Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mdogo wangu anasoma hapo Montsory mkuu, kwahiyo akimaliza atabahatika kupata kibarua au sio??
Kuna vitu vidogo vidogo lazima awe vizuri yeye kama yeye mkuu ajue kujieleza, ajue montessory na mising ya montessory, ushauri wangu anaweza anza kwenye shule za kawaida akafanya kazi miaka 3 (ninauhakika atapata tu) alafu anaapply na international school kutokana na uzoefu Mungu akisaidia atapata....

So ni ndiyo mkuu kuna possibility kubwa atapata, sijapita huko kujua uwezo wao ila ninachojua montesorry inatumika int'l School na wengi wanaofundisha watoto sio pure from montessory college ni wale waliofundishwa tu baada ya kusoma vyuo vya kawaida....
 
Ni kweli mkuu maisha sio kukariri.
Ndio maana kuna swali niliuliza mwanzoni je kuna watu wale wanaomiliki mabus na magorofa kariakoo walisoma International schools?hakuna aliyenijibu
Unaweza kuta wanajua kuandika majina yao tu si vinginevyo
 
Lakini mbona kibongo talent nyingi zinatoka kwa watu ambao ni masikini na wasio na elimu kubwa
Mbona hatuoni hao international wakiongoza kwenye fani nyingi zinazotumia vipaji sana
Issue sio kuongoza issue ni kum expose mtoto na ulimwengu
 
That is true. Nimegundua tatizo la kujieleza ni kwa Watanzania wengi sana . Sio kwa Kingereza wala Kiswahili, changamoto kubwa sana.
Nationalism is an infantile disease. It is the measles of mankind

- Albert Einstein.

Siko hapa kwenye squabbles za Wakenya na Watanzania.

Najieleza tu.

Watanzania tuna lugha yetu tunaelewana wenyewe.

Hii inawezekana East Africa nzima ipo, lakini Tanzania nimeona sana. Labda kwa sababu ndipo nilipozaliwa na kuishi sana.

Haya ni baadhi ya matatizo, haijalishi mtu ana elimu vipi, mara nyingi sana yanajitokeza.

1. Kuongea bila kumaliza sentensi. Kuanzia mtoto mpaka rais, si ajabu kukuta mtu anaongea, halafu anaachia sentensi inaelea hewani bila kuimalizia. Sasa sijui ni aina mahsusi ya mawasiliano au ni mapungufu.

2. Kuongea katika namna ambayo mawazo hayana mpangilio. Mawasiliano bora yanajali mpangilio. Hoja inaanza kutambulishwa, maana za kiini cha hoja zinanyambulishwa, halafu maelezo mengine yanafuata. Tanzania si ajabu mtu akarukia mwisho wa hoja hata bila ya kuitambulisha.

3. Watu kuchukulia kirahisi tu kwamba mtu mwingine anajua wanachozungumzia kama wanavyojua wao. Hili linachangia sana tatizo namba 2 hapo juu.

4. Kujadili mambo kwa ushabiki, mahaba na hashuo badala ya kuangalia hoja. Watu wanachukua upande kama ushabiki wa timu za Simba na Yanga, halafu, baada ya hapo, watafanya kila hila upande wao uonekane ndio bora. Bila kujali hoja. Iwe kwenye siasa, dini, kujadili nchi, na kadhalika. Hapa utakutana na logical non sequitur zote, ad hominem attacks zote, deus ex machina zote, ili mradi mtu ashinde mjadala tu.

5. Non verbal communication. Hili ni janga la kitaifa. Unaweza kukuta rais anahutubia taifa, hapo hapa anajishika pua kama anataka kupenga makamasi.

6. Mikingamo katika dhana. Jana nilikuwa namsikiliza jamaa mmoja shabiki wa timu ya soka ya Yanga. Anasems anataka mambo yawe fair, Yanga ipewe nafasi ibebwe kwa sababu Yanga ilipigania uhuru wa nchi. Yani hapo hapo anasema anataka mambo yawe fair, hapo hapo anasema anataka Yanga ipendelewe. Haoni contradiction hapo. Kauli kama hizi kwa Watanzania si kitu cha ajabu. Hata siasa zetu za "Ujamaa na Kujitegemea" ni contradiction. Ujamaa maana yake ni kutegemeana, na kutegemeana ni kinyume cha kujitegemea, hivyo "Ujamaa" na "Kujitegemea" ni vitu vinavyopingana. Sisi tunaona sawa tu.

7. Kukosa uwazi. Mawasiliano ya Watanzania wengi yametawaliwa na hila na kukosa uwazi. Ama kwa sababu wengi hawana uwezo wa kuchambua hoja na kuiwakilisha vyema, ama kwa sababu hata wenye uwezo wa kukwambia kitu ambacho wanaona hutakipenda, huenda kujipendekeza, kutaka suluhu ya uongo, kueleza mambo yao kama utani na dhihaka, na kadhalika. Kwa Watanzania wengi ni bora akukubalie jambo bila ridhaa ya kweli, halafu akusengenye pembeni, kuliko akuambie ukweli na kukukatalia jambo mbele yako.

