Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Sasa kama ni beyond our tiny capabilities kuelewa, hii Quran imeandikwa ili nani aielewe? Au ameandikiwa nani?

Safi kabisa mkuu! Na kama Kurani ni uncomprehensible document kwa binadamu yeye ameelewaje kwamba ni Uncomprehensible? Hiyo aya iko wapi? Na kama haieleweki kwa wanadamu,ni kwa nini Mungu alikuwa anampatia Muhammad kwa nguvu vile, tena kwa kumpiga kiasi kile, kule Pangoni?

Je,huyu jamaa anataka kutuambia kuwa Kurani hadi leo haieleweki kama vile ambavyo Muhammad alishindwa kuielewa wakati ule (hadi Mungu kuamua kumpiga Muhammad kwa njia ya Malaika Gabrieli)?
 
hahaaaa halafu utasemaje kwamba sayansi ni uwongo wakati ",unatumia material mbali mbali yanayokurahisishia" kuishi kwako "tena matukio hayo yakiwa nizao la sayansi"",hayo maandishi "Yao" yenyewe" walikuwa hawana uwezo " wakuyahifadhi" kwenye karatasi" mpaka pale Ambapo "wanasaynsi "walipogundua" tech ,, yakuhifadhi maandishi" kwenye vitabu"" so kwanini" wasingemwambia "mungu wao awapatie ujuzi wakufanya "hayo yote" kama "Kweli " hayo madai yao huwa ni yamsingi
 
Daah...huu uzi uko jukwaa sahihi kabisa maana una hoja nzito sana. Kama na kwenye kitabu cha wakristu cha Biblia kuna sentensi inayosema Joshua alisimamisha jua....je huu si ushahidi kuwa Mungu anasema Jua ndilo huzunguka dunia na siyo vinginenvyo?
hahaaa"" nilishamjibu mtoa Mada mmoja hivi ""
 
Mkuu akijibu hata hoja mojawapo kati ya hizi unitag
 
Dini nyingi zina hadithi nyingi za kale zisizokuwa na ukweli, primitive mythologies

Swali la Msingi ni kwamba inakuwaje Mungu awaandikie wanadamu hadithi na ngano na kuwaambia kuwa ndiyo matukio halisi? Ina maana Mungu hajui tofauti kati ya Hadithi na tukio halisi?
 
Karibu sana mkuu!Gonga Balimi zako ukiwa na tahadhari sana kwa sababu ikitokea matope linakochwea hilo Jua yaka-overflow, Balimi itageuka kuwa msiba.
Inaonekana mzee una majibu yako tayar na pia unajionyesha kabisa imani yako iko upande gani tayar umeanza kudhihaki kile ulichokiuliza.
Jiulize hivi biblia na quraan inatuambia mtu wa kwanza aliumbwa kwa udongo ambaye ni adamu,wanasayansi wametuambia mtu wa kwanza ametokana na sokwe na fuvu lake limegunduliwa Tanzania sasa hapo mzee wewe una amini lipi labda?
 
Kweli kabisa, yapo mengi yana changanya sana Mud anasema shetani ni mbaya ila jini kiumbe mzuri hana shida anaweza kushirikiana na binadam bila shida.
 
Hakuna la kujadili hapo! Kwasababu unavyoviita 'sayansi' na 'dini' ni vitu viwili tofauti.
Dini ni imani. Ni hiyari yako kuamini au kutoamini uambiwacho. Na si lazima mtu mwingine aamini uaminicho wewe.
Sayansi ni elimu, maarifa au taaluma. Kupitia elimu umeambiwa na umeelewa kwamba dunia ni sayari inayolizunguka jua, si kinyume chake.
Umeambiwa ukifa utakwenda 'mbinguni' labda umeamini; hata kama hujafa! Kuna la kujadili hapo? Ukishakufa ndio utajua ukweli au uongo wa hilo.
Kwanza kuna wengine wenye imani zao watakuona kama ni mchokozi. Unaweza kujikuta anamlaumu Mungu wako kwamba kwanini 'alikuumba' na kichwa kimoja tu; sio viwili au vinne? Ukitumia akili ya imani utapata jibu kuwa umeumbwa kwa mfano wa Mungu, (usiniulize kama Mungu ni mwanaume au mwanamke!)
Napendekeza huu mjadala wako uupeleke msikitini au kanisani kwa jinsi imani yako ilivyo.
 
Swali la Msingi ni kwamba inakuwaje Mungu awaandikie wanadamu hadithi na ngano na kuwaambia kuwa ndiyo matukio halisi? Ina maana Mungu hajui tofauti kati ya Hadithi na tukio halisi?
Mungu huwa haandiki, hakuwahi kuandika na hataandika kamwe. Wanadamu ndio wanaotunga na kuandika kisha kusema ni Mungu ili utunzi wao ukubalike
 
SANCTUS ANACLETUS usitake kupotosha, hapo Mwenyezi Mungu anaeleza kile DHIL QARNAIN (ALEXANDER THE GREAT ) "alichokiona" kwa udhaifu wake, someni muelewe bana, mbona ipo very clear ? .... 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Kwenye Aya nyingine ya SURAH AN'AM ( 6;78 ) anaeleza alichokiona ( Nabii ) Ibrahim
Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina.
So ina maana hapo Qur'ani inasema kuwa Jua ndio Mola mlezi mkubwa wa Ibrahim ?? Na zipo nyingi Aya kama hizo ,
Qur'an huwezi kusoma ukaielewa unavyotaka wewe , uinyofoe aya katikati ( out of context ) mbichi mbichi ikupe tafsiri uonavyo wewe mkuu bila kujua sababu ya kushuka kwake,n.k.
 

