PostGE2025 Muda wa Samia kukaa Ikulu ulikwisha siku aliposema, ‘Kama hamkutaka Serikali tuwaue kwanini mliwaruhusu waingie barabarani?'

PostGE2025 Muda wa Samia kukaa Ikulu ulikwisha siku aliposema, ‘Kama hamkutaka Serikali tuwaue kwanini mliwaruhusu waingie barabarani?'

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

I. USULI

Hii ni Barua ya Kijasiriadola kwa Wakubwa zangu vikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Natumia njia hii kutoa salamu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa Watanzani wote wanaoamini kati uhuru wa kufikiri na kueleza fikra binafsi kama njia mojawapo ya “kuwaongoza viongozi” kwa njia ya kusanifu hoja thabiti, na hatimaye “kutakatifuza malimwengu” kwa njia hiyo.

Hasa, napendekeza kwamba, muda wa Samia kukaa Ikulu ulikwisha siku alipojitenga na Watanzania na kisha kuwauliza hivi, ‘Kama hamkutaka serikali iwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani?’

Najenga hoja kwamba, swali hili ni kielelezo thabiti cha dhamira yake ya kuendelea kutekeleza sera zenye sura ya ukoloni mamboleo na utumwa mambosasa nchini Tanzania, wakati mambo haya yanapingana na Katiba ya nchi, na ndio kiini cha matukio ya wiki ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Hatimaye natoa wito kwa Samia kujiwajibisha mwenyewe au kuwajibishwa na wadau baki, bila kuvunja katiba ya nchi, kama ilivyotokea huko Zimbabwe mwaka 2017.

II. UTANGULIZI

Miaka 64 iliyopita, yaani mwaka 1961, kijana Mtanganyika aitwaye Julius Nyerere alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanganyika” kutoka kwa wakoloni wa Kizungu.

Miaka mitatu baadaye, kijana Mzanzibari aitwaye Abedi Karume, alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Zanzibar” kutoka kwenye ukoloni wa miaka ipatayo 200 chini ya Waarabu wa Omani, waliokuwa wameikalia Zanzibar tangu 1698.

Hatimaye, vijana Julius Nyerere na Abedi Karume walitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanzania” iliyopaswa kuendelea kuwa huru dhidi ya ukoloni mamboleo na utumwa mambosasa.

Vijana Julius Nyerere na Abedi Karume walifanikiwa kuzika kabisa ukoloni mkongwe wa Kizungu uliofanyika kwa miaka 77 na kutokomeza utumwa mambokale wa Kiarabu uliofanyika kwa miaka 1000.

Hivyo, tangu 1964 mpaka Machi 2021, Watanzania waliendelea kuwa huru dhidi ya ukoloni wa Kizungu na utumwa wa Kiarabu, wakiwa wanaongozwa na kanuni ya kuheshimu utu wa kibinadamu unaounganishwa na Katiba moja ya kisiasa.

II. KANUNI YA UTANZANIA NA MATARAJIO YA WATANZANIA

Vijana wawili Julius Nyerere na Abedi Karume waliwafundisha Watanzania, na Watanzania wakakubali, mafundisho mahsusi kuhusu misingi ya utu wa kibinadamu, ambayo hapa nairejea kama Kanuni ya Utanzania.

Kulingana na mafundisho ya Vijana wawili Julius Nyerere na Abedi Karume, Kanuni ya Utanzania inaweza kufupishwa kwenye aya 13 zinazosema:

  1. Kwamba, wakati majini, malaika, miungu na Mungu ni watu wasio na miili, kila binadamu ni mtu mwenye mwili ambao ni kitovu cha hazina ya uhai, akili na utashi huru.
  2. Kwamba, Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia, inayotamka misingi mahsusi ya kiutawala, ndio njia pekee ya kujenga Taifa jipya la binadamu wanaojitawala pasipo hofu ya kukwekwa tena chini ya utumwa au ukoloni na Taifa jingine lolote.
  3. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea heshima ya binadamu, binadamu wote ni sawa katika mizania ya vinasaba vya kiutu, na heshima yao inapaswa kuhifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu.
  4. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea uswa wa haki, binadamu wote huzaliwa wakiwa na haki za msingi sawa, zikijumuisha uhai, uhuru na ustawi.
  5. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea ukuu wa mamlaka ya watu juu ya serikali yao, kwa ajili ya kukuza na kuhami haki, watu makini lazima wakubaliane kuunda Jamhuri ya Kidemokrasia, yenye kutawaliwa na serikali iliyopata madaraka ya kiutawala kutokana na kibali cha kura za watawaliwa, ambapo kura hizo zinazopigwa kwa kufuata utaratibu unaokubalika kikatiba.
  6. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea utawala wa sheria, binadamu wote ni sawa mbale ya Katiba, sheria na kanuni husika, ambapo, vifungu vya kikatiba vinayo nguvu ya kuvipiku vifungu vya kisheria na vifungu vya kisheria vinayo nguvu ya kuvipiku vifungu vya kikanuni.
  7. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea chimbuko la sheria za nchi, sheria za kibunge, kidini na kimila zinazopingana na misingi ya maadili asilia, kama inavyotamkwa kwenye Tangazo la Dunia Kuhusu Haki za Binadamu, huwa ni batili.
  8. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mgawanyo wa madaraka, mamlaka ya nchi lazima yagawanywe katika mihimili mitatu, yaani mhimili wenye madaraka ya utawala (serikali), mihimili wenye madaraka ya kutunga sheria (Bunge), na mihimili wenye madaraka ya utoaji haki (mahakama), itakayofanya kazi kwa kushauriana na kukosoana.
  9. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea uwajibikaji wa kimamlaka, mamlaka ya nchi lazima iwajibike kwa wananchi walioiweka madarakani.
  10. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea ustawi wa watu, lengo kuu la serikali ni ustawi wa wananchi walioiweka madarakani.
  11. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea njia kuu za uchumi, shughuli za Serikali zinapaswa kutekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na kwa kuzuia mtu mmoja kumyonya mtu mwingine.
  12. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mamlaka ya kufukuza serikali, watu wanayo haki ya kutumia mchakato stahiki kufukuza serikali inayohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kuajiri serikali mpya, ambayo, kwa maoni yao, itakuwa na weledi wa kukuza na kuhami haki zao.
  13. Na kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mamlaka ya kubadilisha katiba kwa lengo la kubadilisha muundo wa serikali, watu wanayo haki ya kufuta muundo wa kiserikali unaohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kubuni na kuweka muundo mpya wa serikali, ambao kwa maoni yao utakuwa na yamkini ya kukuza na kuhami haki zao.
Katika muda wote wa utawala wa waasisi wa Taifa letu, hizi kanuni za kikatiba ziliheshimiwa sana kiasi kwamba, kiti cha Uraisi kiligeuka kitako cha mwamba thabiti ulio chimbuko la uimara wa himaya ya Tanzania.

Siku zote hizo Watanzania waliaminishwa na kuamini kihalali kwamba Raisi ni mjuaji wa mambo yote nchini, Raisi ni mweza wa mambo yote nchini, Raisi ni mkazi wa sehemu zote nchini, Raisi ni mpenda watu wote nchini, Raisi ni “mhunzi” wa vitu vyote vinavyoonekana nchini.

Kwa sababu hizi Raisi alichukuliwa kuwa ni Baba au Mfalme aliye alama ya umoja wa kitaifa, nguzo ya matumaini, mlinzi mkuu wa uhai wa raia wote, na msimamizi mkuu wa usalama wa Taifa lote.

III. SERA 17 ZA UKOLONI MAMBOLEO, UTUMWA MAMBOSASA NA USALITI WA KANUNI YA UTANZANIA

Hata siku moja, Watanzania hawakuwahi kufikiri kwamba wangempata Rais atakayejitenga nao na kisha kuwakejeli kwa kuwauliza swali tata, kama ilivyotokea tarehe 02 Desemba 2025, pale Samia alipowauliza Watanzania kwamba: “Nyie Watanzania, kama hamkutaka serikali iwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani?”

Napendekeza kwamba, swali hili ni kielelezo cha ujasiri alio nao Samia katika azima yake ya kutekeleza program ya sera haramu, ambayo sasa inafahamika kwa jina la “NEW DECIDED MOPPERS.”

Hii ni programu inayoongelea sera haramu 17, kila sera ikiwakilishwa na herufi moja katika kifungu cha maneno yafuatayo “NEW DECIDED MOPPERS,” kwa maana ya sera zifuatazo:

(1) Nepotic autocracy in state administration; (2) Emigration of Indigenous Africans; (3) War on the Natural Moral Law as opposed to Shariah Law; (4) Detentive abductions and tortures; (5) Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges; (6) Court capture and litigation dramas; (7) Inquiry commission dramas; (8) Deregistration of critical associations; (9) Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges; (10) Disinformation, media capture and mind capture; (11) Military politicisation, capture and intimidation; (12) Organised violence against republican principles; (13) Parliamentary capture and legislative dramas; (14) Police and paramilitary forces brutality; (15) Embezzlement of financial and natural resources; (16) Religious oppressions; and (17) Security forces outsourcing for domestic oppressions.

