuitumia elimu yake kuongeza thamani ya hiyo kazi akatoboa haraka sana.

Kama huyo mpwa wako yupo Dar, karibu na Kigamboni niunganishe nae mimi nitampa sehemu ya kujifunza bure na kumsaidia mawazo nini cha kufanya na anawezaje kupata mtaji wa icho anachotaka kufanya.
 
Tatizo lenu ujinga mwingi kwani fundi selemala au cherehani hajasoma? Unaweza kuwa seremala au fundi cherehani bila kusomea? Kwani Wewe na wenzio akiwemo mleta mara mnadhani uselemala na cherehani hausomewi Kama hausomewi kwa Nini mnaenda kufundishwa? Fundi cherehani kasoma .Elimu yake kasomea ufundi cherehani huyo meingine kasoma kasomea mambo ya community development.
Mleta mada kichwa Chako kibovu .
kenge wa kike wewe.

nimelalamika hapo au nimeelezea ninachokifanya???

mimi ni seremala na najivunia kuwa fundi seremala pamoja na degree zangu mbili.
 
Watanzania wanasoma ili serikali iwaajiri hiyo ndiyo shida
Asilimia kubwa ya wanaojilipua nje za
Nchi ni wasiosoma
Sasa serikali itaajiri wangapi
Me naona ni sawasawa tu wacha wajazanee huko mtaani itafika mahali nchi itakuwa na raia wanaojitambua



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa sasa hiyo kawaida sana. Kuna vijana walikuwa wanafanya field ninakofanyia kazi baada ya kuhitimu chuo na wamerudi mtaani na ukizingatia maisha tait siku ya siku nikawakuta madogo wako site wanapiga kibarua sidia fundi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahitaji ya dunia yanabadilika sana, Inatakiwa mshonaji ambae anaweza kumudu vitu kama lugha na matumizi bora ya mtandao namna ya kumudu masoko kidigitali zaidi kumpa huduma bora mteja ni ujuzi mwingine ambao hauji tuu ila kwa kipawa binafsi au elimu,na kucheza na soko linahitaji nini.

Atashona nguo lakini kwa kutumia elimu aliyonayo, na asiangalie kushona nguo tu afanye kwa malengo elimu iko pale kumsaidia kuongeza ujuzi wa hiyo biashara ndani ya miaka mitatu anaeza akawa tofauti kulinganisha na aliowakuta kwenye game au akapata mafinikio ya haraka hata kama si makubwa kiviile.

Issue ni kufanya hichohicho kitu kinachoonekana kawaida kwa namna tofauti ambayo huitwa ubunifu kwa lugha nyingine na ubunifu huanzia tangu mteja anapoingia hadi anatoka eneo la biashara na akitumia maarifa ya elimu aliyonayo ita msaidia zaidi.

kwa mwenye degree lazima ana ujuzi wa kompyuta basi eneo lake anaweka pc wateja wakija hata wanapata email za maendeleo ya nguo walizompelekea kutumia pinterest kucompare mishono ni vitu vya ubunifu tu si kazi rahisi .

Mteja ni kucheza na saikolojia yake, dunia inapobadili mweleko na wewe unageukia hukohuko hakuna namna.
Asante, kwa jibu hili nimepata wazo la kukusanya haya maoni nimwandikie summary nimpe kama nyongeza ya mchango wa mawazo kwenye mradi wake. Binafsi nilivyojaribu kujiweka katika nafasi yake nimehisi kama ningekuwa very frustrated, lakini kumbe kuna haya unayosema hapa ya kutumia elimu yake kufanya mradi wake uwe tofauti na wa wale ambao hawajasoma. Nakushukuru.
 
Ufikiri wa jamii, na wewe ukiwemo ndio shida, hakuna kazi za walioelimika na wasioelimika, shuleni huwa tunaenda kusoma ili kupanua mawazo yatakayo tusaidia katika kuendesha maisha yetu.

Sasa hizi degree tunasomea, mengi ni mambo ya utawala, ndipo unajikuta umesomea, utawala wa biashara, au maendeleo ya jamii, lakin, ni biashara gani unayoitawala? skills za hiyo biashara hauna, Au maendeleo ya jamii, je jamii inajihusisha na kazi zipi? hauna hiyo elimu.

Ni kweli kuna kashida kadogo kwenye mfumo wa elimu wetu, nao ni hako ka kuto incoroprate vocational training kwenye mafunzo yetu. Dogo kasoma, kaona anahitaji kujifunza cherehani, ili labda sasa aje atumie elimu yake ya chuo kikuu, kuendesha biashara ya cherehani, kwanza apatie mtaji,kisha ajikite huko. Wazo ambalo ni jema sana, na namuunga mkono 100%. Amini amini nakuambia, kwa moyo ambayo huyo dogo anaonesha, kuna kitu amekiona kwenye huo mchoro wake, na ndio manufaa ya elimu hayo. mwache aende, 5 years anaweza kuwa na story ya tofauti kuliko huyo fundi anaemfundisha? Je Haukusoma habari za mafundi vyerehani waliobahatika kutoka nchini mwetu hapa? Akina Speshoz, na Wengine, Kama Speshoz ni ana had masters kabisa, kaanza na kushona pia ila leo ana biashara kubwa ya fashion na sports. Sasa kwa nini kijana wa miaka 30, ndio anamikataba ya jezi kwa timu mbalimbali nchini, na ndo anaivalisha stars na Wasanii kama Diamondplatunuzm, anashina suti za harusi kwa bei karibu na mshahara wa miezi mitatu wa mwalimu mwenye degree? ni kwa sababu hakuwa fundi cherehani wa kawaida, nini kilimfanya asiwe fundi cherehani wa kawaida, ni Elimu yake ya masters. Na unajua ni kwa nini kwanini sio wote wenye elimu ya masters na hata wengine maprof hawaingizi mkwanja mrefu kama anaongiza yeye saivi? ni kwa sababu yeye nje ya Elimu yake ya mastars ana ujuzi, huo ujuzi ambao wewe unadhani dogo kapotea kuutafuta saivi. Ujuzi wa kushona.

So muache dogo afanye anachoona, na hayo ndiyo matumizi ya elimu.
Asante sana, this is very inspirational. Nakiri kuwa kwa kiasi fulani nimeathiriwa na hii mentality ya classes kwenye kazi. Dogo kaniingiza shule leo, na hili darasa litafika kwa wanangu.
 
Kasoma Art and community development, Sasa ushonaji sio Art kweli? Hapo changamoto ni hiyo kujifunza kibarazani locally but kama ameridhia mwenyewe sioni tatizo.

Kikubwa apate ujuzi wa kushona, kwa kutumia hiyo degree yake Sasa ndio ataboresha aina na mitindo ya mishono, Pia mashine za kushonea za kisasa zaidi na ofisi kubwa kama mbunifu wa mavazi badi kuwa na cloth line. Kwani kina Dickie's etc walianzaje?

Umeshindwa kumsaidia mpwa wako kwa hiyo decent job unayoiweza Wewe na bado unataka kuua ndoto yake ya kujikomboa? Jaribu kuwa na mawazo na mchango chanya kwenye mipango ya watu. Hakika baraka utaziona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimemsapoti kwa vingi, na hata kwenye wazo lake hili nimemsapoti pia na mtaji nimempa. Mafunzo anaanza kesho. Amenuia na anaonesha ana furaha juu ya huu mpango wake. Namuombea baraka na mafanikio.
 
Kuna mambo mawili inabidi serikali iliangalie kwa jicho LA tatu ilikupunguza changamoto hii,,,moja kupunguza umri was kustaafu,,pili kuna baadhi ya fani MTU afanye kwa mda mfano unafanya kwa miaka kumi zen wanakuja kundi lingine LA wasomi wanachukua nafasi na tatu uhamiaji watoe passport kwa wepesi ili vijana wakatafute fursa nchi za nje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom