Muda ni Mwalimu mzuri sana: Siasa ni kama upepo, hubadilika wakati wowote

Haiwezekani labda pia hayo hayakufanyika enzi hizo kabla ya 2015 kwa sababu hakukuwa na upinzani mkubwa na mkali sana kwa CCM kama uliopo sasa?
 
Nini imesababisha hali hii kwa Watanzania wengi ? Inawezekana daraja la chini halina ugumu wa maisha labda kama Kenya? Ni elimu? Ni state propaganda ya nchi imekuwa smart sana? Nini hasa sababu??
 
Ndauli Mwagito....​
Ulichokiandika nilianza kukiona uchaguzi wa 2010 na kuendelea. Kilichofanyika uchaguzi wa 2020 ilikuwa ni kuzuia nature kufanya kazi yake. Uchaguzi wa 2025 ilikuwa ni copy and paste ya kosa la 2020 na ndio tukafikia hapo. Kwa hapa tulipofikia wanatakiwa watu wanaoweza kuheshimu ukweli ili tuende sawa kama taifa, lakini iwapo hakuna atakayesoma alama hizi za nyakati na akataka jana iwe Leo ama kesho, basi taifa hili litaenda kuishia yalipoishia mataifa mengine kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Kiongozi fanya utafiti wako vizuri,
CDM ni chama kinachowagusa watu wote na haijapoteza dira yoyote, CDM ni chama cha upinzani hawana kitu maalum cha kusema tutafanya hivi kwa ajili ya wananchi, hawana ahadi yoyote ambayo utasema ni dai kwa wananchi, hawa ni watu wa kuwasemea wananchi dhidi ya mambo maovu ya serikali na kero zote ambazo wanaziona mahala popote ili hatua stahiki zichukuliwe.
Usisahu CDM walikuwa kifungoni, walikuwa hawana jukwaa lolote la kusema kwa muda mrefu,lakini hiyo haiondoi bond, Mahusiano ya wananchi na CCM ni kwa maslahi, katika nyakati hizi ukiona mtu yoyote anasapoti CCM waziwazi ujue kuna kitu anafaidi aidha ndani ya mfumo au nje ya mfumo au ana mtu anamtegemea sana yuko ndani ya mfumo.
Wananchi walio wengi wako na CDM, Ila huku CCM Ni maslahi zaidi, Hata sisi wananchama tusiofungamana na maslahi ya watu tunatambua nguvu ya CDM.
 
Mada nzuri ila umekosea sana kuchamgaya hizi takataka 2 toka tz na uganda kuziweka kapu moja na hao wengine.
 
Ulichokiandika ndicho nilichomaanisha

CDM inategemea kuvurunda kwa serikali ya CCM ili ipate kitu cha kuongea na kukiamini. Lakini pia narrative ya katiba waliyoichagua bado ipo weak na communication yake yenyewe ipo weak.

Ukifuatilia jinsi Mange alivyoiongelea katiba, Instagram iliwaka moto, narrative ya katiba ikashuka hadi kwa mtu wa mwisho ila kwa nini CDM hata iwe na hadhara kubwa lakini bado hawakupata kuishusha narrative yao hadi kwa mtu wa chini sana ??... Ni kwa sababu communication yao na department yao ya communication ipo weak

Ukiangalia tangazo la tonetone ilikuwa total failure na sijui ni nani aliwashauri. Sasa kama kitu kidogo kama kile walishindwa, inaonesha nini kwenye kitengo chao cha mawasiliano ???...

CDM ya kuondoa ufisadi ilikuwa na narrative strong, wananchi waliijua, viongozi wa CDM walipata kung'ara kwa sababu ya kuibua vitu vilivyokuwa vinaendelea na si tu kuisema serikali inapokosea kwenye vitu obvious. Kwa sasa hadi kiongozi akikosea matamshi tayari inakuwa ni agenda kwa viongozi wa CDM mtandaoni

Kwa hiyo mkuu, unaona lipo sawa. CDM ilipaswa kujiimarisha kwa sasa kwa sababu ina upper hand ila inaendelea kujikita kwenye makosa ya CCM na kuuza katiba kisomi badala ya kujisimika na kutengeneza trust kwa wananchi ambao pengine si wasomi wala si wafuasi wa CDM

Hili ndilo nasema hata CDM ni mtihani pia. Wakitaka kufanikiwa strategists na communication department yake waweke vichwa ila kama ni hivi. Bado kwa upande wangu

Na utaliona hili akitokea mtu proper wa kuuzwa kutoka CCM, watamtengenezwa narrative nzuri na CDM haitoifuta kirahisi. Ila CDM ikija vizuri na kiutofauti, hapo watawin
 
Nini imesababisha hali hii kwa Watanzania wengi ? Inawezekana daraja la chini halina ugumu wa maisha labda kama Kenya? Ni elimu? Ni state propaganda ya nchi imekuwa smart sana? Nini hasa sababu??
Vipo vitu vingi sana ila nitahighlight vichache

Ujamaa uliondoa individualism, watu wakaacha kufikiria kama individuals na kuanza kuona usisi na kutegemea serikali kwa kila kitu. Huku wafanyabiashara na matajiri wakipigwa vita kama wahujumu uchumi ilhali wenye vichache wakaonekana wazalendo.

Hii ilifanya umaskini uonekane ni tunu na ni kawaida, extreme dependency kwa government "maendeleo ya hisani na si kwa stahiki" Kwa hiyo presha kwa viongozi katika kuuondoa ikaondolewa

Elimu mbovu, mtanzania wa kawaida hafundishwi basic business or economics. So hajui hata uchumi unaendaje, ni tofauti na Kenya ambapo home economics inafundishwa. Inawasaidia kujua serikali inapataje mapato na ina_spend vipi na ina maana gani . Hivyo wanajua jukumu lao ni nini lakini la serikali ni lipi ndio maana kwenye mgomo wao wa mafuta unaona wapo detailed kuhusu kodi zinazopigwa ila watanzania wataumia "serikali itupunguzie bei ya mafuta".
Hawajui hata serikali inaongezaje wala kupunguza bei ya mafuta na ukiongezwa poor reading culture. Bhasi tunakuwa na uninformed & data blinded society


Kuna role ya imani za DINI & USHIRIKINA. Watu kuamini katika Better days na siku mbaya zinazosababishwa na shetani. So yakitokea yoyote kuna ile comfort "Mungu atatulipia, Mungu ataleta ridhki", hii inaondoa individual responsibility ya kuondoa vitu kwa sababu MUNGU YUPO NA ATATENDA KIMIUJIZA. Na ikishindikana wataenda kwa mganga. So ile hali ya kuishurutisha serikali ifanye A B C ni ngumu kwa sababu tayari unaamini destiny yako ishaandikwa na supreme power hii inatengeneza mazingira ya viongozi kutokuwa accountable.
Hata kijamii binti akibakwa au akiuliwa, watu wanakaa chini wanayamaliza, sheria za nini na aliyefariki harudi na pengine "Mungu amepanga"

Bado kuna integration ya serikali na Chama aliyoifanya muasisi. Na hii ndio inaila taifa hadi leo, aliamini katika kutengeneza chama imara kama msingi wa uimara wa nchi badala ya kutengeneza wananchi strong ambao watapambania nchi. So mambo yalivyogeuka, Simba wakaanza kuongoza kondoo wanavyotaka kiurahisi kwa sababu mentally and emotionally washakuwa disarmed

Issue ya malezi traditional ndio ikatumaliza kabisa, kiongozi wa familia "baba", hasemwi, hupaswi kumjibu hata akikosea, anaweza kukukufanya chochote anachotaka na ukimya wako ndio obidience. Na hizi zipo applied kwa jamii nzima. Sasa kama mtu huwezi kum_face baba yako, utaweza kum_face kiongozi mkubwa wa nchi. Hata viongozi wanalijua hili ndio maana kwenye utetezi wao lazma " Maadili, heshima, tamaduni, malezi" Vitawekwa kwa sababu wanajua ukigusa hapo, umegusa kwenye core ya mtanzania yoyote yule. Kwa hiyo kiongozi akikosea, usimseme kwa lugha yoyote. Ongea nae kistaarabu, kwa heshima, upole na ustahimilivu, atakusikiliza. Yani mtu amekosea ila inabidi umfate kwa unyenyekevu. Hii ni tofauti na nchi kama Kenya


