Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Nina mashaka kama umesoma. Ungekuwa umesoma na kuelimika ungegundua mwanzisha mada hakusema kuwa wote wanaosoma huko kajamba nani wanaishia pabaya ila ameongelea zaidi wenye chance kubwa.
Ok! utagundua kwamba wengi wanaosoma huko ni watoto wa wakubwa hivyo ni lazima wawe na chance kubwa.
 
Hivi maadili ya kitanzania ni yapi hasa, ambayo hao wazungu hawana?

Manake naona wenzetu wana maadili kuliko sisi, Sisi tuna uvivu mwingi, hatujali muda, wizi wizi tukipewa nafasi n.k

Labda maadili ya kimaskini ndio tunayo.
Huu ushoga ndo maadili ya kitajiri...
 
Huwezi kufaulu katika viwango vya juu kama huna hizo analytical skills, hakuna mitihani inayotungwa kwa ajili ya wanafunzi wanaokariri labda ujitungie mwenyewe.
Wanafaulu owa ukariri shule hasa hizi za binafsi zinakarrisha Sana wanafunz
HAKUNA kabisaa analytical skills
Pia curriculum ya Tz NI exam based Kama hujui had mjengi mtoto kujitegemea hata mitihani inayotungwa na ufundisaji kwa ujumla kunapenga kumsaiidia mtoto kufaulu mtihani
Watoto wanatankiwa kuangalia Katika nyanja tofauti Kuna talents ,creativity nk acha ubishi

Mwaka Jana nimeshhidia watoto wamedisco pale udsm Tena form six walikuwa na div one kaliii
Shida wanakadirishwa


Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwani University ni lazima ziwe za bongo, tatizo lako unakariri na unaonekana kabisa uko brainwashed, sawa nimesoma za sirikali at the basic level but kwenye University with International reputation..vp wewe..
 
Unajifariji tu. Scholarship unapata lakini haina maana kuwa ubora wako uko kama wa graduate wa IST. Walimu wanafundisha hapo chuo kikuu lakini hawawezi kujieleza kwa Kiingereza na wamepata skolaship za UK, US, Australia.. wamefanya PhD nk huko.
Cc. Mzee wa chatu.
 
Tatizo lipo kwa wanafunzi wengi na hao unakuta hawasomi hata vitabu kupanua uelewa wao, muda mwingi ni kusolve past papers. Kwa hiyo nakubaliana na hoja kwamba elimu yetu inawaandaa zaidi vijana kufaulu mitihani.
 

That is true. Nimegundua tatizo la kujieleza ni kwa Watanzania wengi sana . Sio kwa Kingereza wala Kiswahili, changamoto kubwa sana.
 
Tatizo hizi international schools hata watoto wa kiume wanakua kama madem tu sijui kwanin au ndo mitaala yao.
Mkuu sio wote, ila shule haziingili someone privacy mfano hizo mambo na dini (japo kuna int'l za dini kama HOPAC) japo kuna dogo wa HOPAC way back alitoa speech ya kuhamasisha ushoga kwenye international day guess ni mwakajuzi, ikabidi shule ikanushe vikali ,

ila kuna wengine wahuni tu na wanaishi maisha ya starehe full kushinda beach usiku kucha na girls wakizungu, kuvuta bangi na pombe kali.....waliograduate IST mwaka jana watakuwa wanamjua Erick alisoma Art ya kuchora macartoon na kundi lake....zile fantasy zao na kujiona migos ni balaa....
 

[emoji23][emoji1541]

1. Kwa kuwa umesema hutoweza, hakika hutoweza.
-
2. Hata ukiweza, hutoweza.
 
Mzee,laiti kama Dr. Mahera akiligundua jina lako unalogombea hakika hutatokea kwenye karatasi za kura.
 
