Uwezo wa kuajiri wengine unaweza kuwa ni kigezo kimoja wapo maana hata huko nje tunakokusifia si kwamba kila mtu kajiajiri. Lakini pia na wewe unaweza kuleta vigezo vingine na kuvijengea hoja badala ya kusema tu nilichoandika mimi hakitoshelezi.
Kuhusu IST kuwa msaada kwao binafsi na familia zao, hayta wa Kayumba pia ni msaada kwao na familia zao kwa uwezo wao. Je tuishie kuwa kila mtu asome kwaajili ya maendeleo yake binafsi na siyo ya jamii? ndio purpose ya elimu?
Hoja yangu ilikuwa ni vigezo gani wanavyotumia kusema elimu hiyo ni bora zaidi (ukiacha uwezo wa kujieleza kwa kingereza). Nimewafikirisha tu kwamba angalau tutumie kigezo cha uwezo wa elimu kutatua matatizo yaliyopo kwenye jamii ya Tanzania whether imepatikana international au Kayumba. Kama elimu ya intenational haiwezi kutatua changamoto za jamii kama hii ya Kayumba maana yake ni kwamba Tanzania kama nchi tutazidi kuwa masikini. Elimu yoyote ile ingekuwa bora zaidi kama ingeweza ku deal na matatizo yaliyopo kwenye context yetu sisi waTanzania. Ni mtazamo wangu tu.
I hear you Mkuu venine.
Huu ni mtazamo wangu wa elimu ya IST.
Sijasoma kujaribu kutatua matatizo ya nchi. Bali nasoma kujielimisha, kujua kupanga fikra zangu vizuri, kupanua ubongo wangu kielimu, kuandika mawazo vizuri, kuwasiliana vizuri na wengine kwa lugha za kigeni na kadhalika. Kujiajiri au kuajiriwa sio lengu la elimu kwa mtazamo wangu. Elimu ni kufunguo ubongo wako utumike vizuri.
Pia, kwenda Harvard au vyuo vingine vya ivy league haimaanishi kuwa utatajirika ukihetimu. Hii inategemea na mtu kwa mtu. Kuna rafiki wanafanya kazi non-profit org na wanaishi maisha ya kawaida sio ya kitajiri.
Pia inategemea na somo ulilisoma.
Mhitimu wa Filosofia na mhitimu wa Biochemistry kama wakiamua kuajiriwa, mmoja atapewa mshahara mkubwa zaidi kuliko mwingine japokuwa wote ni wahitimu wa Harvard.
Vile vile, Mfilosofia anaweza kuandika vitabu au kufungua biashara inayoweza kumtajirisha kuliko mhitimu wa biochemistry.
Inategemea unataka nini katika maisha yako.
Binafsi, faida kubwa ya elimu ya IST zaidi ya serikali au private school nyingine ni networking.
Alumi Association ya IST inakufungulia milango kila kona ya dunia. Unakutana na wanafunzi wa nchi 100, wanarudi kwao, wanakuwa mabalozi, mawaziri, CEO wa makampuni, billionaire, madaktari na kadhalika.
Kwa Tanzania, unasoma na watoto wa watu muhimu Tanzania.
Kama una shida ya kibarua watakusaidia kwa mikono miwili iwe New York, Tokyo au DR Congo. Ukihitaji kufungua biashara au kuuza kitu nchini kwao, watakusaidia vile vile.
This network is priceless.
Binafsi, sioni kuwa Mzalendo ni kufanya kazi Tanzania kwa kutumia elimu niliyopata. Nikipeleka pesa za kigeni katika benki ya Tanzania pia ni uzalendo. Uzalendo pia unakuja rahisi baada ya kushiba, sio kabla.
Haya ni maoni yangu na sitegemea wewe utakuwa na mtazazo kama wangu.