PostGE2025 Mtu umechoma, umeiba, umeharibu mali za watu, ugomvi ukaibuka, wenzio wakafa sasa serikali imekosa nini?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hii desturi ya kuilaumu serikali kwa Kila jambo linalotokea katika jamii si sahihi, mzazi/MLEZI ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunatoa malezi yakutosha kwa watoto wetu.

Mtoto akue akijua kuwa WIZI haufai matokeo yake ni kifungo/kifo, ajue kuwa matusi hayafai, ajue kuwa tamaa na wivu Mali za watu haifai...haya mafunzo yatolewe kwa watoto wangali Bado wadogo na yaambatane na motivation & reinforcement.

Sahzi kumekuwa na desturi unakuta kitoto kidogo kinaongea ngono mwanzo mwisho halafu anatokea mla donation mmoja wa ufipa anailaumu serikali....this is childish.
jitu litoke kwao lije kulipua kituo cha mafuta eti ndio linadai haki halafu lichekewe tu?

hiyo ni nonsense,
ni gaidi huyo lazima awe eliminated 🐒
 
Mwanadada akiwa na mwanaye kwenye gari kapigwa risasi leo anaitwa kibaka?

View attachment 3700776

Master Tindwa akiwa barazani kwake kapigwa risasi nae anaitwa kibaka?

View attachment 3700777

Advocate Makundi akiwa kasimama katika lango la kuingia kwake nae kapigwa risasi naye anaitwa kibaka leo?

View attachment 3700778

Hao ni kati ya wengi tu kamwe hatutawahi kusamehe wala kusahau

Mlishindwa kutumia njia sahihi kuwakamata vibaka muwapeleke mahakamani?

Tangu lini adhabu ya vibaka ni kuuwawa pia ?

Kisasi ni dawa yenu kikiwakosa ninyi basi wajukuu wenu au watoto wenu watakipata .

Machawa endeleeni kutumika maana hamna tofuati na toilet paper October 29 haijaisha hadi iishe.

Ni aheri uwendawazimu wa aina yoyote kuliko uwendawazimu wa uchawa. Kwanza mtu kuwa chawa wa wauaji, ni lazima uwe huna akili timamu, na pili lazima umkane Mungu wa kweli. Na kumkana Mungu wa haki, ni kuishi katika laana. Ndiyo maana machawa yote hapa JF, kuanzia Tlaatlaah mpaka mtoto wa shule, ukiangalia tu maondiko yao, unaona wazi kabisa kuwa hao watu wamekosa hata ile akii ndogo kabisa ya tafakri.
 
Machawa watafikiwa tu, wamuulize Cyprian Musiba Majura .
 
Shehe majini alilipua kituo cha nyumbani kwako we chawa mzee?
vita haina macho ndugu mdau,
huenda hata wewe ungekutwa uko sheli, ukiwa na yule bodaboda wako uliomzoea, huenda mngelipuliwa na yale magaidi aise 🐒
 
Hii desturi ya kuilaumu serikali kwa Kila jambo linalotokea katika jamii si sahihi, mzazi/MLEZI ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunatoa malezi yakutosha kwa watoto wetu.

Mtoto akue akijua kuwa WIZI haufai matokeo yake ni kifungo/kifo, ajue kuwa matusi hayafai, ajue kuwa tamaa na wivu Mali za watu haifai...haya mafunzo yatolewe kwa watoto wangali Bado wadogo na yaambatane na motivation & reinforcement.

Sahzi kumekuwa na desturi unakuta kitoto kidogo kinaongea ngono mwanzo mwisho halafu anatokea mla donation mmoja wa ufipa anailaumu serikali....this is childish.
Mkuu; mbona naona kama kichwa cha habari na contents haviendani?
Umeandika kwenye heading - umechoma,umeiba umeharibu mali etc.lakini kwenye contents unazungumzia malezi.
Nilitegemea kwa kuzingatia kichwa cha Habari uandike kwamba kwa mujibu wa Sheria Na........ au Utaratibu.........au kwa kuzingatia kifungu cha Katiba ya JMT....... ilikuwa ni HALALI kwa vyombo vya Dola kuwaua wahusika kwa kuwapiga risasi. Halafu ikikupendeza zaidi utoe uthibitisho wa Ushiriki wa waliouawa.
Ni hayo tu.
 
Wale vibaka walistahili kile kichapo nawapa pole wale wengine ambao walipigwa nyumbani kwao akiwemo master Tindwa walipigwa kwa sababu ya hawa wezi wanaiba barabani wanakimbilia mtaani walifuatwa huko huko ikasababisha na wengine wapoteze maisha
 
Mkuu; mbona naona kama kichwa cha habari na contents haviendani?
Umeandika kwenye heading - umechoma,umeiba umeharibu mali etc.lakini kwenye contents unazungumzia malezi.
Nilitegemea kwa kuzingatia kichwa cha Habari uandike kwamba kwa mujibu wa Sheria Na........ au Utaratibu.........au kwa kuzingatia kifungu cha Katiba ya JMT....... ilikuwa ni HALALI kwa vyombo vya Dola kuwaua wahusika kwa kuwapiga risasi. Halafu ikikupendeza zaidi utoe uthibitisho wa Ushiriki wa waliouawa.
Ni hayo tu.
Swala ni kwamba vibaka wameuana
 
Shekhe sharifu majini, alikuwa mwana CCM kindakindaki, na alipomaliza kutick alienda kwake, ana aka post kuwa ametoka kutick, aliuliwa kwake, huyo nae alienda kuchoma nini?

Ukweli ni kuwa kuna watu waliharibu Mali za watu ambao sio Jambo zuri, lakini masikitiko watu waliuwawa wengi wao hawakushiriki hayo mambo
Hiyo ni kawaida zinapotokea ghasia au vita madhara yatawapata waliokuwemo na wasio kuwemo ila mwisho wa siku anayepasa kulaumiwa yule aliyeanzisha ghasia na si serikali iliyokuwa inazuia hizo vurugu

Na kama serikali isingepambana kuzima hizo vurugu yawezekana hata wewe sahizi ingekuwa umeshakufa

Vipi kama serikali ingeacha vurugu ziendelee Yani tokea October 29 2025 Hadi Leo vurugu zingekuwa bado zinaendelea ni watu wangapi wangekuwa wameathirika Kwa kupoteza maisha na Mali zao
 
Swala ni kwamba vibaka wameuana
Kivipi mkuu? Vibaka walikuwa na AK 47 na SMG? Tena wakitumia Toyota Land cruiser Pick-up. Vibaka hao hao waliweza kukusanya maiti na kuzipeleka
Mortuary........... na Wakati hayo yooote yakifanyika; vyombo vya dola vyenye jukumu la Ulinzi na Usalama vimetulia vinatazama tuu hiyo movie? Hebu kuwa serious kidogo aisee.
 
Kweli tumekubali i vibaka 😂 waliouawa wakiwa nje ya nyumba zao ni vibaka ? Kuna mama alipigwa risasi ya tumbo katika harakati za kukimbia ni kibaka ?

Sawa tumekubali ni vibaka katiba inataka hivyo kwamba kukabiliana vibaka ni kuwapiga risasi kisha kuwarundika hadi mochwari zikajaa. Hakuna njia mbadala ya kukabiliana na vibaka ?

Haya tumekubali ni vibaka mbona mlienda kuwazika wapi? tupeni basi hiyo miili mbona mlienda kuizika na kuificha kwa siri ? 😂

Haya tumekubali ni vibaka , maridhiano ni ya nini ,
Hili jambo mtajiongelesha sana ila Karma italipa tu !!
 
Hiyo ni kawaida zinapotokea ghasia au vita madhara yatawapata waliokuwemo na wasio kuwemo ila mwisho wa siku anayepasa kulaumiwa yule aliyeanzisha ghasia na si serikali iliyokuwa inazuia hizo vurugu

Na kama serikali isingepambana kuzima hizo vurugu yawezekana hata wewe sahizi ingekuwa umeshakufa

Vipi kama serikali ingeacha vurugu ziendelee Yani tokea October 29 2025 Hadi Leo vurugu zingekuwa bado zinaendelea ni watu wangapi wangekuwa wameathirika Kwa kupoteza maisha na Mali zao
Heshima yako Mkuu.
Umetoa ufafanuzi mzuri sana
 
CCM ina vijana vilaza sana.
Mauaji yaliendelea Kwa siku 3 mfululizo.usiku na mchana na asubuhi.
Mimi Sina tatizo na waliokufa tarehe 29;naweza kusema walikuwa kwenye maaandamano.vipi wale waliuliwa tarehe 30 na kuendelea baada y maaandamano kuzimwa?
 
Hiyo ni kawaida zinapotokea ghasia au vita madhara yatawapata waliokuwemo na wasio kuwemo ila mwisho wa siku anayepasa kulaumiwa yule aliyeanzisha ghasia na si serikali iliyokuwa inazuia hizo vurugu
Mkuu; kuwa mkweli wa nafsi yako: Ina maana siku hiyo hakukuwepo Virungu?na maji washawasha? Hapa kuwepo na Mabomu ya machozi? Hapakuwepo na Blank bullets? Hapa kuwepo na Plastick bullets? Kwani hao wanaodaiwa kufanya ghasia walibeba silaha gani? Nilimsikia mtu mmoja akidai eti walikuwa na silaha lakini hakuna silaha hata moja iliyokamatwa kama uthibitisho.
Na kama serikali isingepambana kuzima hizo vurugu yawezekana hata wewe sahizi ingekuwa umeshakufa
Waliohusika kufanya hizo vurugu walikuwa wameshaua watu innocent wangapi ndo Serikali ikaingilia kati?
Vipi kama serikali ingeacha vurugu ziendelee Yani tokea October 29 2025 Hadi Leo vurugu zingekuwa bado zinaendelea ni watu wangapi wangekuwa wameathirika Kwa kupoteza maisha na Mali zao
Serikali esp. vyombo vya Dola wamepata mafunzo chuoni ya jinsi ya kudeal na vurugu za aina mbalimbali. Hakuna mahali ilipoelekezwa kuua mtu anayefanya vurugu.
Yapo mazinira yanayoweza kupelekea askari kumwuua mtu anayefanya vurugu e.g. ilivyokuwa kwa yule jamaa wa Salenda bridge. Lakini hao vijana maskini ya Rabi hata manati hawakuwa nayo.
 
Heshima yako Mkuu.
Umetoa ufafanuzi mzuri sana
Sidhani kama huo ufafanuzi unaosema ni mzuri sana kama una mashiko hata kidogo. Yapo maswali/Hoja ambazo haziko wazi. e.g. Serikali ni kweli ilishindwa kutumia mbinu mbadala?
Serikali inatenda kwa kuzingatia Katiba; Sheria, Kanuni na Taratibu. Je hapo kwenye kutumia risasi za moto dhidi ya hao wahanga ambao hawakuwa na silaha walizingatia lipi kati ya hayo au walikuwa wanaenjoy kuua tu watu rondomly??
 
Kweli tumekubali i vibaka 😂 waliouawa wakiwa nje ya nyumba zao ni vibaka ? Kuna mama alipigwa risasi ya tumbo katika harakati za kukimbia ni kibaka ?

Sawa tumekubali ni vibaka katiba inataka hivyo kwamba kukabiliana vibaka ni kuwapiga risasi kisha kuwarundika hadi mochwari zikajaa. Hakuna njia mbadala ya kukabiliana na vibaka ?

Haya tumekubali ni vibaka mbona mlienda kuwazika wapi? tupeni basi hiyo miili mbona mlienda kuizika na kuificha kwa siri ? 😂

Haya tumekubali ni vibaka , maridhiano ni ya nini ,
Hili jambo mtajiongelesha sana ila Karma italipa tu !!
Itoshe tu kusema Roho zao hao wauaji hazitokaa zitulie ndani mwao.
 
Back
Top Bottom