Sio kitu cha mchezo, ni zoezi linalohitaji mabadiliko ya almost kila kitu, seikali inakwepa hiyo gharama.Hivi inamaana hatuwezi kubadilisha mitaala ya hizi shule zetu ziwe kama za kimataifa. Najiuliza tu. Kwani hatuwezi au ni nini shida
Pia angesema baada ya hiyo PhD amefanya nini cha maanaUnajifariji tu. Scholarship unapata lakini haina maana kuwa ubora wako uko kama wa graduate wa IST. Walimu wanafundisha hapo chuo kikuu lakini hawawezi kujieleza kwa Kiingereza na wamepata maskolaship za UK, US, Australia.. wamefanya PhD nk huko.
Umekuwa mbongo toka lini??
Geza Ulole njoo umuone mtu wako
Danganya watoto wadogo wenzio. Sisi watu wazima tunajua jinsi lugha, hata kama ni Kisukuma, inavyoweza kusaidia. Lugha ni muhimu sana kwenye kupata kazi international ambazo zinalipa vizuri.
Sisi tuliobahatika kutembea nje, unakutana na Waganda, Wakenya, Wanigeria... Watanzania ni shida kuwapata nje. Lugha inatuangusha. Mtanzania akifika Dar anaona amemaliza dunia, anatafuta kiwanja Chamazi, anajenga, ananunua Rav4, anaanza kula ugali hapo huku siku zikienda. Ukoo mzima unamwona tajiri. Na yeye akipigiwa simu za kuombwa 5,000/= kutoka kijijini anajiona amefika kileleni.
Kuna maisha zaidi ya Dar na kuna kazi zinalipa vizuri huko nje lakini lazima lugha za kigeni zipande hasa Kiingereza.
Je, hao waliosoma International schools wamelisaidia vipi taifa?
Mbona mimi nimesoma Kayumba na nimeenda kufanya kazi nje kwenye hizo nchi ulizozitaja.
Na hata sasa hivi kazi zangu ninazoomba ni za nje na nacompete na watu wa mataifa mbalimbali na hapo utasemaje?uoga wenu ndio umaskini wenu,ni confidence tu ndio inawaangusha watu hakuna kingine
Hawa mbona wana branches zao kila mahali duniani na pia wanaajiri watu wa aina zote.Wanaisaidia dunia, ndio maana wanaitwa international. Wako UN, WB, WHO, UNICEF... Sijui kama unaweza kuwapata Halmashauri ya Wilaya ya Bahi hawa.
Wanatakiwa kufanya kwenye national level ili kuinua taifa, that's my opinion. Kama tuna wahitimu katika level ya kimataifa lakini maisha yetu bado duni, kuna faida gani hapo?Wanaisaidia dunia, ndio maana wanaitwa international. Wako UN, WB, WHO, UNICEF... Sijui kama unaweza kuwapata Halmashauri ya Wilaya ya Bahi hawa.
Nimesoma Kayumba pia. Hivi ninavyoandika niko nje ya Tanzania. Mimi mmoja kuwa nje, haina maana kuwa ni rahisi kwa Watanzania wote waliosoma Kayumba kuja kufanya kazi nje ya Tanzania. I am NOT the typical Tanzanian. Kama haujajifunza Kisukuma, confidence haiwezi kukufundisha Kisukuma. Hauwezi kusimama mbele ya watu eti kwa vile una confidence, ukafanya interview katika Kifaransa wakati haujawahi kujifunza kifaransa. Huo ni uongo na ubishi usiokuwa na maana.
Tupe asilimia. TID anawakilisha % ngapi ya watoto waliopita international school? Mimi sina pesa tu ya kupeleka huko wanangu. Ningekuwa nazo ningepeleka huko.
Hawa mbona wana branches zao kila mahali duniani na pia wanaajiri watu wa aina zote.
Ni kichwa chako tu pamoja na connections za wajanja wa mjini unaweza kupata kazi kwa hawa jamaa acheni kudanganyana.
mkuu hata hao watu wenye kipato si kwamba wanapeleka watoto huko sababu ya ubora wa elimu,au wana malengo ya juu sana na watoto wao.laaa
sababu ni kwamba wanaona kayumba hazilingani na hadhi walizonazo.kwanza hao watoto hawako kwenye utegemezi wa ajira baada ya kuhitimu.huwezi mlipia mtoto ada ya milioni 45 kwa mwaka,eti aje aajiriwe kazi za milioni mbili kwa mwezi.
kwahiyo mkuu,tubadili hata namna ya kufikiri tu hata hapa tulipo,kuna watu elimu sio nyenzo ya ukombozi wa maisha yao tena,ila ni sehemu tu ya maisha.
mkuu hata hao watu wenye kipato si kwamba wanapeleka watoto huko sababu ya ubora wa elimu,au wana malengo ya juu sana na watoto wao.laaa
sababu ni kwamba wanaona kayumba hazilingani na hadhi walizonazo.kwanza hao watoto hawako kwenye utegemezi wa ajira baada ya kuhitimu.huwezi mlipia mtoto ada ya milioni 45 kwa mwaka,eti aje aajiriwe kazi za milioni mbili kwa mwezi.
kwahiyo mkuu,tubadili hata namna ya kufikiri tu hata hapa tulipo,kuna watu elimu sio nyenzo ya ukombozi wa maisha yao tena,ila ni sehemu tu ya maisha.
Ni kweli mkuu maisha sio kukariri.
Ndio maana kuna swali niliuliza mwanzoni je kuna watu wale wanaomiliki mabus na magorofa kariakoo walisoma International schools?hakuna aliyenijibu
Arguments zao zinaonyesha wazi kuwa umesoma Kayumba. Na bila shaka wewe ni mwana-CCM. Hakuna mtu mwenye record ya elimu ya watu wanaomiliki maghorofa Kariakoo hapa. Nadhani hata serikali haina. Kama unazo tupe basi.
"Ukiwa na hela peleka international school"
Hii statement tu inatosha kusema mfumo wa elimu nchini ni mbovu kabisa. Haiwezekani elimu ibague walio nacho na wasio nacho, pia hii ni proof kuwa sisi ni masikini, the haves and have-nots ndio inafanya tuwe na Kayumba Vs international. Otherwise tungekuwa kama Finland au Scandinavian countries na mifumo bora kabisa ya elimu ambayo hata mwafrika akienda huko anasoma beeee(bure)
Majority ya watu wanaomiliki mabus na magorofa hawana hayo makaratasi yenu na wanaongea kiswahili tu kiingereza ni kwa mbali sana
We umewaona wapi hao international scholars, ushawaona kwenye hizo ajira za halmashauri au kariakoo wanamiliki meza?Lakini mbona kibongo talent nyingi zinatoka kwa watu ambao ni masikini na wasio na elimu kubwa
Mbona hatuoni hao international wakiongoza kwenye fani nyingi zinazotumia vipaji sana
Haongelei asilimia 1 ya watz, anaongelea wote! Wanagapi wanapata fursa kama yako?Mbona wengine tumesoma hizi hizi shule za sirikali, tena shule ya msingi kijijini kwa babu kuongea kilugha mwanzo mwisho lakini tumefanikiwa kupata scholorship kusoma Masters na PhD kwenye international universities ambazo zipo kwenye world ranking ya 10 bora, what happened?
Wanatakiwa kufanya kwenye national level ili kuinua taifa, that's my opinion. Kama tuna wahitimu katika level ya kimataifa lakini maisha yetu bado duni, kuna faida gani hapo?