Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

lazima afukuzwe kazi mana anaowahudumia ni watu na wanadini na miongini mwao waislam wakiwepo,
amekiuka maadili ya kazi
hawezi toa huduma kwa usawa that why anachuki ya kidini
Mkuu angeshindwa kutoa huduma kwa mtu ambaye si dini yake huko kazini hapo kweli tungeona kosa ila alichofanya sioni kuhusiana na kazi yake.
 
Mtumishi wa Serikali aliyechana Quraan Tukufu asimamishwa kazi, Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo.

RPC Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Maleki, kwa kosa la kuchana na kuchoma moto kitabu cha Juzuu Amma ambacho ni sehemu ya Quran Tukufu.

“Maleki ni Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, alionekana akichana na kuchoma kitabu hicho Kitakatifu cha dini ya Kiislamu, kitendo ambacho kiliwakasirisha Waumini wa dini hiyo na wananchi waliokuwa maeneo hayo na kuamua kutoa taarifa kwa Polisi” RPC Mutafungwa.

Muheshimiwa Jafo amesema, Mtumishi huyo yuko chini ya ofisi ya Rais na jambo alilofanya halileti afya kwa jamii. Muheshimiwa Jafo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa kumsimamisha kazi mtumishi huyo pia afanye uchunguzi na kamati au mamlaka yake ya nidhamu iweze kuchukua hatua kadiri atakavyoona inafaa mara baada ya uchunguzi huo


Huyu kufukuzwa kazi ni sawa, ingawa Mimi ni Morisot
 
Uchawi unathibitishwa kivipi?
Wameuwa mtu asie kuwa na hatia kama kosa lake ni uchawi.

Uchawi unathibitishwa kwa athari na kuna ishara za kujua uchawi na kujua mtu amefanyiwa uchawi, huyo mpaka amepewa hiyo hukumu watu wamejiridhisha ndio maana kauliwa.

Sasa unapokubali kwamba ni mchawi kisha unakanusha kwa kusema ni mtu ambae hana hatia, inaonyesha ni kwa namna gani hujui unacho egemea. Huu ujinga huwa nauona jf pekee watu wajadili jambo wasilokuwa na elimj nalo.
 
Abuu Dharr,
Hapo ndo mutakua mmefanya busara kuliko kuchinja ..ila all in all jamaa kakosea. ...maana ujinga mdogo unaeza Leta machafuko nchi nzima....na ukweli wasingemkamata polisi..huyu angekua akhera madukani....
 
Hapatetewi makaratasi,kinachotetewa ni uvunjifu wa amani.Wafikiri kitendo,cha kukashifu imani ya mtu ni kidogo?Lakini waislam,wa eneo husika,wapewe pongezi,kwa kuwa wavumilivu.
Katika hii dunia tunaoishi kwa raha ni tusiofungamana, juzi wazee Wa "Daddy I Receive" walikua na kibarua cha kumtetea Mwamposa, leo wavaa pedo na makubazi wana kibarua cha kutetea makaratasi

Kujitakia presha za bure tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haiwezi kumwachia , yule kasema( kaandika) kutokana imani yake anaweza akatoa reference lakini yy kaichana Quran ,sijui Ana reference gani
Si inakera lakini kwa mtu anaeamini kwamba Yesu ni Mungu? Reference ya imani ya mtu mwingine inaweza kutumika kwa imani ya mtu mwingine?

Kijana amekosema kuchana hicho kitabu lakini kama kutakuwa na majadiliano huru mahakamani, ni nani anayeweza kuonesha pasipo shaka Quran tukufu ni nini? Jee iliyohifahdiwa kwenye CD/Flash mtu akiifuta nayo itaheshabika ni kosa?

Kama taifa tutoke kwenye kushabikia vitu visivyojenga Imani zetu badala yake tuingie kwenye kupambana na huyo "Shetani" anayetufanya sisi tuwe watu waovu.
 
Back
Top Bottom