Katika aya zifuatazo nitaeleza kila sera kwa ufupi.

1. Nepotic autocracy in state administration:

Samia anatekeleza sera ya kugawa vyeo kwa kuangalia undugu, urafiki na uswahiba, yaani “nepotism”.

Binti yake na mumewe ni Mawaziri; Mtalaka wa bintiye ni DC; Mshenga katika ndoa ya binti yake ni Waziri; na orodha inaendelea.

Maamuzi yote haya anayafanya Samia yeye mwenyewe kinyume cha ushauri thabiti anaopewa na wasaidizi wake makini.

Hii ni tabia ya udikteta wa mtu mmoja, yaani “autocary,” na hovyo kifungu cha maneno “nepotic autocracy.”

2. Elevation of Shariah Law over the Natural Moral Law:

Samia anatekeleza sera ya kuendesha nchi kwa kutumia mfumo wa sheria za kiislamu uitwao “shariah law,” ambao ni mfumo rasmi wa sheria za kuendesha nchi katika mataifa ambayo ni wanachama wa Jumuiya ya Waislamu iitwayo “OIC”.

Ukweli uko hivi: Katiba ya nchi (1977) inakataza uhalifu wa kijinai kama vile utekaji, mauaji holela, na ubadhirifu wa fedha na mali za umma, isipokuwa kama uhalifu huu ukifanywa na Rais mwenyewe.

Ruhusa hii ya kikatiba inapatikana kwenye ibara ya 46 ya Katiba inayompatia Rais kinga dhidi ya mshtaka yoyote ya kijinai. Rais anaweza kujizuia kufanya uhalifu huu kwa sababu za kimaadili tu.

Kama Rais ni Mkristo, ambaye hajui wala hathamini ukuu wa misingi ya maadili asilia kama inavyotamkwa kwenye Katiba ya nchi, atatumia maadili ya Kibiblia yaitwayo “Amri Kumi za Mungu”.

Na kama Rais ni Muislamu, ambaye hajui wala hathamini ukuu wa misingi ya maadili asilia kama inavyotamkwa kwenye Katiba ya nchi, atatumia maadili ya Kikurani yaitwayo “Shariah Law.”

Bahati mbaya mfumo wa "Sharia law" unao "upande mbaya" usiosikilizana na ustaarabu wa haki za binadamu, kama zinavyofahamika katika milenia ya tatu.

Ubaya wakE unatokana na ukali wa adhabu kwa baadhi ya makosa ya kijinai kama vile wizi, uzinzi, uasherati, mavazi, unywaji wa pombe, kusikiliza muziki ya kisasa, kukataa mafundisho ya dini ya Kiislamu na kujitoa kwenye Uislamu, na kukosoa itikadi na sera zinazotekelezwa na serikali ya chama tawala kama walivyokuwa wanafanya Humphrey Polepole, Deusdedit Soka na Mdude Nyagali.

Adhabu dhidi ya makosa haya zinaweza kujumuisha kupigwa viboko, kupigwa mawe hadi kufa, kuuwawa kwa kuchinjwa kwa jambia hadharani, kukatwa mikono kwa panga, kutekwa na kuwekwa kizuizini mahali kusikojulikana, au mhusika kutekwa na kutelekezwa msituni ili afe kwa kuliwa na wanyama wakali.

Hizi ni adhabu ambazo watu wengi huziona kuwa haziendani na viwango vya kisasa vya haki za binadamu.

View attachment 3521732
Jambiah: A Tool for public beheading as per Shariah Law

Kwa ujumla, “Shariah Law” ni mfumo unaongozwa na itikadi ya jino kwa jino, jicho kwa jicho, mkono kwa mkono, damu kwa damu, na matumizi ya "jambia" dhidi ya mtu asiyekubaliana na hoja hata bila kumpa haki ya kusikilizwa kwa ukamilifu.

Kwa sababu hizi zote, ni wazi kuwa “Shariah Law” ni mfumo ambao hautambui "ukuu" wa tunu ya uhai dhidi ya tunu baki.

Kimantiki nasi, “Shariah Law” ni mfumo unaoruhusu utekaji, utesaji, na mauaji ya kupangwa na serikali.

View attachment 3521725

Lakini, kwa mujibu wa ibara ya 3 ya katiba ya Tanzania (1977), Tanzania ni dola isiyofungamana na upande wowote wa kidini, na inayopaswa kuongozwa kwa kufuata misingi ya maadili asilia, kama inavyotafsiriwa na sisi Watanzania wenyewe.

3. War on Indigenous Africans in favor of Foreign Direct Investors:

Samia amefunga mikataba ya uwekezaji wa kigeni inayowasukuma watanzania wazawa nje ya njia kuu za uchumi. Mfano ni mkataba wa DP World katika bandari ya Dar Es Salaam, mkataba wa makaa yam awe huko Tanzania Kusini, Mkataba wa kuuza madini huko Mwadui, Mkataba wa Mwendokasi Dar, na mikataba kama hiyo.

Pia kuna mkataba wa kuwahamisha Wamsai wa Ngorongoro na kuwapeleka Tanga kinyemela ili kupisha wawekezaji wa Kiarabu katika biashara ya uwindaji na biashara ya kaboni kwenye bonde la Ngorongoro.

Hii ni biashara ya “trophy hunting and carbon trade” inayoendeshwa na Waarabu wa Dubai.

Kwa ujumla, Samia anatekeleza sera ya kuwageuza Watanzania watumwa ndani ya nchi yao. Jambo hili halikubaliki kwa kuwa ni aina mpya ya ukoloni mkongwe.

4. Detentive abductions, tortures and enforced dissappearances:

Samia anatekeleza sera ya kuwateka na kuwaweka katika kambi za watumwa waafrika wengi wanaomkosoa.

Kuna watu wengine wanapotea bila maelezo yoyote kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kulinda raia na mali zao.

Kwa mujibu wa ripoti ya chama cha wanasheria wa Tanganyika na UN tangu 2016, alipopotea Ben Saanane, tayari wamepotea Watanzania zaidi ya 200. Hii maana yake ni kwamba, Rais aliyekula kiapo cha kulinda usalama wan chi, raia na mali zao ameshindwa kazi hiyo.

5. Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges:

Samia anatekeleza sera ya kuua wakosoaji wake wazi wazi kama mbinu ya kubaki madarakani.

Kifo cha Mohammed Ali Kibao ni tukio muhimu sana kueleza ukweli huu. Tangu KIbao auwawe serikali haijawahi kutwambia lolote.

Ukimya huo maana yake ni kwamba ama serikali inahusika moja kwa moja au inahusika kwa njia ya mzunguko.

Lakini sio hivyo tu. Mauaji ya waandamanaji wakati wa wiki ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 ni mauaji ya kupanga.

Waandamanani walibatizwa jina la "vibaka" na kumiminiwa risasi za moto kama vile ni nyani. Takwimu rasmi hazijatangazwa na serikali.

Lakini sasa tunafahamu kuwa mauaji ya raia katika wiki ya uchaguzi ni makubwa kuliko mauaji ya raia yaliyofanywa na Idd Amin wakati wa vita ya Kagera, mwaka 1978-79.

Katika vita hiyo, waliuwawa raia wapatao 1,500. Kwa hiyo, mauaji ya Oktoba mwaka huu ni zaidi ya vijana 1,500. Yote haya ni mauaji holela yaliyo haramu kisheria.

Tunayaita "extra-judicial killings" na yanafanyika kwa sababu ya uwepo wa kinga ya kikatiba dhidi ya mashitaka ya jinai yanayomlenga Rais aliye madarakani.

Tunayo katiba ya hovyo sana, lakini Samia anaipenda sana katiba hii kwa sababu ya uhovyo huo.

6. Court capture and litigation dramas:

Samia anatekeleza sera ya kuziteka mahakama na kuzitumia kuendesha kesi za kubumba na hatimaye kutoa humu za kisiasa, na hivyo kuunajisi mfumo wa utoaji wa haki.

Kesi ya uhaini inayoendelea dhidi ya Tundu Lissu na Kesi dhidi ya Bodi ya wadhamini wa chadema iliyosababisha Chadema kuzuiwa kutekeleza shughuli zake za kisiasa ni mifano hai.

7. Inquiry commissions dramas:

Samia anatekeleza sera ya kutumia Tume za Uchgunguzi kuwazunga wananchi. Mfano mzuri ni Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 2025 wakati wa uchaguzi mkuu.

