Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Hahaha naona wewe ndio ushapata mlango wa kutokea kwa kutafuta kuhamisha mjadala , si umeona sasa nilikusihi kwenye paragraph ya mwisho na hukunielewa.. hahaha eti ili Muhammad apate picha gani, kumbe hata hujui hiyo habari ya Dhil Qarnain ilianzaje mpaka ikafikia hapo, eti 300 BC ndo umeona ajabu, na ya manabii wengine yaliyozungumzwa kwenye Qur'an kina Adam, Noah, Idriss, Daud, Solomon, Ibrahim, Musa mbona hujajiuliza ilikuwa B.C ngapi ? Yaani hapo ndo umedhihirisha uko mtupu kwenye masuala haya... Mkuu bora utafute mada nyingine ya kujadili, hii itakuwa too big for you my dear bro..

Naona wewe unafikiria mimi nimesoma Kurani kwa kudokoa.Hayo mambo ya manabii wa zamani subiria muda wake ukifika utabaki mdomo wazi.Kumbe najadiliana na mtu aliyekariri Kurani.Hapa nimeanza kutikisa Kurani kwa kipengele kimoja tu katika Sayansi.Nina mambo mengi sana.Kwa hiyo, stay tuned.Mimi huwa siandiki mambo ya kubumba hata siku moja.Ukiona naandika maana yake nimefanya utafiti.

Mpaka leo huelewi Kurani imejaa nini na Muhammad mambo hayo alikuwa anayatoa wapi? Tulia utapewa moja baada ya jingine tena kwa ushahidi mzito.
 
Dhu'l Qarnnain inasemekana ni Alexander the Barbarian ila mohamed bin abdullah kama kawaida yake aliisikia hii story akaicopy ovyo!!!

hekaya zake ni nyingi tu

the earth is flat like a carpet-quran 2:22
there are 7 earths-quran 65:12
the sun and moon chase one another-quran 36:38-40
the sky would fall on earth if allah didn't hold it up-quran 22:65
quran 31:31 ships sailing through the sea is a miracle by allah
bukhari kitabul ta'abir
"seeing a black woman in a dream is the sign of an oncoming epidermic"
 
kwani wewe unaposikiaga waswahili wakiizungumzia mbingu "" huwa unawasikia wakimaamisha nini" Mimi namaanisha" hiyo rangi ya blue " onayoonekana angani" so Kama wewe waiongelea hiyo " mbona watu wanapita " hapo
Kwa kiswahili chetu neno anga lina maana ya uwazi uliopo kuanzia usawa wa ardhi kwenda juu uliojaa hewa za aina mbalimbali pia humo Nyota, mwezi na jua vipo humo. Lakini anga kwa maana ya FIRMAMENT ina maana ni kitu kinachotenganisha maji yaliyo juu ya mbingu na yaliyo chini. Rejea GENESIS 1:6-9 "Mungu akasema," NA liwe ANGA katikati ya MAJI na MAJI. Mungu akalifanya Anga, akayatenga yale MAJI YALIYO JUU YA ANGA NA YALE MAJI YALIYO CHINI YA ANGA; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile ANGA Mbingu. 9.Mungu akasema Maji yaliyo chini ya Mbingu yakusanyike mahali pamoja. ..

MY WORDS.
Anga linalosema na neno la Mungu ni zaidi ya uwazi uliojaa hewa na gas mbalimbali bali anga ni pamoja na paa linaloifunika dunia ambalo pia paa hilo limebeba maji yaliokuwa juu ya mbingu.
 
Dhu'l Qarnnain inasemekana ni Alexander the Barbarian ila mohamed bin abdullah kama kawaida yake aliisikia hii story akaicopy ovyo!!!

hekaya zake ni nyingi tu

the earth is flat like a carpet-quran 2:22
there are 7 earths-quran 65:12
the sun and moon chase one another-quran 36:38-40
the sky would fall on earth if allah didn't hold it up-quran 22:65
quran 31:31 ships sailing through the sea is a miracle by allah
bukhari kitabul ta'abir
"seeing a black woman in a dream is the sign of an oncoming epidermic"

Hongera mkuu!Leo tuna moja tu hili la Jua kutua katika matope.Bado kuna mambo ya historia yalivyoandikwa visivyo.Mambo ya kisayansi yalivyoelezwa visivyo.Bado mambo ya Lugha ya Kiarabu kuandikwa visivyo na lugha ya Kiarabu kuchanganywa na lugha zingine wakati Kurani inadaiwa kushushwa kwa Kurani pekee! Stay tuned!
 
