MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

Hii mbaya sana. Pole kwa wafiwa. Nini kifanyike? Kwa wenzetu gari za wanafunzi hupewa upendeleo wa pekee sana. Tunaweza kufanya kitu gani kuzuia misiba ya watoto kama hii?
 
Aiseee ila yaonesha alikuwa speed sana....
Nawaonea huruma wazazi, ndugu na jamaa za marehemu
Mungu awape ujasiri
Mzee hapo utakimbiaje?? Gari haikuwa speed, huku nina kiwanja ni sehemu mbaya sana, barabara ni mbovu na ina makorongo sana. Huwezi kimbiza gari hata uwe dereva gani.
 
Mungu tulindie watoto wetu hizi school bus nyingi ni migari mibovubovu tu halafu watoto hubanana kama ndizi humo ndani mtufikirie na wazazi jamani tunapambania hawa watoto wapate elimu ya kupambana East Africa , Africa na Duniani lakini hamtuhurumii wazazi ada kubwa, fare za hizo basi kubwa madereva mnaokoteza tu mitaani au ndugu mnaojuana wengi wao visirani na hawana upeo mkubwa school bus nyingi ni chakavu sana na chache unakuta dereva mmmoja kapangiwa route nyingi kushinda uwezo na anapambana na muda watoto wawahi shule, ukute alikua speed kuukabili muda, inalazimu mtoto aamshwe saa 10 kuandaliwa ili awahi iyo school bus lasivo anaachwa mzazi unaingia gharama nyingine kuna ulazima wa ku reform upya sheria za kuangaza hizi shule na ukaguzi wa mara kwa mara wahayo mabasi, mtoto anauma jamani sikia mitandaoni tu, hakuna mzazi anayefurahia kumzika mwanae tena umri mdogo hivo Mungu awatie nguvu waliofikwa na msiba huu mzito rest in eternal peace little souls, poleni wazazi ndugu jamaa na marafiki na wote walioguswa, hakuna duka la pumzi tuwe makini tuhurumiane jamani.
 
Point mkuu
 
Mwenyezi Mungu awe radhi nao,Inna Lilah wainna ilaih rajiuun
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…