  • MKurugenzi wa uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi wapo na wanajua kilichotokea vituoni nchi nzila,
  • Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na Ma-RPC wapo na wanajua kilichotokea barabarani chini ya usimamizi wa Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Hajj,
  • Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Wizi wa Kutumia Silaha (Special Anti-Armed Robbery Unit-SARU) yupo na anajua kikosi chake kilifanya nini mitaani katika wiki ya uchaguzi na kwa maagizo ya nani,
  • DGIS, ZSOs, RSOs, DSOs, na filed officers wa TISS wapo na wamekusanya taarifa za kilichotokea kwenye makaburi ya halaiki wakati intaneti na umeme vimekatwa,
  • Waziri wa Ulinzi, CDF, Wakuu wa Komandi za JWTZ wapo na wanajua kilichotokea mitaani nchi nzima,
  • Waziri wa TAMISEMI, ma-RCs, ma-DCs, ma-DEOs na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa na wilaya wapo na wanajua kilichotokea kwenye mikoa, wilaya na tarafa zao katika wiki ya uchaguzi, na
  • Mkurugenzi wa Jukwaa la Wahariri, Wahariri na Waandishi wa habari wapo na wanajua matukio yote muhimu japo walikatazwa kuyachapisha magazetini.
Hivyo, taarifa za kawaida za kiutawala zinatosheleza mahitahi ya taarifa anazozihitaji Rais ili aweze kutekeleza majukumu yake.

Kwa sababu hizi zote hakuna sababu nzuri ya kuunda Tume inayopewa miezi mitatu kufanya kazi ya kutafuta ukweli unaojulikana, kama sio mkakati wa kuendesha nchi kiujanjaujanja.

8. Deregistration of critical associations:

Samia anatekeleza sera ya kufuta au kudhoofisha vyama vya kijamii, taasisi za dini, vyama vya siasa, na vyombo vya habari ili kudhoofisha sekta ua asasi za kiraia, na hivyo kupata unafuu wa kutawala bila kukosolewa.

Amesitisha au kudhoofisha shughuli za Kanisa la ufufuo na uzima, Chadema, Jamiiforums, JamboTV, Twitter(X), Telegram, Clubhouse, na tovuti 80,000 kwa mdai kwamba zina maudhi yasiyo adilifu, gazeti la The Chanzo.

9. Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges:

Samia kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi anatekeleza sera ya kuiba uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani tangi 2024. Mwitiko wa wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2025 haukuzidi 20% ya wapiga kura wote waliojinadikisha.

Hata hivyo, Tume ilitangaza matokeo yanayoonesha ushindi wa asilimia zaidi ya 80% kwa wagombea wote. Huu ni ulaghai usiofichika na wenye kuondoa uhalali kwa serikali ya sasa.

Mara tatu, kupitia hotuba zake, Samia amejaribu kutetea ushindi wake pasipo mafanikio. Kila anapojaribu kufafanua ndivyo anavyoongeza mashaka kuhusu uhalali wake.

Ujasiri huu wa kuiba uchaguzi, hasa kura za Rais, unatokana na kinga ya kikatiba iliyo nayo Tume, pale inapokuwa imetangaza mshindi wa kiti cha Urais.

Ibara ya 47(1) inazuia mahakama za Tanzania kusikiliza kesi yoyote ya kupinga tangazo la ushindi huo.

Lakini, ibara hii inapingana na ibara ya 5(1) na ibara ya 8(1) zinazosema madaraka ya serikali yatatoka kwa watu kwa njia ya kuopiga kura.

Pasipo fursa ya kuomba mahakama ihakiki usahihi wa kura zilizotangawa, wanancho wanaweza kuporwa “ukuu” wao kama “wenye nchi” bila kuwa namna ya kujitetea.

Sasa Samia anatumia mwanya huu kufanya uhalifu wa kisasa wazi wazi halafu anasema kuwa yeye ni Rais halali. Hapana. Ushahidi ulioko mitaani kutoka kwenye vituo vya kupigia kura haukubaliani na utapeli huo.

10. Disinformation, media adoption and mind capture:

Samia anatekeleza sera ya kuteka akili za umma kwa kuwanyima habari sasa na kuwalisha habari zilizochujwa.

Samia amelazimisha vyombo vyote vya habari kufanya kazi kama idara ya serikali inayosimamia mahusiano kwa umma. Kwa sasa zinaandikwa habari zisizo na ukosoaji wa aina yoyote dhidi ya serikali.

Hata Jukwaa la wahariri (TEF) limefyata mkia kabisa. Kimapokeo, sekta ya habari inayo majukumu matatu.

Kuna majukumu sita yanayoifanya sekta ya habari kuwa mhimili wa nne wa dola.

Mosi, ni kuandika habari za udukuzi (watchdog), yaani kutafiti na kuchapisha habari za rushwa, kashfa, uzembe, na kuwakosoa wakubwa kwa lengo la kuimarisha utawala bora.

Pili, ni kuchuja, kuhariri na kuandika habari zenye maslahi kwa umma (gatekeeping), katika namna ambayo ni salama na yenye faida kwa umma.

Tatu, ni kuandika habari zenye kuibua matatizo ya kijamii na kupendekeza majibu yake kwa watawala (agenda setting), yaani kuifanya jamii ione matatizo yake na kuyapa vipaumbele sahihi katika kuyatatua.

Nne, ni kutunza kumbukumbu za maisha ya jamii (scorekeeping), yaani kufuatilia siku hadi siku matukio muhimu na kutunza shajara maalum kwa ajili ya matumizi ya baadaye, kwa lengo la kuonyesha nano anafanikiwa, nani anashidwa, na kusaidia kuionyesha jamii wapi inapaswa kwenda kwa kuzingatia ilikotoka.

Tano, ni kueneza utamaduni wa jamii (cultural Transmission), yaani kuandika, kueneza imani, tunu na maadili ya jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Na sita, ni kuwa jukwaa la majadiliano huru ya umma (public forum/agora), yaani kuisadia jamii kupata jukwaa linaloweza kutumiwa na jamii kama soko la mawazo mseto, majadiliano na hatimaye kama njia ya kusukuma mawazo ya pamoja ili yafike serikalini na kufanyiwa kazi.

Lakini sasa, Samia amevipiga marufuku vyombo vya habari kutekeleza majukumu yote haya.

Anachokisema yeye ndio kinapaswa kuchukuliwa kama ukweli, na wengine wote ni waongo. Huu ni uvunjaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania (1977).

11. Military politicization, capture and intimidation:

Samia anatekeleza sera ya kuliingiza jeshi katika siasa, kulidumaza kiweledi kwa kutumia ukanda na udini, na hatimaye kulifanya lishindwe kutekeleza jukumu lake la msingi la kulinda uhai wa Taifa dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania, aliliagiza jeshi kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Agizo hili lilitolewa mnamo Januari 22, 2024, wakati wa Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama (CDF) na Makamanda jijini Dar es Salaam. Malengo makuu ya agizo hilo yalionekana kuwa ni mawili.

Mosi, kuhakikisha usalama wa nchi unakuwa wa kutosha wakati wa mchakato wa uchaguzi, kwani chaguzi zinahusisha vyama vingi na mitazamo tofauti, na hivyo kuna uwezekano wa kutokea changamoto zisizotarajiwa.

Na pili, Kutoa tahadhari viongozi wa jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama ili wawe tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

Rais alisisitiza kuwa maandalizi hayo hayamaanishi matumizi ya nguvu, bali ni kuhakikisha taratibu, sheria na miongozo ya uchaguzi inafuatwa huku jeshi likiwa limekaa tayari kudhibiti uvunjifu wa amani.

Hata hivyo, tamko la CDF tarehe 30 Oktoba 2025 lilionyesha wazi kwamba alikuwa tayari kuliingiza jeshi barabarani ili kukabiliana na waandamanaji, ambayo yeye aliwaita “vibaka wenye silaha.”

Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Vibaka (Special Anti-Armed Robbery Unit-SARU) kiliingia mitaani 29 Oktoba 2025 wakiongozwa na kaulimbiu ya “vibaka wenye silaha wauwawe.”

Waandamanaji wakavalishwa “joho la vibaka wenye silaha” na wakauwawa kama kuku bila kutofautisha kati ya kibaka na mwandamanaji. CP Awadhi Hajj anajua vizuri zaidi walichofanya hawa vijana wa SARU.

Wakati SARU wanaendelea kukabiliana na “vibaka wenye silaha” JWTZ wachache waliokuwa barabarani wakajikuta wanakabiliana na majeshi ya kukodi kutoka nje pia.

JWTZ waliwaua baadhi ya wanajeshi wa kigeni na wengine kuwaweka mateka. Lakini JWTZ wakaambiwa na wakubwa kwamba hao mateka waachiwe kwa kuwa ni kikosi cha “kazi maalum.”

Jeshi la polisi lilishirikiana kuwakabili waandamanaji kwa msaada wa taarifa za kiintelijensia zilizokuwa zinakusanywa kwa kutumia magari ya kivita tuliyouziwa na kampuni ya Uarabuni inayoitwa STREIT, mradi ambao ulisimamiwa na Swahiba wa Samia aitwaye Angela Kiziga.

Magari haya huwa yanapaki kandoni mwa barabara, hasa katika sehemu za makutano, yakiwa na kamera na antenna za kurusha mawimbi mbashara kwenda kwenye kituo cha taarifa jumuishi (control center).

Kwa upande wa Dar Es Salaam mara nyingi magari haya utayakuta Ubungo mtaa, Magomeni, Ocen Road, Faya, Posta Mpya na Kariakoo.

Baadhi ya magari haya yanamilikiwa na JWTZ wakati mengine yanamilikiwa na polisi.

Kwa hiyo, JWTZ walikuwa na nafasi ya kukusanya taarifa haraka na kubaini ukweli kwamba dhana ya “wale sio waandamanaji bali ni vibaka wenye silaha” haina ukweli mwingi.

Hivyo wangegundua kwamba mauaji holela ya waandamanaji ni haramu na hatimaye kuingilia kati kwa mujibu wa dhaman yao ya kikatiba.

Lakini, JWTZ hawakufanya hivyo, kwa kuwa CDF alikuwa tayari amemezeshwa msimamo kwamba “wale sio waandamanaji bali ni vibaka wenye silaha.”

Adande CDF aliendelea na msimamo huu hata baada ya makapteni wake waliokuwa “field” kumpa taarifa mbadala, na kumtaka atoe tangazo la “kuchukua nchi” ili kutuliza “upepo mbaya.”

Hata hivyo, afande CDF alikatazwa na washauri wake wakuu ambao ni wakuu wa komandi za kijeshi, mkurugenzi wa intelijensia jeshini na mkuu wa utumishi jeshini.

Wakubwa hawa wote walikubaliana na kaulimbiu kwamba “wale sio waandamanaji bali ni vibaka wenye silaha.”

Kwa hiyo, ni sahihi kuhitimisha kwamba, tekinolojia ya kijeshi kutoka UAE imechangia katika kufanikisha vifo vya Watanzania katika wiki ya uchaguzi kwa njia ifuatayo:

Jeshi la polisi wameitumia kukusanya taarifa za watu walioitwa “vibaka” na wakafanikiwa kuwashughulikia kwa kutumia risasi za moto.

Lakini, hata JWTZ walitumia tekinolojia hii kukusanya taarifa za “waandamaji” ili waweze kuwapa ulinzi stahiki ili wafanikishe azima yao ya kupigania Tanzania mpya kwa njia ya maandamano ya kufa na kupona.

Hata hivyo, taarifa hizi hazikuwa na msaada maada wakubwa walishaweka msimamo unaowashangaza watu wengi hadi leo.

Kwa sababu hii, tangu siku hiyo ya tarehe 30 Oktoba, makapteni wengi hawana imani na afande CDF, hawana amani na wakuu wa Komandi za JWTZ, hawamwamini Mkuu wa Intelijensia wa JWTZ, na wanamtazama Mkuu wa Utumishi Jeshini kwa kumshangaa hadi wanashindwa kumshangaa.

Kwa ujumla, ukweli kwamba JWTZ walishindwa kuzuia mauaji ya Watanzania zaidi ya 1,500 yaliyofanya kwa kupangwa ndani ya siku tatu mfululizo, ni ushahidi tosha kwamba, jeshi letu limetekwa kiasi kwamba kwa sasa ni sahihi kusema kuwa “JWTZ sio jeshi la wananchi.”

Hili ni tatizo kubwa la kiusalama, na lazima litatuliwe kwa kushughulikia chanzo chake.

12. Organized violence against republican principles:

Samia anatekeleza sera ya ama kudhoofisha au kufuka mfumo wa kijamhuri nchini Tanzania.

Ndani ya chama chake CCM alizuia ushindani ili apite kama mgombea pekee asite na mpizani. Nje ya CCM, akafanya vivyo hivyo. Kwanza alimfunga mpizani wake mkuu Tundu Lissu.

Kisha akatumia mbinu za ubaguzi wa kitaasisi kumwondoa mpinzani wake wa pili, Luhaga Mpina, kwenye uchaguzi.

Badala yake akatengeneza wagombea dhaifu kupitia vyama vya upinzani vyenye “kazi maalum.”

Akashindana nao na hatimaye akatangazwa mshindi kwa 98%, wakati wapiga kura waliojitokeza vituoni hawazidi 10%.

Hapa hakuna demokrasia. Kanuni ya Jamhuri kwamba madaraka hutoka kwa watu kupitia ushindani wa kidemokrasia imekiukwa. Matendo haya yanakiuka Katiba ya ncho ambayo Samia aliapa kuilinda.

13. Parliamentary capture and legislative dramas:

Rais Samia anatekeleza sera ya kuendesha nchi kwa kuliteka Bunge. Alianza kwa kulilazimisha lipitishe mkataba wa kimataifa wa DP World, kisha mikataba ya bandari ya Bagamoyo na makaa ya mawe ya Kiwira.

Baadaye Samia akalilazimisha lipitishe marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa iliyompa madaraka ya Kimungu.

Na hivi karibuni amekuwa na maamuzi ya veto kuhusu nani awe mgombea ubunge na yupi asiwe.

Lengo ni kuwa na wabunge walio upande wake, wasiohoji lolote. Uhuru wa Bunge umeingiliwa, kiasi kwamba kanuni ya kikatiba kuhusu mgawanyo wa madaraka haina nafasi. Uvunjwaji wa katiba wa kiwango hiki haukubaliki.

14. Police and paramilitary forces brutality:

Samia anatekeleza sera ya kulitumia jeshi la polisi kama idara ya CCM. Ni jeshi ambalo limejenga chuki kuu dhidi ya raia wasio wana CCM.

Jeshi linatii maagizo ya viongozi wa CCM hata pale ambapo sheria zinakataza utii wa aina hiyo.

Wahalifu waliovaa nguo za kijani ni raia wema kwa mujibu wa polisi, lakini wasiovaa nguo za kijanii ndio wanavunja sheria. Polisi wanakamata watuhumiwa kininja, usiku wa manane, mbele ya wanafamilia.

Badala ya kuwa walinzi wa raia wema na mali zao, sasa wamegeuka kuwa walinzi wa wana CCM na mali zao. Huu ni utovu wa nidhamu usiokubalika.

15. Embezzlement of financial and natural resources:

Samia anatekeleza sera ya ubadhirifu wa fedha na mali za umma kwa kasi kana kwamba baada ya kuindoka ofisini atahama nchi.

Mara tu alipoingia madarakani alipandisha mshahara wake kutoka milioni 10 kwa mwezi alizokuwa anapokea hayati Magufuli hadi milioni 30 kwa mwezi. Hili ni ongezeko la 300%.

Kwa kuamuzi huu viongozi wastaafu wanaopata 80% ya mshahara wa kiongozi anayekalia ofisi aliyokuwa anaokalia mstaafu, walipata ongezeko la 300% pia.

Ameuza hisa za mgodi wa almasi wa Mwadi kwa bei ya kutupa; ameuza mgodi wa makaa yam awe kiwira kwa bei ya nyanya; ameuza misitu yetu kwa waarabu wanaofanya biashara ya hewa ya ukaa; ameuza wanyama wetu walioko kwenye mbunga za wanyama kwa wanaofanya biashara kuwinda.

Lakini sio hivyo tu. Samia amekopa matrilioni ya fedha na kupanua deni la Taifa hadi kufikia TZS 125 trillion.

Kwa ujumla, katika miongo sita ya uhuru, tangu 1961 mpaka 2025, deni la Taifa limekua kutoka $0.2 billion mwaka 1961 mpaka $53.5 billion mwaka 2025, ambayo ni sawa na ongezeko la 26,650%.

Tangu 2021, wakati wa Rais Samia deni hili limekuwa likikua kwa $6.25 billion kwa kila mwaka. Kwa njia ya ulinganisho wa ukuaji wa deni toka awamu moja hadi nyingine, takwimu ziko hivi:
View attachment 3521738

Kasi ya ukuaji wa deni hili wakati wa Samia inazua maswali mengi kuliko majibu. Lakini taarifa za kuaminika zinataja sababu mojawapo kwamba ukopaji huu unaambatana na utakatishaji wa fedha wa kiwango cha kutisha.

Taarifa zinasema kuwa, theluthi moja tu ya mkopo huu ndio imeingizwa nchini kwenye miradi. Theluthi ya pili imeingizwa nchini na kisha ikahamishiwa Uturuki kwenye biashara zake za majumba (real estates).

Na theluthi ya tatu imeingizwa nchini na kisha ikahamishiwa UAE kwenye biashara zake za majumba (real estates).

Huu ni uporaji wa rasilimali za nchi ambao unavipa vyombo vya ulinzi na usalama sababu tosha ya kumwondoa Samia ofisini na kuanza mkakati wa kurejesha fedga hizo zilizoporwa.

Ni katika mazingira haya swali moja kuu linazuka. Kuna haja ya TAKUKURU, FIU na Polisi kuhangaika na rushwa, money laundering, na makosa kama hayo yenye kuhusisha “pesa ya mboga” wakati Rais anatakatisha na kuhamisha matrilioni kinyemelea namna hii?

Jawabu langu ni ndio, ikiwa TAKUKURU, FIU na Polisi watatusaidia kurudisha hayo matrilioni.

Vinginevyo TAKUKURU, FIU na Polisi waachanane na kazi ya kufuatilia utakatishaji wa fedha na rushwa zinazohusisha “mafisadi vidagaa” wakati “mafisadi papa” wanaikausha nchi.

16. Religious oppressions:

Samia anatekeleza sera ya ukandamizaji wa kidini, akiwa anazilenga dini za Kikristo zinazomkosoa kwa hoja. Ametangaza vita na TEC wa Kanisa Katoliki akidai kwamba “wana-override nchi” kwa kufundisha juu ya misingi ya maadili asilia.

Na amefunga Kanisa la Ufufuo na Uzima, na hivyo kuwaondolea maelfu ya Watanzanoa fursa ya kuabudu, kulea watoto wao kidini, na kuwadhoofisha kiuchumi wachungaji na maaskofu wa Kanisa hilo. Kwa hiyo, Samia anatekeleza sera ya kuua familia za Kikristo kwa njia ya mzunguko. Huu ni ukiukwaji wa Katika ya nchi.

17. Security forces outsourcing for domestic oppressions:

Samia anatekeleza sera ya kuhemea majeshi ya kigeni na kuyaingiza nchi kinyume cha taratibu zinazofahamika kisheria. Kuna ushahidi usiokanushika kwamba wakati wa wiki ya uchaguzi Samia aliingiza majeshi kutoka Uganda, DRC, na Zambia.

Wanajeshi hawa walikuwa hawaguswi na mapolisi wa usalama barabarani mara tu baada ya kuonyesha vitambulishi vyao vya kijeshi vilivyotolewa na nchi zao.

Walipofika nchini mwetu kazi yao ilikuwa ni moja tu. Kufanya “spree shooting.” Walikuwa ni wauaji wa kukodi.

Kwa hiyo, haya yalikuwa na mauaji ya kupanga yakiwa yanajumuisha idara nyingi za serikali. Hata hivyo, majeshi yote ya kukodi hayakuwa yanawajibika kwa CDF. Badala yake, yalikuwa yanaratibiwa na Mtoto wa Samia aitwaye Andul.

Huu ni uvunjifu mkubwa wa Katiba ya nchi inayoweka jukumu la kulinda uhai wa Taifa mikononi mwa JWTZ. Samia anayo kesi ya kujibu mbele ya makapteni.

IV. SAMIA KIINI CHA MPASUKO KATI YA MATARAJIO NA MANG'AMUZI YA WATANZANIA

Ufafanuzi katika sehemu ya I na sehemu ya II hapo juu unaeleza ukweli kwamba kuna mpasuko kati ya matarajio ya watu kuhusu uendeshaji wa nchi kwa mujibu wa katiba na na mang’amuzi yao kuhusu hali halisi ilivyo.

Mpasuko huu ndio ilikuwa sababu ya maandamano ya GenZ wakati wa wiki ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

GenZ waliingia barabarani kupigania "Kanuni ya Utanzania" kama ilivyofunbdishwa na vijana Julius Nyerere na Abed Karume, na kama inavyoonekana kwenye katiba ya Tanzania ya leo.

GenZ waliingia barabarani kupinga uvunjwaji wa Katiba ya nchi unaofanywa na serikali ya Samia.

Waliamua kufanya maandamano ya kufa na kupona ili kutetea ukweli huu, wakiwa tayari kutoa uhai wao kwa ajili ya ukombozi wetu tuliobaki hai. Walikufa kifo cha kishujaa. Tulioko hai lazima tuendelee kuwakumbuka na kuenzi ajenda yao.

Tayari mara kadhaa Samia amemfahamishwa kwa udadavuzi wa maandishi laini kuhusu msingi wa ukweli wanaopigania GenZ.

Ameelezwa kwamba anapaswa kuendesha nchi kwa kufuata, sio matakwa binafsi wala misahafu, bali kwa kufuata misingi ya maadili asilia inayotajwa katika katiba ya nchi.

Mfano, amewahi kupewa ushauri ifuatao kuhusu "MISINGI YA MAADILI ASILIA," yaani "NATURAL LAW POLICY FRAMEWORK," anayopaswa kuifuata:

“Specifically, in every human person’s nature there are natural inclinations that are the origin of our moral choices and actions, as opposed to our immoral choices and actions, namely: (1) Natural inclination to the good as opposed to an aversion to the evil; (2) Natural inclination to preserve life as opposed to an aversion to intentionally causing death of an innocent person; (3) Natural inclination to preserve health as opposed to an aversion to sickness; (4) Natural inclination to copulation as opposed to an aversion to pedication; (5) Natural inclination to marriage as opposed to an aversion to celibacy; (6) Natural inclination to knowledge of truth as opposed to an aversion to ignorance; (7) Natural inclination to live in society as opposed to an aversion to solitude; (8) Natural inclination to self-integration as opposed to an aversion to self-disintegration; (9) Natural inclination to ownership as opposed to an aversion to material poverty; (10) Natural inclination to technology as opposed to an aversion to technological aversion; (11) Natural inclination to personal self-determination as opposed to an aversion to subjugation; (12) Natural inclination to order as opposed to an aversion to chaos; (13) Natural inclination to peace as opposed to an aversion to violence; (14) Natural inclination to coherence as opposed to an aversion to incoherence; (15) Natural inclination to culture; (16) Natural inclination to the common good as opposed to an aversion to the common evil; and (17) Natural inclination to knowledge of religious truth as opposed to an aversion to religious ignorance.”

Hata hivyo, Samia haonekani kusikiliza ushauri wowote wakati hii ni misingi ya madili asilia iliyotajawa kwenye Katiba ya nchi ambayo Samia aliapa kuilinda.

Yeye anaendelea na programu y sera haramu 17, nilizoziiita “NEW DECIDED MOPPERS POLICY FRAMEWORK,” kwa maana ya sera zifuatazo:

(1) Nepotic autocracy in state administration; (2) Emigration of Indigenous Africans; (3) War on the Natural Moral Law as opposed to Shariah Law; (4) Detentive abductions and tortures; (5) Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges; (6) Court capture and litigation dramas; (7) Inquiry commission dramas; (8) Deregistration of critical associations; (9) Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges; (10) Disinformation, media capture and mind capture; (11) Military politicisation, capture and intimidation; (12) Organised violence against republican principles; (13) Parliamentary capture and legislative dramas; (14) Police and paramilitary forces brutality; (15) Embezzlement of financial and natural resources; (16) Religious oppressions; and (17) Security forces outsourcing for domestic oppressions.

kuna mpasuko usioweza kusuluhishika kati ya fikra za Samia kama zinavyojieleza kupitia “NEW DECIDED MOPPERS policy framreork,” kwa upande mmoja, na fikra za umma wa Watanzania, kwa upande mwingine, kama zinavyojieleza kupitia ""NATURAL LAW POLICY FRAMEWORK".

Hivyo, napendekeza kwamba, ni sahihi kuhitimisha kwamba, Samia amepoteza uhalali wa kukaa ikulu, japo huenda rafiki yangu MALCOM LUMUMBA asipende wazo hili.

V. HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

Hivyo basi, kwa kuwa watu huunda serikali kwa ajili ya kuitumia kama nyenzo ya kulinda uhai wao na haki zinazoambatana na uhai;

Kwa kuwa watu wanayo haki ya kubadili serikali inayohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kusimika serikali mpya, ambayo, kwa maoni yao, itaweza kukuza na kuhami haki zao;

Kwa kuwa watu wanayo haki ya kufuta muundo wa kiserikali unaohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kubuni na kuweka muundo mpya wa serikali mpya, ambao kwa maoni yao utaweza kukuza na kuhami haki zao;

Na kwa kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya Samia na muundo wa serikali mbili vimethibitika kuhahatarisha haki za watu kwa utaratibu endelevu, tangu 2015;

Hivyo basi, natoa mapendekezo yafuatayo, kwa ajili ya utekelezaji kabla ya tarehe 01 Januari 2026:

  1. Mosi, Samia aitishe kikao cha Baraza la Mawaziri ili limpe taarifa sahihi kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Afya, Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Tamisemi.
  2. Pili, Samia aitishe kikao cha Baraza la Usalama la Taifa ili limpatie taarifa sahihi kuhusu matukio ya wiki ya uchaguzi.
  3. Tatu, Samia apitie ushahidi atakaopewa na hatimaye kukubali kwa hiari yake kwamba serikali yake ilifanya makosa makubwa, na hatimaye kuvunja serikali na Bunge ili kutengenza mazingira rafiki kwa mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
  4. Nne, Samia akubali kuunda serikali ya mpito itakayosimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
  5. Tano, Samia akubali kujiuzulu na kuipa nafasi serikali ya mpito kusimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa, kuundwa kwa katiba mpya na kusimamia uchaguzi mtakatifu chini ya Katiba Mpya.
  6. Na sita, kama Samia hakubaliani na mapendekezo haya, wakati ushahidi wote uliowasilishwa unaonyesha bayana kuwa ameshindwa kuendesha nchi kwa mujibu wa Katiba, basi, bila kuvunja Katiba ya nchi, JWTZ wasimamie mchaka wa mapinduzi ya kidemokrasia kama ilivyofanyika huko Zimbabwe mwaka 2017.
Nawasilisha.
Nyerere aliiongelea hatari ya vyama vingi katika muktadha wa uwepo wa vyama vya kikabila, hakuongelea hatari ya vyama vingi katika muktadha wa baadhi yetu kugeuka mawakala wa wageni kwa nia ya kuwasaidia hao hao maadui zetu.

JPM amefariki kwa mapenzi ya Mungu lakini ukimfuatilia sana Lissu unaweza kuona ni kwanini alitakiwa aage dunia tarehe 7 Septemba 2017, kwa akili na hulka zile zile za ujuaji mwingi ambao ndani yake unaficha nia chafu za kuidalalia Tanzania kwa mataifa ya kizungu.

Samia ni msimamizi mkuu wa dola ya JMT, ana haki kuwasikitikia wazazi ambao watoto wao walipoteza maisha kwa kupigwa risasi na askari wetu, vifo vingeweza kuwa vichache iwapo wazazi wale wangeweza kukaa majumbani na watoto wao. Watoto wasio na makosa wametolewa kafara katika vita pana kati ya serikali na maadui wake wa siri.

Amiri Jeshi mkuu yupo kikatiba kumbuka jeshi lina wajibu wa kuilinda katiba Polisi ndio wanaohangaika na masuala ya kisheria. Samia angekuwa hana uhalali wa kuongoza TZ mpaka muda huu asingekuwa Rais wa JMT.

Nyinyi ndio wale vijana mnaolitukana jeshi huko instagram bila ya kujua kwamba lina wajibu wa kula kiapo cha kumlinda Amiri Jeshi Mkuu.

Mna akili za kutaka kujenga hisia za chuki kati ya walinzi wa katiba na wananchi wanaopaswa kuitii katiba.
 
...kumbuka jeshi lina wajibu wa kuilinda katiba Polisi ndio wanaohangaika na masuala ya kisheria. Samia angekuwa hana uhalali wa kuongoza TZ mpaka muda huu asingekuwa Rais wa JMT. Nyinyi ndio wale vijana mnaolitukana jeshi huko instagram bila ya kujua kwamba lina wajibu wa kula kiapo cha kumlinda Amiri Jeshi Mkuu.

UFAFANUZI: JWTZ HAWAKUUA WAANDAMANAJI KATIKA WIKI YA UCHAGUZI NA UHALALI WA SAMIA UNAFAHAMIKA KWA WAKUU WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA ZAIDI KULIKO KUFAHAMIKA KWA RAIA

Nataka usome hoja yangu vizuri na usinilishe maneno. Tofauti na watu baki wanavyofikiria, mie najua fika kuwa mauaji yaliyofanyika katika wiki ya uchaguzi mkuu hayakufanywa na JWTZ.

Hawa watu, hasa katika ngazi zilizo chini ya wakuu wa komandi, walifanya kazi kubwa sana. Walikuwa tayari kuokoa maisha ya GenZ lakini walikwazwa.

Kwa sehemu kubwa, Wahusika wakuu wa mauaji yaliyofanyika katika wiki ya uchaguzi mkuu ni Jeshi la Polisi, na hasa kitengo nilichokiita Special Anti-Armed Robbery Unit (SARU).

Hawa waliongozwa na kaulimbiu kwamba "waandamanaji ni vibaka wenye silaha," na hivyo wenye kustahili kupata adhabu ya kifo cha papo hapo, kwa mujibu wa "shoot to kill order" waliyopewa.

Bila shaka Mkuu wa Operesheni za Kipolisi, CP Awadhi Hajj, anajua nani alitoa amri hiyo, maana ndiye anaisimamia SARU.

KUhusu uhalali wa Samia, kauli unayoitetea na ambayo naikosoa ni tamko kwamba, "Kama Samia angekuwa hana uhalali wa kuongoza TZ mpaka muda huu asingekuwa Rais wa JMT." Nina mawazo tofauti.

Mpaka sasa Samia ni Rais kwa sababu amesimikwa na jeshi. Ndio maana Samia alikula kiapo akiwa kwenye kambi ya jeshi, mbele ya mtutu wa bunduki, huku MC akiwa CDF.

Nje ya mtutu wa bunduki uhalali wa Samia ni mazungumzo baada ya habari kuu.
 
UFAFANUZI: JWTZ HAWAKUUA WAANDAMANAJI KATIKA WIKI YA UCHAGUZI NA UHALALI WA SAMIA UNAFAHAMIKA KWA WAKUU WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA ZAIDI KULIKO KUFAHAMIKA KWA RAIA

Nataka usome hoja yangu vizuri na usinilishe maneno. Tofauti na watu baki wanavyofikiria, mie najua fika kuwa mauaji yaliyofanyika katika wiki ya uchaguzi mkuu hayakufanywa na JWTZ.

Hawa watu, hasa katika ngazi zilizo chini ya wakuu wa komandi, walifanya kazi kubwa sana. Walikuwa tayari kuokoa maisha ya GenZ lakini walikwazwa.

Kwa sehemu kubwa, Wahusika wakuu wa mauaji yaliyofanyika katika wiki ya uchaguzi mkuu ni Jeshi la Polisi, na hasa kitengo nilichokiita Special Anti-Armed Robbery Unit (SARU).

Hawa waliongozwa na kaulimbiu kwamba "waandamanaji ni vibaka wenye silaha," na hivyo wenye kustahili kupata adhabu ya kifo cha papo hapo, kwa mujibu wa "shoot to kill order" waliyopewa. Bila shaka Mkuu wa Operesheni za Kipolisi, CP Awadhi Hajj, anajua nani alitoa amri hiyo, maana ndiye anaisimamia SARU.

KUhusu uhalali wa Samia, kauli unayoitetea na ambayo naikosoa ni tamko kwamba, "Kama Samia angekuwa hana uhalali wa kuongoza TZ mpaka muda huu asingekuwa Rais wa JMT." Nina mawazo tofauti.

Mpaka sasa Samia ni Rais kwa sababu amesimikwa na jeshi. Ndio maana Samia alikula kiapo akiwa kwenye kambi ya jeshi, mbele ya mtutu wa bunduki, huku MC akiwa CDF.

Nje ya mtutu wa bunduki uhalali wa Samia ni mazungumzo baada ya habari kuu.
Yale hayakuwa maandamano katika uhalisia wake yanaitwa maandamano na kina Larry Madowo wanaofanya kazi ya kuhabarisha mabwana zao wa CNN.

Hakuna maandamano ambayo vituo vya mafuta vinachomwa moto kwa mamia. Hakuna maandamano ambayo vijana walipanga kwenda kuchoma moto matenki ya mafuta kule TPA, unajua hasara kiasi gani ingetokana na uhayawani huo?.

Hakuna maandamano ambayo ATM zinavunjwa na watu wanachukua pesa, hakuna maandamano ambayo waandamanaji wanachoma vituo vya mwendokasi ambavyo jamaa zao wanaosoma shule wanavitumia kila siku kwendea mashuleni.

Ule ulikuwa uhuni ambao ni sehemu ya mapinduzi haramu yaliyopangwa na watu ambao hawakuwepo Tanzania, serikali ilipambana na uhaini, huwezi kupambana nao kwa kuwapelekea maua vijana ambao wanaichoma nchi kwa hasira ambazo zimepandikizwa vichwani mwao kwa miezi kadhaa.

Siku zote dola inapopambana na uhaini mambo mawili huwakuta wahaini hao, aidha wapigwe risasi wafe au wakamatwe washtakiwe.

Samia tulimpigia kura sisi vyama 17 nyinyi mawakala wa wazungu CHADEMA mnaeleweka kuwa na misimamo ya kupinga kila kitu.

Hamkutaka wakurugenzi wa halmashauri wasimamie uchaguzi mkuu, hawakuwepo wakurugenzi hao.

Kikao cha kwanza cha majadiliano kwa msajili hamkwenda mkaishia kuja na kauli mbiu ya 'no reform' mkadhani mnaikomoa dola!.
 
Gen Z wametolewa kafara kwa sababu ya uchanga wao kwenye masuala ya kisiasa, Anayewalipa na kuwasakizia wakaingia barabarani anasubiriwa na hukumu ya Mungu.

..hata Polisi waliofanya mauaji kiholela ni Gen Z.

..kwa hiyo usilaumu upande mmoja kwa kuwatumia vijana wetu vibaya.
 
Yale hayakuwa maandamano katika uhalisia wake yanaitwa maandamano na kina Larry Madowo wanaofanya kazi ya kuhabarisha mabwana zao wa CNN.

Hakuna maandamano ambayo vituo vya mafuta vinachomwa moto kwa mamia. Hakuna maandamano ambayo vijana walipanga kwenda kuchoma moto matenki ya mafuta kule TPA, unajua hasara kiasi gani ingetokana na uhayawani huo?.

Hakuna maandamano ambayo ATM zinavunjwa na watu wanachukua pesa, hakuna maandamano ambayo waandamanaji wanachoma vituo vya mwendokasi ambavyo jamaa zao wanaosoma shule wanavitumia kila siku kwendea mashuleni.

Ule ulikuwa uhuni ambao ni sehemu ya mapinduzi haramu yaliyopangwa na watu ambao hawakuwepo Tanzania, serikali ilipambana na uhaini, huwezi kupambana nao kwa kuwapelekea maua vijana ambao wanaichoma nchi kwa hasira ambazo zimepandikizwa vichwani mwao kwa miezi kadhaa.

Siku zote dola inapopambana na uhaini mambo mawili huwakuta wahaini hao, aidha wapigwe risasi wafe au wakamatwe washtakiwe.

Samia tulimpigia kura sisi vyama 17 nyinyi mawakala wa wazungu CHADEMA mnaeleweka kuwa na misimamo ya kupinga kila kitu.

Hamkutaka wakurugenzi wa halmashauri wasimamie uchaguzi mkuu, hawakuwepo wakurugenzi hao.

Kikao cha kwanza cha majadiliano kwa msajili hamkwenda mkaishia kuja na kauli mbiu ya 'no reform' mkadhani mnaikomoa dola!.

UMEANDIKA HIVI:

Yale hayakuwa maandamano [ya amani] katika uhalisia wake. Yanaitwa maandamano [ya amani] na kina Larry Madowo wanaofanya kazi ya kuhabarisha mabwana zao wa CNN.

Hakuna maandamano [ya amani] ambayo vituo vya mafuta vinachomwa moto kwa mamia. Hakuna maandamano [ya amani] ambayo vijana walipanga kwenda kuchoma moto matenki ya mafuta kule TPA. Hasara kubwa sawa ingetokana na uhayawani huo.

Hakuna maandamano [ya amani] ambayo ATM zinavunjwa na watu wanachukua pesa. Hakuna maandamano [ya amani] ambayo waandamanaji wanachoma vituo vya mwendokasi ambavyo jamaa zao wanaosoma shule wanavitumia kila siku kwendea mashuleni.

MAJIBU:

Maandamano yalianza yakiwa ya amani, lakini provocation ya mauaji ya polisi ikayabadilisha kuwa maandamano ya fuja za kujibu mapigo.

UMEANDIKA HIVI:

Ule ulikuwa uhuni [wa maandamano ya fujo] ambao ni sehemu ya mapinduzi haramu yaliyopangwa na watu ambao hawakuwepo Tanzania. Serikali ilipambana na uhaini.

Huwezi kupambana na uhaini kwa kuwapelekea maua vijana ambao wanaichoma nchi kwa hasira ambazo zimepandikizwa vichwani mwao kwa miezi kadhaa.

Siku zote dola inapopambana na uhaini mambo mawili huwakuta wahaini hao. Ama wanapigwa risasi wafe au wanakamatwa ili washtakiwe. [Serikali iliamua kuua baadhi na kushitaki waliobaki hai.]

NAJIBU HIVI:

Kuwapiga risasi watuhumiwa wa uhaini ili wafe badala ya luwakamata ili washtakiwe, ni kosa kisheria liitwalo extra-judicial killing. Adhabu yake ni kifo.

UMEANDIKA HIVI:

Samia tulimpigia kura sisi vyama 17 bila ushiriki wa chadema. Ninyi CHADEMA mawakala wa wazungu mnaeleweka kuwa na misimamo ya kupinga kila kitu.

Hamkutaka wakurugenzi wa halmashauri wasimamie uchaguzi mkuu. Hawakuwepo wakurugenzi hao, lakini bado mkapinga.

Kikao cha majadiliano ya kanuni kwa msajili hamkwenda, mkasusa kusaini na mkaishia kuja na kauli mbiu ya 'no reform no election.' Mlidhani mnaikomoa dola kumbe mnajikomoa wenyewe.

NAJIBU HIVI:

Haki ya chama cha siasa kushiriki uchaguzi ni haki ya kikatiba, ilinayotafsiriwa kisheria na kikanuni. Lakini, vifungu vya kanuni haviwezi kufuta vifungu vya sheria, na vifungu vya sheria haviwezi kufuta vifungu vya katiba.

Kwa hiyo INEC haina mamlaka ya kuzuia chama cha siasa kushiriki uchaguzi kama walivyofanya dhidi ya Chadema.

It was impunity, pure and simple.
 
Miaka 64 iliyopita, yaani mwaka 1961, kijana Mtanganyika aitwaye Julius Nyerere alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanganyika” kutoka kwa wakoloni wa Kizungu.
Nalichukulia bandiko hili kama literacy work hivyo nikikutana na factual errors, nitakuonyesha.
Miaka mitatu baadaye, kijana Mzanzibari aitwaye Abedi Karume, alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Zanzibar” kutoka kwenye ukoloni wa miaka ipatayo 200 chini ya Waarabu wa Omani, waliokuwa wameikalia Zanzibar tangu 1698.
Wa Oman walianza kuitawala Zanzibar mwaka 1734 wakati Sultan Seyyid Said, alipohamishia makao makuu ya sultanate yake toka Oman to Zanzibar.

Hivyo alivivamia visiwa vya Zanzibar Pemba, na eneo la maili 10 za pwani yote ya Africa Mashariki.

Sultan alitambuliwa rasmi na ule mkutano wa Berlin wa Scramble for Africa, ulioitishwa na mtawala wa Ujerumani, Von Bismarck mwaka 1884, hivyo Zanzibar was never colonized.

Ujerumani ilimilikishwa Tanganyika ikiitwa Germany East Africa. Mwaka 1890, iliingia mkataba wa Hellingoland na Zanzibar chini ya ulinzi wa Uingereza, kuziachia zile maili 10 za coastal strip

Mwaka 1918 baada ya Ujerumani kushindwa vita vya dunia, ilipokonywa makoloni yake yote na German East Africa kukabithiwa kwa Waingereza na kuuita Tanganyika

Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Desemba 1963, toka kwa Waingereza huku ikiwa monarch ya Sultan, na mwezi mmoja baada ya uhuru, ile January 12 mwaka 1964 ndipo yanafanyika yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Hatimaye, vijana Julius Nyerere na Abedi Karume walitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanzania” iliyopaswa kuendelea kuwa huru dhidi ya ukoloni mamboleo na utumwa mambosasa.

Nawasilisha.
Ile mwaka 1964 kulifanyika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania na sio uhuru wa Tanzania.

P
 
Nilidhani uko serious na andiko lako mpaka niliposoma point ifuatayo:

Bahati mbaya mfumo wa “Shariah Law” inaruhusu mauaji holela, kwa kuwapiga mawe watuhumiwa hadi wafe, hata bila kufuata mfumo wa kimahakama, inahalalisha utekaji na utesaji wa watuhumiwa kwa kuwachapa viboko hadi 100, na kadhalika. Kwa ufupi mfumo wa “Shariah Law” hautambui ukuu wa tunu ya uhai.

Utekaji, mauaji na utesaji wa raia unaoendelea nchini ni ushahidi kuwa sasa mfumo wa “Shariah Law” umerasimishwa kinyemelea nchini Tanzania.

Nikaconclude kuwa wewe ni mdini uliyejimask kama msomi. Umeonyesha ujinga wa kiwango cha juu au chuki kali dhidi ya waislamu.

Baada ya kusema hayo, mimi naamini Samia ni incompetent, hatoshi kwenye hiyo nafasi, kaingia kwenye hiyo nafasi kwa uchaguzi feki na wa kimagumashi na naamini analo la kujibu juu ya mauaji ya wananchi yaliyotokea Octobe 29 na siku kadhaa baadae.
🖕🖕
 
Yale hayakuwa maandamano katika uhalisia wake yanaitwa maandamano na kina Larry Madowo wanaofanya kazi ya kuhabarisha mabwana zao wa CNN.

Hakuna maandamano ambayo vituo vya mafuta vinachomwa moto kwa mamia. Hakuna maandamano ambayo vijana walipanga kwenda kuchoma moto matenki ya mafuta kule TPA, unajua hasara kiasi gani ingetokana na uhayawani huo?.

Hakuna maandamano ambayo ATM zinavunjwa na watu wanachukua pesa, hakuna maandamano ambayo waandamanaji wanachoma vituo vya mwendokasi ambavyo jamaa zao wanaosoma shule wanavitumia kila siku kwendea mashuleni.

