uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 17,060
- 32,400
RPC Mtwara aliutangazia umma kwamba kuna askari 7 wamepandishwa kizimbani wakishtakiwa kwa kosa la kumuua kijana mfanyabiashara wa madini musa hamisi huko mtwara.
Aidha kuna taarifa kwamba askari mmoja aliyekuwa mmoja wa watuhumiwa hao alijinyonga wakati wakiwa mahabusu kabla ya kupandishwa kizimbani.
Kwanini taarifa ya huyo RPC haikueleza kwamba walikamatwa na kuwekwa mahabusu askari 8 ila mmoja alijinyonga wakiwa mahabusu hivyo saba tu ndio wamepelekwa mahakamani.
Halafu kuna taarifa kwamba huyo aliyejinyonga (kama kweli alijinyonga au alinyongwa na wenzake) alikuwa na taarifa za kina kuhusu hilo sakata.
Halafu inawezekana vipi mtuhumiwa ajinyonge akiwa mahabusu?
Isije ikawa mambo ya kupoteza ushahidi kama ishu ya kina zombe.
RPC mtwara inabidi awajibishwe
Sasa una maana mtuumiwa akiwa na taarifa Za kina kuhusu tukio atakuwa shahidi WA jamhuri kujikaanga?