Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
nafuu ya shetani nimbaya watu wanaaminishwa Kuwa
anga la blue ni mbingu nawao wanaamimi
We naamisha nini? Cause neno anga nalo limenenwa kwenye maandiko pia, na sio anga tu kirahirahisi kama kiswahili kinavyotambua, bali FIRMAMENT, yaani a VAULT OF HEAVEN.
Kwa kumaanisha vault, ina maana hapana awezae kukatiza hapo.
 
Mkuu kaa vizuri sana katika uzi huu kwa maana ukija pupa utakosa mlango wa kutokea! Hapo Mungu anaongeleaje habari za Alexander the Great? Alexander, aongelewe hapo kwa faida ya nani hasa? Mungu alikuwa anamueleza Muhammad habari za Alexander kwa ili Muhammad apate picha gani hasa?

Hivi unafahamu kuwa Alexander the Great aliishi miaka mingi sana kabla ya hata Yesu Kristu kuzaliwa au hata Muhammad?

Mtawala aliyeitwa Aleksanda Mkuu (Alexander the Great) alikuwa ni mtawala(Mfalme) wa Makedonia (336-323 KK).Makedonia ni eneo la kijiografia na kihistoria katika Peninsula ya Balkani, kusini-mashariki mwa bara la Ulaya.Je,ni lini Muhammad aliwahi kufika Makedonia kabla hajazaliwa hadi akaweza kuona jinsi Alexander alivyoliona Jua likizama katika matope?
Kwani alioliona jua linazama kwenye matope ni Muhammad au Dhur Qanain?
 
kwani wewe unaposikiaga waswahili wakiizungumzia mbingu "" huwa unawasikia wakimaamisha nini" Mimi namaanisha" hiyo rangi ya blue " onayoonekana angani" so Kama wewe waiongelea hiyo " mbona watu wanapita " hapo
 
Hata kama wamegundua kwamba Mungu hakuwahi kusema hivyo kwamba Jua linachwea katika matope meusi,ni suala la kukiri tu hadharani na kufuta hiyo aya na kisha maisha yanaendelea.Kwani kuna shida gani kufuta hiyo aya katika Kurani na kubakisha yale yaliyo ya kweli?
Kwa hiyo kuna uwezekano wa aya zote za Quran zikawa sahihi kwa hiyo ifutwe hii tu ili kitabu kizima kikamilike?
 
Kwa hiyo kuna uwezekano wa aya zote za Quran zikawa sahihi kwa hiyo ifutwe hii tu ili kitabu kizima kikamilike?

Wewe unaonaje? Ikiwa Kurani ni neno la Mungu (na ndiye aliyeandika kwa mkono wake) na ikaonekana aya moja ni batili,je,hizo zingine zinasaliaje kuwa sahihi wakati mwandishi wa aya zote ni Mungu yule yule?
 
Wanajukwa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.

Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?

2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?

3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?

· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?

· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.
Picha ya kwanza na ya tano nikiwa namsimulia mtu jinsI nilivyoliona jua linazama nikamiambia nimeliona jua linazama kwenye maji nitakua namaanisha linazama kwenye maji kweli au ndivyo nilivyoona kwa muono wangu? VipI kuhusu picha ya pili Jua si naliona linazama ardhini? Na picha ya tatu utamuelezeaje mtu kwamba unaliona jua linazama vipi? Nikisema nyuma ya mlima nitakosea? Picha ya nne nikisema jua limezama kwenye mawingu meusi je?

Nadhani hata huyo anaesimuliwa katika Qur an anasema aliliona jua linazama katika matope meusi kwa muono kama huo hapo juu.
images%20(4).jpeg
images%20(3).jpeg
images%20(1).jpeg
images%20(5).jpeg
images.jpeg
 
Kwani alioliona jua linazama kwenye matope ni Muhammad au Dhur Qanain?

Mkuu unaniuliza swali ambalo liko wazi namna hiyo? Kiswahili kilichotumika kwenye hiyo aya mbona ni kirahisi sana? Basi,ngoja tuirejee tena aya husika hapa halafu kisha tubainishe hapo ni wahusika gani wanaongea na mambo gani wanaongea:

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Kwa hiyo ,mambo yafuatayo yako wazi:

1. Mungu alikuwa anamsaidia Muhammad kutoa historia ya Dhul-Qarnaini na katika kufanya hivyo anampa Muhammad kisa hicho cha Dhul-Qarnaini dhidi ya Jua.

2. Kwamba Dhul-Qarnaini aliliona Jua linatua katika Matope.

Sasa maswali la kujiuliza:

1. Mungu, anapomuadithia Muhammad kwamba Dhul- Qarnaini wakati akitembea alifika mahali akaliona Jua linazama katika matope meusi,Mungu alimaanisha nini hasa?

2. Je,kwa aya hiyo, Sio kwamba Mungu alikuwa anamuelezea Muhammad jinsi Dhul- Qarnaini alivyoliona Jua likizama katika matope?

3. Je,kama ndivyo Mungu alivyomaanisha hapo katika namba 2, Muhammad hakuamini hadithi hiyo?

4.Na kama Muhammad aliamini,je,si ni kweli kwamba kumbe Jua linazama katika matope meusi?
 
Mambo ya imani huwezi kuyaprove kisayansi kirahisi hivyo. Hata suala la Yesu kutembea juu ya maji kisayansi halina mashiko, suala la kubadilisha maji kuwa mvinyo na kujaza makombo ya samaki wawili wasiojaa hata robo ya kikapu kwenye vikapu kumi halina mashiko ya kisayansi.