Kwa hiyo Topic ni ndefu ila inahitaji kitabu kizima na kichambuliwe. Natural nimejitahidi kukujibu
 
Haya maisha hayatabiriki kabisa, miaka michache iliyopita Humphrey Polepole alikua anawatukana sana Chadema na kuona Ccm ni watu wa maana sana... Leo hii hao hao Ccm wamemuua...

You never know huko mbeleni, unaweza ukakuta Tundu Lissu ameshinda Urais... Mara Mama Samia kahamia zake Chadema.. Mara Jakaya Kikwete kafungwa Jela na Serikali ya Tundu Lissu kwa sababu ya kudai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Mara utasikia mwigulu Nchemba ambaye ni mwenyekiti wa Chadema Taifa anamtukana John Heche Katibu wa Ccm taifa ambacho ndo chama cha upinzani... Mara Rais Tundu Lissu amemteua Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi.
 
Ukiangalia haya matatizo ni mengi sana sijui kama kuna siku demokrasia ya kweli itafanya kazi Tanzania maana ili demokrasia iweze kufanya kazi na iwe na maana inahitaji raia wengi walio informed (wenye taarifa sahihi) na active participation yao kwenye mchakato wa demokrasia.

Ifike mahali hata watu watakaoruhusiwa kupiga kura wafanye kwanza tests za somo la uraia na kodi kupima uelewa wao wa msingi katika haya mambo.
 
Hapo umenipata vizuri,
Kuna sehemu nilishawahi kuongea na watu kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya wapiga kura ambao hawastahili kupiga kura. Yani hawajui chochote kile ila wanapiga kwa sababu ni haki yao.


Kwa namna hii ni ngumu sana demokrasia kufanya kazi ile inayowapasa kwa sababu yoyote anaeweza ongea lugha ya wanyonge na kuwalaghai kwa khanga na 10k.bhasi anachaguliwa

Lakini nachokiona hadi sasa chama tawala kinajikaanga kwa mafuta yake yenyewe. Maana wanaoiendesha wamesahau kuwa ile hali ya maisha kustahimilika kutokana na inflation rates kuwa chini na subsistency economy, ndio inayowasaidia kuishi comfortably

Ila hii hali ya kuzidi kubonyeza watu panapouma kiuchumi ni sawa na kuujaribu uvumilivu wao.. Ipo siku itaitika

Kingine usambazaji wa taarifa umekuwa mkubwa sana, kiasi kwa sasa narrative haiwi controlled na media ambazo zilikuwa zipo controlled na serikali. Kwa hiyo hata CCM inatakiwa kuwa na watu wenye akili sana na sio machawa kwa sababu ile media control advantage inazidi kupungua siku hadi siku. Ukiangalia power struggle utaona role ya traditional media impungua sana na mbaya zaidi inazidi kupoteza credibility ambayo ndio roho yake dhidi ya social media. Ndio hayo unaona influencers na activists wana power kubwa kuliko media moguls na wakaweka na Ithibati kiasi ni ngumu kwa media kutengeneza influential media personality maana wanategemea wanachuo wa habari pekee na sio kama zamani ambapo wangeweza kumpika mtu yoyote mwenye uwezo na star quality


Kingine malezi ya millenials kwa kizazi chao yamekuwa westernized. Ule ukimya na hofu vimepungua kwa kiasi kikubwa na hali itazidi kuwa mbaya pale millenials ndio watakuwa seniors na wala si mbali. 2030-2040

Kww hiyo kile kizazi cha zidumu fikra za mwenyekiti zinaondoka.


Ila watawala hawalioni hili kuwa CCM muda wowote itaenda kufa natural death na kama wapinzani wakiwa loyal na vizuri. Kazi yao sio kubwa sana kwa sasa ila kitakachoamua ni NEXT STEP YAO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…