Mungu ninayemwamini amuhukumu mtu wa lugha yake, jinsia yake wala matendo yake maovu Mungu ninayemwamini anamuhukumu mtu kwa sababu moja tu ya kutokumuamini Kristo.
Matayo:28.19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Matayo:28.20
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Marko:16.15
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Marko:16.16
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Marko:16.17
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Marko:16.18
watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Matayo:24.14
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Ieleweke kwamba yeyote amuaminiye Kristo hawezi kutenda uovu