Hata Mwenyezi MUNGU huwezi kumthibitisha kisayansi. Mussa kapiga maji kwa fimbo yakagawanyika kisayansi huwezi kuprove, Joshua kusimamisha jua ambalo halizunguki huoni kama ni ajabu! Pilipili ya shamba yakuwashia nini mkuu??Mkuu waache waaminio wapate kuamini.
 
Nimekuuliza hivyo sababu wewe umemuuliza mtu huko juu kwamba lini Muhammad alienda Mekodonia akaliona hilo jua linazama kwenye tope sasa ndio nakauliza hiyo habari anayesimuliwa kuliona ni Muhammad au Dhel qanain?
 
Picha ya kwanza na ya tano nikiwa namsimulia mtu jinsI nilivyoliona jua linazama nikamiambia nimeliona jua linazama kwenye maji nitakua namaanisha linazama kwenye maji kweli au ndivyo nilivyoona kwa muono wangu? VipI kuhusu picha ya pili Jua si naliona linazama ardhini? Na picha ya tatu utamuelezeaje mtu kwamba unaliona jua linazama vipi? Nikisema nyuma ya mlima nitakosea? Picha ya nne nikisema jua limezama kwenye mawingu meusi je?

Nadhani hata huyo anaesimuliwa katika Qur an anasema aliliona jua linazama katika matope meusi kwa muono kama huo hapo juu.View attachment 814741View attachment 814742View attachment 814743View attachment 814744View attachment 814745
wajinga hawataiona hii comment
 
Kwani katika aya hiyo ambayo nimeinukuu ni nani anayeongea hapo? Ni Muhammad au Mungu pekee? Je,Ni Mungu na Muhammad au Dhul-Qarnaini? Ni nani anayemueleza Muhammad kuwa ikiwa kuna watu wanakuuuliza habari za Dhul-Qarnaini,sisi tutakupatia historia yake? Naomba utueleze ni nani hasa hapo anayempa Muhammad stori za Dhul-Qarnaini.Ikiwa ni Mungu,si ina maana ndiye aliyemuona Dhul-Qarnaini akiliona Jua likizama katika matope au vipi? Na kama Mungu aliliona Jua likizama katika matope kama alivyoliona Dhul-Qarnaini ni wapi kuna utata au uongo? Na kama ndivyo,nimekosea wapi kusema Muhammad ndiye aliyeliona Jua likizama katika matope?Hivi huelewi kuwa Muhammad anasema kwa kinywa cha Mungu yale yale ambayo Mungu aliyaona?
 
Kwaiyo kwa mujibu wa hizo picha unakubali jua linaweza kuonekana linazama katika matope,maji au nyuma ya mlima?
 
Mkuu kaa vizuri sana katika uzi huu kwa maana ukija pupa utakosa mlango wa kutokea! Hapo Mungu anaongeleaje habari za Alexander the Great? Alexander, aongelewe hapo kwa faida ya nani hasa? Mungu alikuwa anamueleza Muhammad habari za Alexander kwa ili Muhammad apate picha gani hasa?

Hivi unafahamu kuwa Alexander the Great aliishi miaka mingi sana kabla ya hata Yesu Kristu kuzaliwa au hata Muhammad?

Mtawala aliyeitwa Aleksanda Mkuu (Alexander the Great) alikuwa ni mtawala(Mfalme) wa Makedonia (336-323 KK).Makedonia ni eneo la kijiografia na kihistoria katika Peninsula ya Balkani, kusini-mashariki mwa bara la Ulaya.Je,ni lini Muhammad aliwahi kufika Makedonia kabla hajazaliwa hadi akaweza kuona jinsi Alexander alivyoliona Jua likizama katika matope?
Hahaha naona wewe ndio ushapata mlango wa kutokea kwa kutafuta kuhamisha mjadala , si umeona sasa nilikusihi kwenye paragraph ya mwisho na hukunielewa.. hahaha eti ili Muhammad apate picha gani, kumbe hata hujui hiyo habari ya Dhil Qarnain ilianzaje mpaka ikafikia hapo, eti 300 BC ndo umeona ajabu, na ya manabii wengine yaliyozungumzwa kwenye Qur'an kina Adam, Noah, Idriss, Daud, Solomon, Ibrahim, Musa mbona hujajiuliza ilikuwa B.C ngapi ? Yaani hapo ndo umedhihirisha uko mtupu kwenye masuala haya... Mkuu bora utafute mada nyingine ya kujadili, hii itakuwa too big for you my dear bro..
 
Mambo ya imani huwezi kuyaprove kisayansi kirahisi hivyo. Hata suala la Yesu kutembea juu ya maji kisayansi halina mashiko, suala la kubadilisha maji kuwa mvinyo na kujaza makombo ya samaki wawili wasiojaa hata robo ya kikapu kwenye vikapu kumi halina mashiko ya kisayansi.

Hata Mwenyezi MUNGU huwezi kumthibitisha kisayansi. Mussa kapiga maji kwa fimbo yakagawanyika kisayansi huwezi kuprove, Joshua kusimamisha jua ambalo halizunguki huoni kama ni ajabu! Pilipili ya shamba yakuwashia nini mkuu??Mkuu waache waaminio wapate kuamini.

Kwa hiyo mambo ya Mungu tunaya-prove kwa njia gani? Ndio maana uzi unauliza kwamba, ni nani muongo kati ya Mungu na wanasayansi? Ina maana kwa hitimisho lako, wanasayansi ni waongo na Muhammad ndiye yuko sahihi kwamba Jua huchwa katika matope?Hilo la pilipili nisizozila zinaniwasha vipi,nadhani unapaswa kuelewa kuwa mimi niko naishi hapa duniani na kwa hiyo suala linaloongelea dunia ninayoishi ni muhimu kulifahamu nje ya mduara wa Mashaka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom