Muda ni protocol ya usafiri kwenye msiba wa Malkia, kila kiongozi angetumia usafiri wake kungekuwa na foleni

Hata Mimi siwapendi mambo yao, lakini huwezi kunitowa akili ya kutofautisha msiba na official state visit.

Hao wote Leo wanakwenda Marekani UN, fuatilia mapokezi yao utaona tofauti ya protocol ilivyo.

Tusiache mioyo yetu ikajaa chuki ya kupitiliza.
Ile safari aliyofanya SSH huko Marekani ilikuwa inaitwaje tena, hebu nikumbushe. Je alipokewa na nani vile! Je alinusa hata harufu ya Jemadari Mkuu mwenzake?
 
eti wazungu hawaja hoji.....lazima tuhoji mambo yakula hela za walalahoi na kutanua nani anapenda hawa ndo ikitokea vurugu akatafuta hifadhi nitamnyanyasa ki......
 
MARAIS WA AFRIKA KUPAKIWA KWENYE BUS NI DHIHAKA?

Na Abbas Mwalimu
(0719258484).

Jumatatu tarehe 19 Septemba, 2022.

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu viongozi wa Afrika kupakiwa kwenye usafiri (bus) wa gari moja wakati wakielekea kwenye ibada ya mazishi Westminster Abbey.

Swali ni je walikuwa viongozi wa nchi za Afrika pekee?

Kwa nini matukio makubwa au mikutano hutumia mabasi?

Kimsingi hawakuwa viongozi wa Afrika pekee waliopanda kwenye mabasi bali viongozi wengi walioalikwa walitumia mabasi.

Tukumbuke kuwa tukio lile lilikutanisha Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali na Wawakilishi zaidi ya 500 kutoka nchi na taasisi mbalimbali duniani hivyo maandalizi ya usafiri yalihitaji kuratibiwa vizuri.

Kimsingi baadhi ya viongozi waliopanda mabasi ni Waziri Mkuu wa Ireland Micheál Martin, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, Mfalme Abdullah II wa Jordan na mkewe Malkia Rania.

Aidha wengine waliopanda mabasi ni Rais wa Malaysia Agong Al-Mustafa Billah Shah, Rais wa Singapore Halimah Yacob, Mfalme wa Japan Naruhito, Rais wa Poland Andrzej Duda, na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.

Vilevile, Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden na mkewe Silvia, Malkia Margrethe II wa Denmark, Mfalme Felipe na Malkia Letizia wa Hispania, Rais wa Italia Sergio Mattarella, Rais wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Mfalme Harald wa Norway na mkewe Malkia Sonja nao walipanda mabasi.

Matukio makubwa kama mikutano au msiba kama ule wa Malkia Elizabeth II ambao ulikutanisha viongozi wengi njia rahisi ya kuwafikisha katika tukio kwa muda uliopangwa ni kutumia usafiri wa pamoja.

Tufahamu kuwa matukio ya namna ile yanaongozwa na itifaki (protocol) na miongoni mwa mambo muhimu katika protocol ni muda.

Sasa tujiulize kama kila kiongozi angepangiwa muda wake na msafara wake (motorcade) hali ya msongamano ingekuwaje?

Ni muda gani ungetumika kukamilisha idadi ya viongozi wote kufika Westminster Abbey?

Hatudhani kuwa muda wa ibada ya mazishi ungeathiriwa na misafara ya viongozi?

Ifahamike kuwa katika matukio kama lile na yafananayo na lile utaratibu wa usafiri, malazi na usafiri huratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi husika.

Katika muktadha huu suala la usafiri wa viongozi wa nchi na serikali liliratibiwa Ofisi ya Masuala ya Kigeni, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (Foreign, Commonwealth and Development Office/ FCDO) ya Uingereza.

Utaratibu huu hufanyika ili kurahisisha usalama wa viongozi mbalimbali duniani kwa wakati mmoja na hii ni kwa sababu itifaki na usalama wa viongozi ni mambo yanayoenda pamoja na kamwe hayawezi kutenganishwa.

Hii si mara ya kwanza kwa viongozi kupakiwa kwenye mabasi kwa sababu hata katika Mkutano wa Jumuiya ya Madola mwaka 2018 (CHOGM2018) uliofanyika London na Windsor viongozi kutoka nchi zaidi ya 54 walipakiwa kwenye mabasi kwenda na kurudi kwenye mikutano kwa siku zote za mikutano.

