MTWARA: Basi la Shule ya King David lapata ajali, watu 10 Wamefariki na wengine 19 Wakijeruhiwa baada ya gari 'kufeli breki'

Mbona haraka sana imetajwa sababu ni kufeli breki.
 
Kuna mzazi amepoteza Mtoto wake wa 1 na wa 2 na ndo hao pekee aliojaliwa. Najitahidi kuvaa viatu vyake miguu yangu inapwaya.
Nimetoka kusoma huko mtandaoni; nikashindwa hata kupata picha huyo mama ana hali gani muda huu. Mungu pekee ndiye anaweza kumpa faraja ya kweli na, kumfunga mikanda ya sirini na kumganga moyo wake. Viatu vyake havitutoshi kabisa.

Mungu apumzishe roho za marehemu wote, na awape afya njema majeruhi wote. Na kwa wafiwa wote; Mungu akawape nguvu na faraja yake isiyo na kikomo
 
Kwenye ile thread yangu ndefu, nilishawahi kutoa hint kuhusiana na swala hili la ajali; kwamba kuna events fulani mahali fulani ambazo huwa zinaonekana ku-coincide vizuri sana na hizi ajali; kwamba event hizo zinapokuwepo ndani ya wiki husika, ajali nazo huwa zinatokea ndani ya wiki hiyo. Kwa upnade mwingine, events hizo zinapokuwa hazipo na ajali nazo zinakuwa hazipo. Unless iwe kwamba kwa wiki hii, coincidence ya aina hii haikutokea. Siwezi kujua kama events zime-coincide na ajli hii sababu kwa wiki hii ninamiss ratiba ya wiki ya mahali ambapo ajali hizi huwa zinaonekana kuumana na matukio yake. Nimejitahidi kujaribu kusikiliza ratiba online lakini mtandao umegoma!
 
 
Uzembe Uzembe Uzembe Uzembe Uzembe.
Utasikia tunaanza kuisingizia bahati mbaya.
Utasikia kesho jeshi la polisi linaanza operation maalum dhidi ya haya magari.

Watoto wamekufa bila hatia bali uzembe wa mababa zao, mama zao na kaka zao.
Ndugu hivi ajali zote ni uzembe tumia basi ubongo wako hata kufikiri. Humu karibia wote watatoa lowama kua ni uzembe kitu ambacho sio kweli. Hamjajua chanzo lkn lowama zimekua nyingi sana. Mimi Kuna siku nimetumbukiza gari mtaron kwa kusababishiwa. Bus imeovatake uso kwa uso na Mimi ndo dereva ilinibidi nitumbukize kwenye mtaro.

Sasa ajali kama hiyo wapita njia wote walikua wanatoa lowama kwa uzembe wa dereva ameingiaje huko. Kila mtu alikua akiongea lake. Bila kujua chanzo ni nini?

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Huku nilipo magari ya wanafunzi spidi yao huwa ni ndogo, inakuaje huko mpaka madogo wanakufa kabisa daah.

Na vile watoto huwa wanakaa hovyo hovyo ni rahisi zaidi kupata madhara gari ikipata ajali, na huwa wanajazwa mno aisee.
 

Kila ajali inayotokea duniani lazima kuna uzembe mahala, inawezekana mzembe sio wewe ila mzembe mwingine amekusababishia ajali, bado itakuwa ni uzembe tu, jaribu kufikiri vizuri.

Mtu akilewa chakari akaendesha gari vibaya na wewe ukammkwepa na kuingia mtaroni, hapo mzembe sio wewe bali uzembe ni wa yule dereva mlevi matokeo ya uzembe wake ni wewe kwenda mtaroni.

Tunaposema uzembe jaribu kuvuta picha kubwa, hapo kwenye hiyo ajali kuna uzembe na umeshaambiwa gari ilifail brakes, kwanini ifail brakes, inafanyiwa ukaguzi kila siku, inafanyiwa maintenance, brakes pads zinabadilishwa kila muda gani, check list ya gari inasemaje?, idadi ya watoto ni kupakia ilikuwa sawa, dereva ana akili timamu, dereva ana afya njema, dereva sio mlevi, dereva analipwa vizuri na kwa wakati?, Hilo hata ukiliangalia tu kwenye picha linaonekana kuwa ni chakavu na hali mbaya.

UKWELI: Magari mengi ya wanafunzi ni yale yaliyochoka na hayawezi kufanya kazi za abiria, mengi ni mabovu na yasiyofaa.
 
Duh.king david maskin asubuh nawaona wenyewe nikiwa nakuja mikindani boma hotel pahali pangu pa kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…