Danganya watoto wadogo wenzio. Sisi watu wazima tunajua jinsi lugha, hata kama ni Kisukuma, inavyoweza kusaidia. Lugha ni muhimu sana kwenye kupata kazi international ambazo zinalipa vizuri.
Sisi tuliobahatika kutembea nje, unakutana na Waganda, Wakenya, Wanigeria... Watanzania ni shida kuwapata nje. Lugha inatuangusha. Mtanzania akifika Dar anaona amemaliza dunia, anatafuta kiwanja Chamazi, anajenga, ananunua Rav4, anaanza kula ugali hapo huku siku zikienda. Ukoo mzima unamwona tajiri. Na yeye akipigiwa simu za kuombwa 5,000/= kutoka kijijini anajiona amefika kileleni.
Kuna maisha zaidi ya Dar na kuna kazi zinalipa vizuri huko nje lakini lazima lugha za kigeni zipande hasa Kiingereza.