Muda ni Mwalimu mzuri sana: Siasa ni kama upepo, hubadilika wakati wowote

Bahari inapochafuka jambo la kwanza Nahodha anatakiwa kufanya ni kuhakikisha anapunguza mizigo mizito isiyo ya thamani ambayo inaelemea meli.
MALCOM LUMUMBA ,ukitumia jicho la tai mbona nahodha alichukua hatua na anaendelea kuchukua??

Kinachoisumbua nchi yetu kwa sasa ni matumizi kidogo ya akili coz inaonekana nchi inaongozwa kwa maamuzi ya kihisia zaidi!


β€œYour mind is the starting point of all war and all strategy. A mind that is easily overwhelmed by emotion, that is rooted in the past instead of the present, that cannot see the world with clarity and urgency, will create strategies that will always miss the mark.” ―

Robert Greene, The 33 Strategies of War
 
Huyu aliyeropoka kwamba "Polisi walirushiwa mawe" hakutakiwa awepo pale.

Kwenye kikao Bibie kaletewa kabrasha anaambiwa kwamba jamaa hafai.

Bibie kaanza BIG-BABBY TANTRUMS za kulia na kujifungia chumbani hataki kuongea na mtu.

Kisa, wanamdharau, kaomba aletewe ghahawa anywe peke yake ndani.

Kuona hali ni mbaya, ikabidi waliite lile lizee la Cold-War kazi maalumu ambalo halitaki kustaafu.

Lile lizee kufika na kuzungumza naye ndiyo kulazimisha hiki kituko kuwekwa pale ambapo unakiona leo.
========================================================================================

Huyu ni MWENZAO, MAKE NO MISTAKE...
​
 
daima maisha hayana extra time,
fanya upasalo kutenda maishani kikamilifu, kwa usahihi, kwa wakati na kwa muda muafaka, vinginevyo hutakua na historia πŸ’
Angalau hujaziita porojo nonsense gentleman
 
MALCOM LUMUMBA ,ukitumia jicho la tai mbona nahodha alichukua hatua na anaendelea kuchukua??
Makosa yalianza kwa kutosikiliza Wananchi kwa mazoea tu kwamba ndivyo walivyo.
Matatizo yalipotokea jambo la kwanza ilikuwa kuwajibika! Hakuna aliyewajibishwa ikieleza hakuna majuto
Hatua zinazochukuliwa hazina ''vote of confidence'' kutoka katika Umma! House of cards

MALCOM LUMUMBA kasema '' muda''
 
Alafu anatokea mtoto wa buku mbili anakwambia mwenye bandiko hili hana elimu🀣🀣🀣🀣
 
Ooh yeah, codes zimezingatiwa.
 
Umefanya uchambuzi ulionyooka kumkosoa huyo kubwa jinga Kijakazi

Huyo jamaa hata mkewe akichukuliwa mkewe na wahuni wakina secretarybird na Maghayo atatupa lawama kwa Muslim na communism Wanataka kusambaza Uislamu katika familia yake
 
Mkuu fanya kutoa na effects matokeo kwetu sisi raia wa kawaida iwapo mswaada wa USA utapita. Tujue namna ya kujipanga mapema
Mswada unatamka ''kupitia mahusiano kati ya Marekani na Tanzania'' . Hii si vikazo vya uchumi (economic sanctions). Mswada unaeleza maeneo yasiyoathirika ikiwemo huduma za kibinadamu na usalama.
Usalama ndipo tulipoponea kwasasababu Tanzania ilikuwa ''stable' katika ukanda. Marekani inatumia kwa Usalama.

Kinachokusudiwa ni vikwazo kwa wanaohusishwa na matukio. Wahanga watawekewa vikwazo vya kusafiri na vijisenti vinaweza kuwa ''freezed''. Hawa wataonja joto ya jiwe moja kwa moja kwasababu hata Familia zao zitaathirika.

Mtu wa kawaida utalionja joto ''indirectly'' kutokana na kuathirika kwa baadhi ya maeneno.
Marekani ndio wenye Bretton Wood Institution iliyoanzisha World Bank (WB) na Internationa Monetary Fund (IMF)

Ukopaji unaweza kuathirika na kuathiri miradi ya ndani inayotegemea pesa. Mtiririko utaathiri ajira za Watu kwa mnyororo hadi mama ntilie ingawa anaweza asione athari moja kwa moja

Marekani ina masoko makubwa ya Mitaji. Wawekezaji watakuwa na wasi wasi na huenda wakahitaji ''ulinzi'' wa dhamana zao kwasababu tayari tutaonekana ''unstable country''. Uwekezaji ukiathirika na unagusa hadi chini

Misaada itapotea hasa ile inayopitia serikalini. Kumbuka misaada hiyo ni sehemu ya ''fedha''
Tunatumia Dollar kwa shughuli za biashara za nje na hata ndani. Dollar ikiathirika kidogo tu Tsh inakuwa matatani. Sina uhakika lakini inflation hatuwezi kuiondoa katika equation na ina athari kwa watu wa kawaida

Kubwa zaidi mswada unapelekwa kama sheria na kufutwa lazima urudi katika mabunge.
Ingalikuwa executive order ya Rais hiyo inafutwa mara moja pengine na Rais ajaye. Hapo napo kuna tatizo
 
Ahsante sana kwa elimu.

Hapa ni kufunga mkanda hasa
CCM sio kabisaa
 
Duh!....Ila naamini usingeuwa mtu au kumpeleka Uhamishoni.
 
Umekumbusha kitu adhimu sana na mfano mzuri ni industrial revolution ilibadilisha nguvu ya dunia. Mabadiliko ambayo mataifa yaliyochelewa kutokwenda kwa mabadiliko ya viwandani historia ilionesha yalibaki nyuma.

Kuna mahali nilisoma wajuzi watafafanua zaidi, walionesha ya kwamba; mifumo mingi huanguka si kwa sababu haina nguvu bali ilichelewa kuutambua wakati sahihi. Yaani ilichelewa kutambua kuwa mazingira tayari yamebadilika.

Na historia ikitazamwa huwa inasema kwamba kila zama huwa zina teknolojia yake, fikra zake, kizazi chake n.k

Kwa bahati mbaya tatizo la mamlaka za kwetu zinadhani kuwa utulivu au kutumiwa nguvu na kulazimishwa utulivu kwenye mabano tuseme utulivu wa sasa basi ndiyo usalama wa muda mrefu. Wanaamini kwa kuwa mfumo unasimama basi upo salama.

Tunakoelekea si pazuri. Inabidi ieleweke kuwa mabadiliko ni sheria ya kijamii, ndiyo kanuni na nidhamu yake huwezi kupambana nayo. Njia iliyo bora ni kuyaratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…