Mimi naona mitaala ya kufundishia maana walimu waliotoka vyuo vyetu nao hufundisha hzo shule wakutoka nje ni wachache Sana,
Upo sahihi kabisa kuna mtu kasema eti walimu wa Tz ni assistant teachers kwa kuwapeleka watoto chooni.....hajui 70 ya walimu wa international school ukitoa IST ambayo sijui ni pure Tanzanians....

Kuna waTanzania wanafundisha ila sio A-levels nafikiri (wakufundisha A-levels wapo wachache) ila kuanzia PYP inayohusisha Nursery na MYP....nimetaja Nursery hapo ili kuonesha waTz wanafundisha Int'l schools maana wazungu wanaheshimu sana miaka midogo na elimu ya mtoto mdogo maana wanajua ndio age ambayo mtoto atajifunza vitu vingi vitakavyomshape..... Hii inaonesha they trust Tanzanians

Montessorry wanayotumia international schools kwa watoto wadogo mbona inafundisha na vyuo vya dar tena kimoja kinaitwa Montessory kabisa....

Ulikuwa sahihi kabisa madam.
 
We umewaona wapi hao international scholars, ushawaona kwenye hizo ajira za halmashauri au kariakoo wanamiliki meza?
Kutokana na shule zao kukuza vipaji nilitegemea kuwaona wakiipeleka bongo movie international, music, mpira na fani nyingine nyingi ila siwaoni humo
Je ni vipaji gani vinakuzwa humo
 
Kwani University ni lazima ziwe za bongo, tatizo lako unakariri na unaonekana kabisa uko brainwashed, sawa nimesoma za sirikali at the basic level but kwenye University with International reputation..vp wewe..
Uandishi wako unatia mashaka, hata shule unazosema umeenda nina mashaka kama ulienda.

Anyway, sawa msomi wa university with international reputation.
 
Mkuu kwanza waliosoma International school 80 target yao ni kusoma International Universities na wakifaulu vizuri A-levels na kuwa assessed kwenye CIA wanaenda hizo Versitt za nje ....

hao wachache wanaobaki basi unakuta wamepoteza passion kutokana na kuhisi wameshuka standard hata masomo yatakuwa tofauti maana mfano kuna wanaosomea Art ya kuchora mavinyago na macartoon hao ukimleta atachagua masomo yasio preference yake...
Mimi sizikubali sana hizo international school kwasababu mkifika Chuo kikuu,hakuna Significance difference ya wale waliosoma St.Kayumba na waliosoma International.
 
Ukisomesha mtoto hizo international schools unamuandaa aje aajili watu na siyo kuajiliwa,
Tofauti na shule zetu hizi mtt ukimaliza watu wanakaushari kasake ajira
 
Mdogo wangu anasoma hapo Montsory mkuu, kwahiyo akimaliza atabahatika kupata kibarua au sio??
 
Huwezi kufaulu katika viwango vya juu kama huna hizo analytical skills, hakuna mitihani inayotungwa kwa ajili ya wanafunzi wanaokariri labda ujitungie mwenyewe.
Unaweza. Na ndiyo wafaulu wengi Tanzania wanavyofaulu. Nimesoma shule za Tanzania na za nje ya Tanzania hivyo niliona tofauti ya ufundishaji, ufanyaji mitihani na uelewa wa wahitimu.
 
Ok! utagundua kwamba wengi wanaosoma huko ni watoto wa wakubwa hivyo ni lazima wawe na chance kubwa.
Kuna correlation kubwa kabisa kati ya watoto wa wakubwa vs elimu nzuri vs chances nzuri. Hivi vitu vinaendana ndugu yangu. Kumbuka mimi sisemi kuwa watoto wanaosoma shule za kawaida hawaina akili bali nasema aina ya elimu wanayoipata siyo nzuri. Shule nyingi za Tanzania ndiyo zilivyo na ndiyo maana unaweza kukuta mtu amesoma mpaka akapata Phd tena kw kutumia lugha ya kiingereza lakini anashindwa kujieleza kwenye mambo ya kawaida kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…