8. Kasumba/Generalization/Stereotyping.
Watanzania wakitaka kuoa wengi wanaanza kuuliza "kabila fulani tabia zao zipi?". Hili tatizo la ukabila hata Kenya lipo, tena zaidi.Bora yetu, huko hata kuoana makabila tofauti nafikiri bado ni mzozo. Ila Tanzania watu wanaishi kwa kukariri sana na labda kwa kiasi fulani kuna mantiki, lakini imezidi sana. Mpaka inaharibu mawasiliano. Kwa sababu mtu kabla hajawasiliana na kujua ukweli kashaweka dhana Wachaga wezi.
Kuna hotuba moja ya rais Magufuli aliletewa kesi ya Mchaga akasema nyie mlitegemea nini, huyo mtu ni Mchaga, akimaanisha kuwa walitakiwa wajue Wachaga ni wezi. Halafu nchi hiyo hiyo kuna watu wanajisifia kinafiki haina ukabila. Yani kwa watu wengine ukiwa unaishi nje wewe ni beberu tu. Cha ajabu, wewe beberu wakipata matatizo wanakufuata kukuomba msaada! Hapa tqtizo la kasumba limechanganyika na tatizo la namba 6 la contradiction. Wao wanaona sawa tu.

9.Kutotaka kujifunza. Watanzania wengi unaweza kuona mtu kakosea, ukamsahihisha. Tena kwa heshima tu, iki asikisee tena sehemu mbaya zaidi. Mwenzako anakwambia "Si umeelewa tu?". Yeye ukweli kwamba kakosea na anatakiwa kujifynza si kitu muhimu. Anakulazimisha wewe uwe umeelewa hata alipokosea.

10. Uzalendo wa kijinga. Watanzania wengi serikali inawapiga, inawatukana, inawanyanyasa. Lakini wanaitetea bado kwa "cognitive dissonance" ya " my country, wrong or right".

Si Watanzania wote walio hivyo. Tuna watu sharp wengi. Watu wanafunguka macho. Upinzani unakua.

Lakini naona kama majority ndiyo wako hivyo. Kibaya zaidi wengine wengi ni watoto wa mjini ambao walitakiwa kujua zaidi.

Before you gleefully gang on us with vitriolic schadenfreude, let it be known that I am a country agnostic equal opportunity offender and I can dish the same ten point harangue on Kenya.
 
Tofauti huwa ni kubwa sana kati ya mwanafunzi mwenye uelewa wa kawaida na yule mwenye uelewa wa juu. Yeye atatumia nusu saa kuelewa material ambayo wewe itakubidi kukesha ili uambulie chochote..
Huo uelewa mnaupima vipi? Maana hata mimi nimesoma special school ilboru sec tena advance na nikatoka na 1 ya mwisho mwisho huko , sasa mkuu kwa taarifa tu ni kwamba hakuna tofauti kati ya anaesoma special school tena hapa bongo na yule asiyesoma special school ni kwamba wengi tuliosoma shule hizi zinazoitwa special ni tuna mentality ya u superior wakati wote tunameza kwa ajili ya necta tu na chuo mnakutana na mwenye three yake safi na wote mna mkopo na wote tena mnaeza mkawa mnasoma course moja.
Special school mbele sio hapa bongo.
 
Mtu ukiwa na hela ya kueleweka ama kama unataka kuwekeza kweli kwa watoto wako, wasomeshe international schools au shule zenye mitaala ya kimataifa.

Hizi shule zenye mitaala ya kimataifa zinawajenga watoto kwenye analytical skills, reasoning, logic, creativity, competence na mambo kama hayo.

Ukikutana na mtoto wa darasa la 6 wa hizi shule, reasoning yake ama analytical skills zake ni sawa na kijana wa form six wa necta schools.

Shule hizi hazilengi kuona mtoto anapata nini au maksi gani darasani bali kuibua talents nyingine alizonazo mtoto sio hizi za necta ambazo zimejikita kwenye ufaulu tu wa mwanafunzi.

Ukitaka kuwekeza kwenye elimu ya kweli kwa mwanao na kama uwezo upo peleka mwanao shule zenye mitaala ya kimataifa.
Wakimaliza hizi shule wanaenda kukutana vyuoni, UDSM,SUA,UDOM, nk.Umekwepa nini !!Mwisho wa siku wote wanaajiriwa na TAMISEMI au VODACOM. Au wanaenda kufanya kazi international mkuu hawajiliwi hapa? Kama sivyo haina haja.Af Dunia ya sasa imejikita katika teknolojia kama AI, Big data, Robotics nk hapo sijaona makuzi ya kitknolojia.
ELON MUSK baada ya kugundua mtaala was marekani hauwajengi watoto wake kiteknolojia ameanzisha shule take na walimu anaowataka.Kwa hio hizo inter.. Hazina jipya.
 