Kwa kiswahili chetu neno anga lina maana ya uwazi uliopo kuanzia usawa wa ardhi kwenda juu uliojaa hewa za aina mbalimbali pia humo Nyota, mwezi na jua vipo humo. Lakini anga kwa maana ya FIRMAMENT ina maana ni kitu kinachotenganisha maji yaliyo juu ya mbingu na yaliyo chini. Rejea GENESIS 1:6-9 "Mungu akasema," NA liwe ANGA katikati ya MAJI na MAJI. Mungu akalifanya Anga, akayatenga yale MAJI YALIYO JUU YA ANGA NA YALE MAJI YALIYO CHINI YA ANGA; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile ANGA Mbingu. 9.Mungu akasema Maji yaliyo chini ya Mbingu yakusanyike mahali pamoja. ..

MY WORDS.
Anga linalosema na neno la Mungu ni zaidi ya uwazi uliojaa hewa na gas mbalimbali bali anga ni pamoja na paa linaloifunika dunia ambalo pia paa hilo limebeba maji yaliokuwa juu ya mbingu.
ndio maji ya matope jua linapozama😀🙁🙁🙁
 
Daah...huu uzi uko jukwaa sahihi kabisa maana una hoja nzito sana. Kama na kwenye kitabu cha wakristu cha Biblia kuna sentensi inayosema Joshua alisimamisha jua....je huu si ushahidi kuwa Mungu anasema Jua ndilo huzunguka dunia na siyo vinginenvyo?
Kwa hiyo ilitakiwa iwe alisimamisha dunia?
 
Mambo ya imani huwezi kuyaprove kisayansi kirahisi hivyo. Hata suala la Yesu kutembea juu ya maji kisayansi halina mashiko, suala la kubadilisha maji kuwa mvinyo na kujaza makombo ya samaki wawili wasiojaa hata robo ya kikapu kwenye vikapu kumi halina mashiko ya kisayansi.

Hata Mwenyezi MUNGU huwezi kumthibitisha kisayansi. Mussa kapiga maji kwa fimbo yakagawanyika kisayansi huwezi kuprove, Joshua kusimamisha jua ambalo halizunguki huoni kama ni ajabu! Pilipili ya shamba yakuwashia nini mkuu??Mkuu waache waaminio wapate kuamini.

Nimependa sana mstari wa mwisho mkuu.
 
Kwaiyo kwa mujibu wa hizo picha unakubali jua linaweza kuonekana linazama katika matope,maji au nyuma ya mlima?

Mimi siwezi kutoa majibu kwa kuangalia picha tu! Mbona unataka kunipeleka katika kufikiri kama Mende? Kwa hiyo, unataka mimi kunifikirisha kuwa nikiona tu Picha ya mtu nisiyemfahamu nihitimishe kuwa ni wewe? Yaani nione picha hizo kisha nihitimishe kuwa ni Jua hilo? Vipi kama hicho ninachokiona katika picha zako ni Tochi kubwa sana ndio inaonekana katika hizo picha zako?
 
Wanajukwa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.


Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?


2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?


3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?


· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?


· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.
Sikupingi kwa mifano ya kisayansa ila hizo zimeelezea kituo ambapo jua likitua atakuta watu aliotakiwa awakute aina maana jua linatua tu na ndio maana binadamu awez kanyaga maji akatembea kwa jua lakn kiiman watu wametembea kwenye maji ni mambo ya kiiman kwa muktadha maalum
 
Mambo ya imani huwezi kuyaprove kisayansi kirahisi hivyo. Hata suala la Yesu kutembea juu ya maji kisayansi halina mashiko, suala la kubadilisha maji kuwa mvinyo na kujaza makombo ya samaki wawili wasiojaa hata robo ya kikapu kwenye vikapu kumi halina mashiko ya kisayansi.

Hata Mwenyezi MUNGU huwezi kumthibitisha kisayansi. Mussa kapiga maji kwa fimbo yakagawanyika kisayansi huwezi kuprove, Joshua kusimamisha jua ambalo halizunguki huoni kama ni ajabu! Pilipili ya shamba yakuwashia nini mkuu??Mkuu waache waaminio wapate kuamini.


Suala la Yesu kutembea juu ya maji, suala la kubadilisha maji kuwa mvinyo na kujaza makombo ya samaki wawili wasiojaa hata robo ya kikapu kwenye vikapu kumi. Kisa cha Mussa kapiga maji kwa fimbo yakagawanyika, Joshua kusimamisha Jua ambalo halizunguki,YOTE HAYO ni miujiza.Sasa naomba kuuliza kuwa suala linaloongelewa na Muhammad mintarafu sula la Jua kuzama ni muujiza ndio ulikuwa unatokea?
 
