Mtu Mwenye miaka 35 ni Kijana?

Mtu Mwenye miaka 35 ni Kijana?

Kuna ule wepesi wa mwili baada ya miaka 35 ni kama unaanza kuwa mzito, Putin bodyguards wake wale commandos wanakuwa replaced wakitimiza 35. Angalia hata michezo, bondia n.k

Lakini pia jinsi umri unavyokwenda ndivyo busara , hekima vinaongezeka huku nguvu ya mwili inapungua.

Hivyo kusema kijana kikomo ni 35 waliangalia zaidi ile physical fitness ya mwili, ndio peak yake ya juu kabisa kwenye graph baada ya hapo graph inaanza kushuka chini.
Ni kweli kabisa lakini 35 mpaka 45 mtu si bado yupo kwenye chart hasa kama ela ipo.
 
Ni mara nyingi utasikia mtu mwenye zaidi ya miaka 35 anajiita kijana. Wengine wana miaka 45 na zaidi hasa wanasiasa lakini wana jiita vijana.

Mnaonaje hili wakuu ni kwamba Ujana una makundi tofauti au ni huwa tuna/wana jifariji tu kujiita vijana ilihali wanajua wazi kwamba umri tayari umesha watupa mkono.

Wasalam.
Ujana ni big deal sana kwamba mtu akijiita kijana kuna kitu anawapunguzia?
 
Ila ni muda wakutoendelea kufanya makosa,ila ni muda wakurekebisha ulipokosea iwe ni mambo ya kifamilia,kiuchumi,mahusiano na malengo ya dhati katika maisha.🤔
Kabisa kabisa ni umri wa marekebisho na kutuliza akili sana.
 
Bongo ukiwa na hela hata ukiwa na 50yrs watakwambia bado kijana mdogo ila ukiwa huna Hela hata ukiwa na 24 watakwambia "ushakua Mtu mzima wewe jiongeze"
Dah maisha hayako poa. Ukiwa na ela unaitwa uncle bado kijana na umri ni 50 ila ukiwa na miaka 24 pesa huna shikamoo zina kuwa nyingi.
 
Ni mara nyingi utasikia mtu mwenye zaidi ya miaka 35 anajiita kijana. Wengine wana miaka 45 na zaidi hasa wanasiasa lakini wana jiita vijana.

Mnaonaje hili wakuu ni kwamba Ujana una makundi tofauti au ni huwa tuna/wana jifariji tu kujiita vijana ilihali wanajua wazi kwamba umri tayari umesha watupa mkono.

Wasalam.
Inategemea na muktadha husika

1. Kocha mwenye miaka 35 ni kijana kabisa ila mchezaji mwenye umri huo huo ni mzee

2. Rais mwenye miaka 50 ni rais kijana, ila angekua ni Askari huyo tayari ni mzee

Ndio maana sikushangaa eti Joketi naye ni UVCCM
 
Ni kweli kabisa lakini 35 mpaka 45 mtu si bado yupo kwenye chart hasa kana ela ipo.
Ni kweli mkuu..
Kama unakula vizuri, unafanya mazoezi, no stress na pesa ipo...Hata miaka 55 bado upo vizuri unless uamue kuzeeka mwenyewe.
Sean-Combs-rapper-clothing-line-fashion-world.jpg


Jamaa miaka 54.
 
Back
Top Bottom