Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7

hakuna shida kwa kijana wa 25yrs kumiliki 33mili tena mfanyabiashara ya madini..

kumbuka wengine wakimaliza lasaba tu wanaingia mtaani kutafuta, wengine form four inatosha... machimboni lolote linaweza kutokea kadili ya uhangaikaji wako na bahati..
 
RPC Mtwara aliutangazia umma kwamba kuna askari 7 wamepandishwa kizimbani wakishtakiwa kwa kosa la kumuua kijana mfanyabiashara wa madini musa hamisi huko mtwara.

Aidha kuna taarifa kwamba askari mmoja aliyekuwa mmoja wa watuhumiwa hao alijinyonga wakati wakiwa mahabusu kabla ya kupandishwa kizimbani.

Kwanini taarifa ya huyo RPC haikueleza kwamba walikamatwa na kuwekwa mahabusu askari 8 ila mmoja alijinyonga wakiwa mahabusu hivyo saba tu ndio wamepelekwa mahakamani.

Halafu kuna taarifa kwamba huyo aliyejinyonga (kama kweli alijinyonga au alinyongwa na wenzake) alikuwa na taarifa za kina kuhusu hilo sakata.

Halafu inawezekana vipi mtuhumiwa ajinyonge akiwa mahabusu?

Isije ikawa mambo ya kupoteza ushahidi kama ishu ya kina zombe.

RPC mtwara inabidi awajibishwe
 
Ila jeshi la polisi inabidi libalike, baadala ya kulinda raia wao wamekua sehemu ya kuua raia.
 
Hawawezi kuwa wapumbavu kiasi hiki,kwamba wamuue mtu kwa milioni tano kila mtu.

There is something behind that amount of money.
Hiv polis unawachukuliaje ndugu? Yaan ni wapumbavu mno tena zaidi ya hata neno lenyewe, polis anauwezo wa kukuua kwa ajili ya 5k, sijawah kumkubali askar polis maisha yangu yote, yaan siwapendi kiiiinyama.
 
Umeshaenda kwa wakulima wa vitunguu na Miwa ama mchele. Kuna vijana ni matajiri wa kutupwa wanamiliki pesa nyingi sana milioni 33 ni pesa ndogo mno kama una goli la maana. Ila ukweli kuna watu wengi sana wanakufa mikononi mwa haya mapolisi majizi. Kwa hili hata RPC wamtoe tu.
 
Jeshi Linakwenda Kumuua Mtu Mmoja Kwa Silaha Nzito Kisa Millions 70
Ambazo Raia Mwema Kazitafuta Kwa Jasho Lake
Ndiyo Maana Baadhi Yao Ukiona Wana Nyumba 5
Gari, Biashara, Wanalima Kumbe Kazi Kubwa Uporaji Wa Raia
 
Kwani ilikuwaje hadi huyo kijana kufa, uzi hauna nyama.
 
Mauaji ya polisi hayajaanza leo toka enzi za Kina Zombe Mama ndio alikua Rais kipindi hicho ?...enzi za Magu wapo polisi waliweka pembe za ng'ombe kwa mstaafu na kuchukua rushwa ya 100m matukio yao ni mengi kwa awamu tofauti inatakiwa uwe na kumbukumbu tuu...
 
Huyo benadi....kina zombe..hayo mambo walikua wanafanya zama za magu???.

Mbona umemaliza andiko lako kikolo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Said Mwema ndo alikua IGP makini.
Siro na Mahita ndo ma IGP wa hovyo sana.
 
Hawa ndio magaidi sasa. Unamuua raia badala ya kumlinda?.
 

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2018 huyo kijana aliuwawa ndani ya mahabusu ya kituo cha polisi mtera mpwapwa dodoma huko na askari aliemuua alikuwa anaitwa mwita,adhabu aliyopewa huyo askari ni kuhamishwa pale kituoni na ni mtumishi wa jeshi la polisi mpaka leo JESHI LA POLISI CHINI YA IGP SIRRO LIMEOGA DAMU ZA WATANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…