So, if Muhammad in moving and finally viewing the boundary,was that enough for him to conclude that what he was seeing was the dark muddy spring onto which the Sun had set in?So who was seeing on the way, the Sun moving towards boundaries,God or Muhammad?

Hivi kwa maelezo yako hayo unaelewa maana ya Kurani? Usitupotoshe kwa kutuletea maana tafsiri nyingine ya Kurani.Kurani maana yake ni maneno aliyoyaandika Mungu kwa mkono wake mwenyewe na kisha kumpatia Malaika Gabrieli (naye bila editing wala addition) akampatia Muhammad.Kwa hiyo,hiyo suala lolote linalosemwa na Muhammad maana yake ni Mungu anasema na sio vinginevyo!
 
Mungu huwa haandiki, hakuwahi kuandika na hataandika kamwe. Wanadamu ndio wanaotunga na kuandika kisha kusema ni Mungu ili utunzi wao ukubalike

Maneno hayo kwamba Mungu ndiye aliandika na kisha kumpatia Muhammad, yako katika Kurani na wala sio yangu, mkuu.Mimi nasaidia tu kueleza kile ambacho Mungu ameshakisema kupitia Kurani.
 
Kweli kabisa, yapo mengi yana changanya sana Mud anasema shetani ni mbaya ila jini kiumbe mzuri hana shida anaweza kushirikiana na binadam bila shida.
nafuu ya shetani nimbaya watu wanaaminishwa Kuwa
anga la blue ni mbingu nawao wanaamimi
 
Mie naona unatuletea uongo wa sayansi juu ya juwa.
 
Binafsi elimu dunia nimeisoma na kuilinganisha na elimu ya Mungu. Elimu ya Mungu iko pure na hapana chembe ya uongo. Suala la jua kutozunguka hiyo ni uongo wa kisayansi, kwani kiuhalisia hata kwa kulitazama jua lina Move.
Kwamba dunia ni elliptical sphere, pamoja kung'ang'anizwa nikariri hivyo mpaka leo hii nimekataa na naona kwa macho yangu dunia ni flat, Jua, Mwezi na Nyota zote zinazunguka juu ya uso wa dunia, Jua na mwezi zikiwa na ukubwa sawa na kiwango cha mwanga tofauti lakini Nyota zikiwa ni ndogo kuliko jua na mwezi.
By the way, Jua sio Nyota na wala Nyota sio jua kama sayansi inavyolazimisha.
Zaidi ya hapo vitu vinavyoitwa sayari is just "sci-fi" tu but in reality hakuna kitu kinaitwa sayari angani but kuna Mwezi, Jua, na Nyota.
Drama za NASA hasa ni za kupinga ukweli halisi (ambao hata wao wa Naujua) na kule launch uongo mkuu kwa malengo maalumu kabisa.
Bila Shaka Dunia sio sayari na haijawahi kuwa, tena ni kweli Antarctica sio bara la saba kwa ukubwa bali ni Sio bara kabisa ndio maana hata kwenye bendera ya UN naya USGS halijaoneshwa kwa kwa kuwa sio bara.
Kwa kumalizia ni kwamba sio wanasayansi wote wanaothibisha kuwa jua ni Immovable objects lipo kundi kubwa tu la wanasayansi wa kale na wa kisasa wanaothibisha pasipo chembe ya shaka kuwa dunia ni immovable, na jua, mwezi na Nyota ni movable objects.
So neno la Mungu always linabaki sahihi na la binadamu (hao wanasayansi) uongo wa makusudi wenye nia ovu!!
 


Mkuu kaa vizuri sana katika uzi huu kwa maana ukija pupa utakosa mlango wa kutokea! Hapo Mungu anaongeleaje habari za Alexander the Great? Alexander, aongelewe hapo kwa faida ya nani hasa? Mungu alikuwa anamueleza Muhammad habari za Alexander kwa ili Muhammad apate picha gani hasa?

Hivi unafahamu kuwa Alexander the Great aliishi miaka mingi sana kabla ya hata Yesu Kristu kuzaliwa au hata Muhammad?

Mtawala aliyeitwa Aleksanda Mkuu (Alexander the Great) alikuwa ni mtawala(Mfalme) wa Makedonia (336-323 KK).Makedonia ni eneo la kijiografia na kihistoria katika Peninsula ya Balkani, kusini-mashariki mwa bara la Ulaya.Je,ni lini Muhammad aliwahi kufika Makedonia kabla hajazaliwa hadi akaweza kuona jinsi Alexander alivyoliona Jua likizama katika matope?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…