Mimi siwezi kutoa majibu kwa kuangalia picha tu! Mbona unataka kunipeleka katika kufikiri kama Mende? Kwa hiyo, unataka mimi kunifikirisha kuwa nikiona tu Picha ya mtu nisiyemfahamu nihitimishe kuwa ni wewe? Yaani nione picha hizo kisha nihitimishe kuwa ni Jua hilo? Vipi kama hicho ninachokiona katika picha zako ni Tochi kubwa sana ndio inaonekana katika hizo picha zako?
Basi ukifika mda wa machweo tupigie picha wewe jua alafu tutakuambia kile tunachokiona linazama wapi.
 
Ila Yoshua aliekasimamisha Jua sio uongo? Na vipi sayansi inasemaje mtu akifa anaweza kufufuka kama Biblia inavyotuaminisha juu ya Yesu na Lazaro au napo tumepigwa?

ahaa! Huko huko kwenye imani Kuna sababu ya kuamini! ILI JAMBO LITHIBITIKE UKWELIBWAKE LAZIMA KUWE NA MASHAHIDI WAWILI HADI WATATU [emoji117]
IMG_20180721_162922_734.jpg
hivyo kisa cha Jushua na Yesu MASHAHIDI WALIO SHUHUDIA WAMETIMIA...sasa kama hicho kisa cha jua kuzama matopeni tuwekee hata Dalili za mashahidi!
 
Nimekuuliza hivyo sababu wewe umemuuliza mtu huko juu kwamba lini Muhammad alienda Mekodonia akaliona hilo jua linazama kwenye tope sasa ndio nakauliza hiyo habari anayesimuliwa kuliona ni Muhammad au Dhel qanain?

Kasome upya Kurani mkuu!Kafanye hivyo kwa faida yako.Mungu aongelee suala la Alexander the Great kwa Muhammad kwa faida gani hasa? Kuna relevance gani katika hicho kisa cha Alexander kuliona Jua likizama na jamii ambayo Muhammad alikusudiwa kupeleka huo Ujumbe? Kwa mfano,nikuulize leo kwa Uislamu wako, hicho kisa cha Alexander the Great kuliona Jua likizama katika matope kinakusaidiaje wewe katika maisha kiasi kwamba hata hiyo aya isalie humo kwenye Kurani?
 
ahaa! Huko huko kwenye imani Kuna sababu ya kuamini! ILI JAMBO LITHIBITIKE UKWELIBWAKE LAZIMA KUWE NA MASHAHIDI WAWILI HADI WATATU [emoji117] View attachment 814812 hivyo kisa cha Jushua na Yesu MASHAHIDI WALIO SHUHUDIA WAMETIMIA...sasa kama hicho kisa cha jua kuzama matopeni tuwekee hata Dalili za mashahidi!
Mimi sipo kiimani nipo kisayansi hayo mambo tunathibisha vipi kisayansi?
 
Basi ukifika mda wa machweo tupigie picha wewe jua alafu tutakuambia kile tunachokiona linazama wapi.

Mkuu hata nikikupigia picha haitasaidia kujibu hoja iliyo mbele yako.Usipende kunitoa kwenye reli.Kapige picha wewe mbashara na majibu utayapata.Hoja hapa ni kwamba ikiwa Mungu alikuwa kwa mjibu wa Aya hiyo ya Kurani anamuadithia Muhammad alichokiona Alexander the Great(Dhul-Qarnaini), ina maana Mungu naye si alikuwa analiona Jua likitua katika matope au vipi? Na kama ndivyo,kama Muhammad ameripoti habari hiyo sawa sawa na alivyoadithiwa na Mungu, si ina maana Muhammad naye aliamini stori hiyo au vipi?

Hiyo ndio hoja inayohitaji majibu.Mambo mengine ni kujaribu kututoa katika reli tu.
 
Sikupingi kwa mifano ya kisayansa ila hizo zimeelezea kituo ambapo jua likitua atakuta watu aliotakiwa awakute aina maana jua linatua tu na ndio maana binadamu awez kanyaga maji akatembea kwa jua lakn kiiman watu wametembea kwenye maji ni mambo ya kiiman kwa muktadha maalum

Ni sehemu gani sasa hapo lilipotua Jua halafu akawakuta hao watu? Ni sehemu gani mahali hapo duniani? Na watu gani hao au ni akina nani ambao walikuwa hapo Jua lilipotua kama njia ya kuwa-iedentify?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom