Kipala
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 3,763
- 700
Mkuu, jaribu kujielimisha kuhusu matokeo ya utafiti wa sayansi. Siku hizi wataalamu hukubaliana kwamba Homo Sapiens (sisi sote) alianza Afrika na kusambaa kote duniani. Rangi si kitu sana kibiolojia; watu walibadilika katika mwendo wa miaka elfu nyingi.Awali ya yote ningependa kuwasalimu wanajamii wenzangu habari zenu, natumai ni wazima wa afya.
Nina maswali kadhaa ambayo ningependa kupata majawabu kutoka kwenu wana Jamiiforums yatakayo kuwa msaada na faida kwa jamii nzima na kubadili
taswira na mtazamo wa jamii nzima juu ya asili ya mtu mweusi [ mwafrika ] na uwepo wake hapa duniani.
Maswali:
1. Je mtu mweusi[ Mwaafrika ] ni uzao wa Adamu na Hawa ?
2. Je Adamu na Hawa walikuwapo pekee duniani ? na Afrika kulikuwa hakuna watu?
3. Je uzao wa mtu mweusi ni kutoka ndani ya Afrika au nje ya Afrika ? Na Kama ni kutoka nje ni kutoka kwa nani watu wa bara la Ulaya [wazungu], watu wa Mashariki ya Kati, watu wa Asia ya mbali au watu wa bara la Amerika?
4. Je inawezekana mtu mweupe kwa mweupe [ mfano mzungu kwa mzungu ] kuzaa mtu mweusi?
N.b: Matusi na lugha za kuudhi hazitakiwi , pia unaweza kuongeza maswali yako kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.
Maana rangi nyeusi-nyeusi ni kinga dhidi miale ya uruajimno (ultraviolet) inayosababisha kansa kwa watu wanaokosa rangi hiyo. Kinyume rangi nyeusi ya ngozi inapunguza uwezo wa kujenga "Vitamini D" mwilini hivyo watu weusi-weusi wana weza kuwa na magonjwa kutokana na uhaba huo wa vitamini D (hasa kudhoofika kwa mifupa tangu utotoni).
Hivyo watoto wenye rangi nyeupenyeupe kidogo walistawi vizuri zaidi katika maeneo penye Jua kidogo huko kaskazini.
Mengine ni kanuni zilizotambuliwa na Bwana Darwin na wanabiolojia / matibabu: waliofaa aidi kwa mazingira walistawi zaidi na hivyo kiasi ha "weupe" na "weusi" kiliongezeka polepole katika maeneo tofauti ya Dunia.
Hii utaona pia Uhindini Kusini penye watu weusi sana (wasiofanana na Waafrika) na kule Amerika karibu na Ikweta.