Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

Nalaani hilo tukio, lakini pia tujifunze kutokutembea na pesa nyingi kwa ajili ya usalama.

Unatembeaje na milioni thelathini na tatu cash ni hatari sana.
 
Yale Yale ya wakina Abdallah Zombe kwa wale wafanyabiashara ya Madini wa Mahenge.
Jeshi letu la Polisi Nchini,linaongoza kwa uhalifu....
Katiba mpya ndio Suluhu ya haya madhira
In traffic, I don't panic when I see them police lights ,I got them pigs in my pockets like Jody Weis.
Gangster Disciples, Black Stones, BDs The biggest street gang is the C-P-D.







 

Attachments

  • VID-20220125-WA0121.mp4
    11 MB
  • VID-20220125-WA0018.mp4
    15.1 MB
Your browser is not able to display this video.

JESHI la Polisi Mkoani Mtwara limewakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.

Inadaiwa maafisa hao wa polisi walijipatia kiasi hicho cha pesa wakati wakimfanyia upekuzi mfanyabiashara huyo.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera imesema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara.

Maafisa wanaoshikiriwa ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje -Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango - Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza - Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya Mganga - Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Chanzo: Habari leo
 
Kwa mazingira yalivyokuwa na kwa muda uliopita toka tukio la mauaji litokee naamini Mhe. Waziri Mkuu ambaye ni mzaliwa Lindi anapotoka marehemu alishirikishwa na wananchi. Yawezekana Polisi walimdanganya kuhusu ukweli lakini kwa hiki kinachoendelea naamini kwa Nafasi yake anao uwezo wakuelekeza kuhamishwa Kwa RPC ambaye sidhani kama kwake malalamiko ya Ndugu wa marehemu akuyasikia.

Maafisa waliokamatwa ni wakuu wa vitengo na kwa taratibu za kijeshi na muundo wa Polisi maafisa ambao wapo nje na awajakamatwa ni Staff officer na RPC, waliobaki wote kwa taarifa inayosambaa wapo maabusu. Swali lakujiuliza wamekamatwa na Nani? Obviously wamekamatwa na wakubwa zaidi Yao na wakubwa hao lazima watakuwa wametoka makao makuu au wameelekezwa kutoka mikoa mingine.

Swali la pili, Hadi wanaelekezwa kwenda kuwakamata wasaidizi wa RPC huyo RPC alikuwa wapi? Naweza kutabiri kwamba alikuwepo ofisini lakini alipuuza kilio Cha walalamikaji aidha Kwa kusikia kupitia intelligence yake au kwa kufuatwa ofisini na walalamikaji.

Kama Timu imetoka nje ya Mkoa, kwanini Sasa RPC siyo mtuhumiwa angalau akarejeshwa makao makuu kuepusha kuvurigika Kwa kazi ya upelelezi? Lakini je kwa tukio lililotokea chini yake alipaswa yeye kujitokeza kwenye vyombo vya habari kulizungumzia? Ni kweli askari alijinyonga kwa tuhuma hizi na hakuna taarifa iliyotolewa hadi mwananchi walivyoandika?

Yapo maswali mengi Ila yote haya nimpongeze Mhe. Majaliwa Kwa kutimiza Wajibu wake bila kuviingilia vyombo husika. Kuiendea haki ni vyema sasa akashauri uwepo wa tume huru kuhusu suala la askari na kifo cha mfanyabiashara. Ni vigumu askari kupata kitanzi mahabusu.
 
Mkuu nimeona kwa jicho la mwewe rpc anatoa taarifa huku akiwa mwenye wasiwasi wa ajabu nadhani.. wazi anaona kuwa naye anatuhusishwa iwapo upepelezi wakina ukifanyika kwa taarifa za ndugu.
 
Ishu tangu tarehe tano ni kwa vipi RPC anakosekana kuwa ndani? Jee OCD Yuki wapi? Kiufupi hao wote ni wahusika wanatakiwa kuwa ndani mahabusu na kesi yao iendeshwe mapema na haraka wanyongwe ili kuleta nidhamu kwa jeshi la polisi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Haba ipo nusu hio, wakitaka nimalizie ri' yani kumaanisha "Habari" basi waseme baada ya kuwakamata hizo hela zipo wapi?

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…