Hayo yamekuwa yakifanyika hata Tanzania pia labda kwa bahati mbaya wengi huwa hawafuatilii.

Hivyo si dhihaka kama wengi wanavyodhani bali ni sehemu ya utaratibu katika kurahisisha usalama wa viongozi.

Zaidi, kitendo hiki cha kuwapatia usafiri mmoja viongozi hutoa nafasi kwa viongozi kuyasoma mazingira ya nchi au eneo husika na wao kupata muda wa kuchanganyika na kubadilishana mawazo ambapo kitendo hicho huitwa poding.

Wenu:

Abbas Mwalimu
(Facebook|Instagram|Twitter|Clubhouse).

+255 719 258 484.

Uwanja wa Diplomasia
(Facebook|WhatsApp).
View attachment 2362139View attachment 2362140View attachment 2362141
Uongo, si wangeingia na convoy zao wanashushwa gari zinatoka na zingine zinaingia fasta fasta tu.
 
Hata utetee nini. Tushajuwa miungu mitu yaweza panda Hiace. Coaster hata daladala. Mzungu katuonyesha😁😂🤣😅👉☝️✌👌👏👏👏
 
Mbona juzi tu mama kasafiri na boat ya Azzam kutoka Zanzibar?
 
Ile safari aliyofanya SSH huko Marekani ilikuwa inaitwaje tena, hebu nikumbushe. Je alipokewa na nani vile! Je alinusa hata harufu ya Jemadari Mkuu mwenzake?
Mimi siyo chawa labda unanifananisha, hiyo ni kazi ya machawa wa Samia.
 
Shukran nyingi ziende kwa wazungu kwakuwarundika miungu watu wa Africa kwenye mwendokasi.
 
..kuanzia sasa hatutaki utitiri wa MISAFARA hapa nchini.

..viongozi waanze kutumia usafiri wa pamoja ktk ziara za ndani.
 
Wewe ni miongoni mwa wale waliokosa lishe bora na kupelekea akili kudumaa.

Mnashindwa kutofautisha kitu kidogo tu msiba na official state visit.
Biden alikuwa amekwenda harusini sio msibani
 
Mimi siyo chawa labda unanifananisha, hiyo ni kazi ya machawa wa Samia.

..kwa mfano kwenda uwanja wa ndege kumpokea au kumuaga Raisi kwanini viongozi wasitumie usafiri wa pamoja?

..ua Raisi anapokuwa ktk ziara mikoani ni vema kama viongozi wa chini yake, na wasaidizi watatumia usafiri wa pamoja ili kubana matumizi.

..pia idadi ya viongozi wenye misafara ipunguzwe. Wakati wa Mwalimu Nyerere, Raisi, Makamu, na Waziri Mkuu, walikuwa viongozi pekee wenye misafara.

Siku hizi idadi ya viongozi wenye misafara imeongezeka kupita kiasi. Ongezeko hilo ni mzigo kwa walipa kodi.
 
Usafiri wa basi uendelee hata hapa nchini,badala ya V8, 80 tutumie mabasi manne ,Mkuu wa nchi ndiye apewe 'state car' ,tubane matumizi
Na maendeleo yatakuja kweli. ? Rushwa itapungua kweli.? Muda utatosha kweli??
 
We ndio huna akili,ishu sio kupanda basi ishu ni kwa nini wakija huku misafara yao inakuwa na magari 60,wakati wangeweza kupunguza gharama
Mkuu, sasa ukiweka mawaziri wote ndani ya bus moja kisha likatokea la kutokea hauoni kama unaweza kukuta tunapoteza serikali nzima ndani ya dakika chache tu/within fraction of a second?

Lakini hao marais waliopanda bus moja hata likitokea la kutokea kila nchi inakuwa imepoteza Rais mmoja mmoja tu. Kumbuka mawaziri wote ni marais watarajiwa.

NB: Siombei jambo lolote baya kwa viongozi wetu na hata wa nchi jirani. Mungu tunakuomba uepushie mbali wote warudi salama.
 
Back
Top Bottom