Unaweza kuwa umefika huko lote lkn reasoning yako ikawa bado chini tu.
Mbona wengine tumesoma hizi hizi shule za sirikali, tena shule ya msingi kijijini kwa babu kuongea kilugha mwanzo mwisho lakini tumefanikiwa kupata scholorship kusoma Masters na PhD kwenye international universities ambazo zipo kwenye world ranking ya 10 bora, what happened?
 
Mbona wengine tumesoma hizi hizi shule za sirikali, tena shule ya msingi kijijini kwa babu kuongea kilugha mwanzo mwisho lakini tumefanikiwa kupata scholorship kusoma Masters na PhD kwenye international universities ambazo zipo kwenye world ranking ya 10 bora, what happened?
Ni mmoja kati ya wangapi? fanya upembuzi then utajua wangapi wanapotea njiani
 
International School tambua watoto wengi huwa hawaendi kutafuta kazi, kule watoto huwa kwa sababu wanajengewa confidence kubwa sana huweza kutunia vipaji vyao kuishi,.

Na pia wanapata Exposure kubwa sana, Exposure ina nguvu sana kuliko elimu, watoto wa International School kwanza unakuta rafiki zao Baba zao wana miliki ma investment ya kufa mtu, Wewe fikilia nakutana na mtoto wa Mengi au MO shuleni, yaani tiyari pale hutakuwa na mawazo ya kwenda kutafuta kazi.

Hapo ume-exaggerate sana, sijajua kama ulikua unanogesha ngano yako au lah. Ni kweli hizo shule ni nzuri hasa hasa kumpa mtoto exposure na kujifunza lugha zingine kwa ufasaha kama kiingereza au kifaransa.

Ila ukija ktk uwezo wa utendaji na ufanisi sio kweli hao wanatuzidi ila wao kwa asilimia kubwa wanaonekana wako smart ni kwa sababu wanakuwa wanajifunza kwa lugha za kigeni tangu awali. Kama ukichanganya mtoto aliyesoma shule msingi Bunge na shule ya kimataifa ya Tanganyika uwapime uwezo wao kwa lugha ya kiswahili utahamaki ukweli wa mambo, ni ngumu sana mtoto anayesoma lugha ya kigeni kwa kugusa gusa awe sawa kwa kujiamini na mtu aliyesoma shule ya kimataifa kwa lugha ya kigeni.

Binafsi nimesoma shule za umma kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu, nimebahatika kufanya kazi na watu waliosoma shule za kimataifa kama Tanganyika na Moshi pia vyuo vikuu wamesoma Ivy league (Harvard, Princeton, Brown) ila sijawahi kuona utofauti mkubwa baina yao na sisi. Jaribu kwenda ofisi kama World bank country office (Mirambo 50) au auditing firms (Kpmg, delloitte, EY, PwC) au oil & gas companies huwezi kuona utofauti baina yao na sisi.

Changamoto kubwa sana niliyoigundua asilimia kubwa ya watu ambao waliosoma shule za umma kuanzia chini mpaka vyuo vikuu ni kupata shida kuimudu lugha ya kigeni kwa ufasaha hii hupunguza hali ya kujiamini kwa kiasi kikubwa sana. Labda serikali wajaribu kuboresha mitaala ya elimu lugha ya kiingereza ianze kutumia kuanzia chini yaani shule ya msingi na sio kuanzia sekondari. Watumie mfumo unaotumika kwa shule za msingi kama Bunge, Mlimani na Olimpio.
 
Mkuu kuna world scholars kibao ambao hawajakanyaga hizo international schools na wanaheshimika kwenye field zao. Nafikiri hizo shule zimeanzishwa purposely kwa ajili ya watoto wa mabalozi kwenye nchi husika, hakuna jipya...
Upo sahihi kabisa mkuu. Lengo la shule kama IST ni watoto wa foreigners
 
Ach ujinga wale hawaandaliwi kiwa wafanya kazi, sio kama nyie mnawaza kazi masaa 24, wale asilimia kubwa sana huja kuwasaidia wazazi wao,

Mule watoto hawafundishwa eti waje kuwa sijui Mameneja huo ujinga uko kwenye shule za kajamba nani
Talent ni nini
Na wewe ndiyo utupe mifano ya hao ma international scholars waliokuzwa vipaji vyao mashuleni kwao tuwaone kitaifa na wawe wakubwa kimataifa sio kusifia tu hizo shule nadhani wengi wao wanaishia ama kusimamia biashara za familia zao au kupewa nyazifa kwenye serikali ambao labda wazazi wao ni viongozi na wengine kuajiriwa nje huko ambayo inawakuta hata waliosoma shule za kata na ku scholarship

Lakini katika mpira, mziki, uigizaji, ngumi,dancerz na vipaji vingine vingi ni akina sisisi tu na Kama ukimkuta huko
Aliyesoma international kwenye familia huwenda wanamuona Kama kapotea vile
 
Back
Top Bottom