Ule ulikuwa uhuni ambao ni sehemu ya mapinduzi haramu yaliyopangwa na watu ambao hawakuwepo Tanzania, serikali ilipambana na uhaini, huwezi kupambana nao kwa kuwapelekea maua vijana ambao wanaichoma nchi kwa hasira ambazo zimepandikizwa vichwani mwao kwa miezi kadhaa.

Siku zote dola inapopambana na uhaini mambo mawili huwakuta wahaini hao, aidha wapigwe risasi wafe au wakamatwe washtakiwe.

Samia tulimpigia kura sisi vyama 17 nyinyi mawakala wa wazungu CHADEMA mnaeleweka kuwa na misimamo ya kupinga kila kitu.

Hamkutaka wakurugenzi wa halmashauri wasimamie uchaguzi mkuu, hawakuwepo wakurugenzi hao.

Kikao cha kwanza cha majadiliano kwa msajili hamkwenda mkaishia kuja na kauli mbiu ya 'no reform' mkadhani mnaikomoa dola!.

..jaribu kutupia macho HALI NGUMU YA KIUCHUMI ya wananchi wetu.

..Je, haiwezekani kwamba wizi na uporaji tulioshuhudia ni matokeo ya umasikini, tamaa, na hali ngumu ya kiuchumi?

..kila panapotokea ajali tumeshuhudia wizi na uporaji mkubwa. Wakati mwingine hata katika mazingira ya hatari kwa mfano uporaji wa mafuta kunapotokea ajali za magari yanayosafirisha mafuta.

..hata katika maisha yetu ya kawaida wizi na uporaji upo. Kwa mfano wengi tunakuwa na wasiwasi wa kuibiwa au kuporwa ktk maeneo yenye foleni za magari.

..sasa kama ukweli wa maisha yetu ya kila siku ndio huo kwanini tunashangaa wizi na uporaji uliotokea siku ya maandamano?

..kwani tulitaraji wezi na vibaka wote waende wapi, na wafanye nini, siku ya maandamano makubwa? Tulitarajia watakaa majumbani kwao? Tulitarajia watabeba mabango?

..kwa hiyo hili la uporaji wakati wa maandamano tuliangalie ktk muktadha wa changamoto za kipata na kiuchumi wanazopitia wananchi wetu.
 
Nalichukulia bandiko hili kama literacy work hivyo nikikutana na factual errors, nitakuonyesha.

Wa Oman walianza kuitawala Zanzibar mwaka 1734 wakati Sultan Seyyid Said, alipohamishia makao makuu ya sultanate yake toka Oman to Zanzibar.

Hivyo alivivamia visiwa vya Zanzibar Pemba, na eneo la maili 10 za pwani yote ya Africa Mashariki.

Sultan alitambuliwa rasmi na ule mkutano wa Berlin wa Scramble for Africa, ulioitishwa na mtawala wa Ujerumani, Von Bismarck mwaka 1884, hivyo Zanzibar was never colonized.

Ujerumani ilimilikishwa Tanganyika ikiitwa Germany East Africa. Mwaka 1890, iliingia mkataba wa Hellingoland na Zanzibar chini ya ulinzi wa Uingereza, kuziachia zile maili 10 za coastal strip

Mwaka 1918 baada ya Ujerumani kushindwa vita vya dunia, ilipokonywa makoloni yake yote na German East Africa kukabithiwa kwa Waingereza na kuuita Tanganyika

Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Desemba 1963, toka kwa Waingereza huku ikiwa monarch ya Sultan, na mwezi mmoja baada ya uhuru, ile January 12 mwaka 1964 ndipo yanafanyika yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Ile mwaka 1964 kulifanyika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania na sio uhuru wa Tanzania.

P

TAKING STOCK OF ZANZIBAR HISTORY

The statement which you assert and which I deny is that, “Zanzibar was never colonized”.

So the disputed question is: “Was Zanzibar ever colonized, if yes, by who and when?”

My answer is in the affirmative as follows.

Zanzibar was colonized, first by the Portuguese for about 200 years, then falling under Omani colonial rule, and eventually becoming a British protectorate in 1890, a status that ended with independence in 1963, leading to the Zanzibar Revolution and union with Tanganyika to form modern Tanzania. Key Phases of Control are:

  • Portuguese Era (Late 15th Century-1698): Vasco da Gama's arrival marked the beginning of European influence, with Portugal controlling Zanzibar for nearly two centuries as part of its empire.
  • Omani colonial Rule (1698-1890): Omani Arabs took control, turning Zanzibar into a major trade hub for slaves, ivory, and spices, earning it the nickname "Spice Islands". Hence, your unfounded claim that, "Wa-Oman walianza kuitawala Zanzibar mwaka 1734 wakati Sultan Seyyid Said, alipohamishia makao makuu ya sultanate yake toka Oman to Zanzibar."
  • British colonial rule (1890-1963): Through the Heligoland-Zanzibar Treaty, Germany ceded its claims, and Britain established a protectorate, reducing the Sultan's power and curbing the slave trade.
  • Independence & Revolution (1963-1964): Zanzibar gained full independence as a Commonwealth member in 1963, but a revolution in January 1964 overthrew the monarchy, and the island soon united with Tanganyika to form Tanzania in April 1964.
 
..jaribu kutupia macho HALI NGUMU YA KIUCHUMI ya wananchi wetu.

..Je, haiwezekani kwamba wizi na uporaji tulioshuhudia ni matokeo ya umasikini, tamaa, na hali ngumu ya kiuchumi?

..kila panapotokea ajali tumeshuhudia wizi na uporaji mkubwa. Wakati mwingine hata katika mazingira ya hatari kwa mfano uporaji wa mafuta kunapotokea ajali za magari yanayosafirisha mafuta.

..hata katika maisha yetu ya kawaida wizi na uporaji upo. Kwa mfano wengi tunakuwa na wasiwasi wa kuibiwa au kuporwa ktk maeneo yenye foleni za magari.

..sasa kama ukweli wa maisha yetu ya kila siku ndio huo kwanini tunashangaa wizi na uporaji uliotokea siku ya maandamano?

..kwani tulitaraji wezi na vibaka wote waende wapi, na wafanye nini, siku ya maandamano makubwa? Tulitarajia watakaa majumbani kwao? Tulitarajia watabeba mabango?

..kwa hiyo hili la uporaji wakati wa maandamano tuliangalie ktk muktadha wa changamoto za kipata na kiuchumi wanazopitia wananchi wetu.
Hayakuwa maandamano yale mkuu, licha ya hali kuwa ngumu. Walitaka kutengeneza mazingira ya nchi kutokutawalika, hakuna dola inayoweza kukubaliana na ujinga ule.

Kwamba wao wanapoiba inakuwa ni kawaida tu lakini wanapopigwa risasi ili kuzuia ushenzi usiendelee basi Samia ni muuaji!!.

Hao wanaomuita muuaji wangeichukulia vipi dola ya Tanzania ambayo ingekuwa imeshindwa kujitetea dhidi ya uharamia?.

Wanaleta political blackmailing ambayo ni mbinu inayotumiwa na mataifa makubwa katika kutengeneza mazingira ya kuzibana nchi ndogo za afrika.
 
Hizi ni pumba tu tunezoea kuzionantoka kwa anayejiita Doctor Mama Amon.

Pelekea nguruwe
Chawa najua ujumbe huu umekupatia maumivi makali mno kuliko yale uliyoyapata ulipopigwa mshale katikati ya makalio na mwenye shamba ulilokuwa ukiiba mkungu wa ndizi
 
UMEANDIKA HIVI:

Yale hayakuwa maandamano [ya amani] katika uhalisia wake. Yanaitwa maandamano [ya amani] na kina Larry Madowo wanaofanya kazi ya kuhabarisha mabwana zao wa CNN.

Hakuna maandamano [ya amani] ambayo vituo vya mafuta vinachomwa moto kwa mamia. Hakuna maandamano [ya amani] ambayo vijana walipanga kwenda kuchoma moto matenki ya mafuta kule TPA. Hasara kubwa sawa ingetokana na uhayawani huo.

Hakuna maandamano [ya amani] ambayo ATM zinavunjwa na watu wanachukua pesa. Hakuna maandamano [ya amani] ambayo waandamanaji wanachoma vituo vya mwendokasi ambavyo jamaa zao wanaosoma shule wanavitumia kila siku kwendea mashuleni.

MAJIBU:

Maandamano yalianza yakiwa ya amani, lakini provocation ya mauaji ya polisi ikayabadilisha kuwa maandamano ya fuja za kujibu mapigo.

UMEANDIKA HIVI:

Ule ulikuwa uhuni [wa maandamano ya fujo] ambao ni sehemu ya mapinduzi haramu yaliyopangwa na watu ambao hawakuwepo Tanzania. Serikali ilipambana na uhaini.

Huwezi kupambana na uhaini kwa kuwapelekea maua vijana ambao wanaichoma nchi kwa hasira ambazo zimepandikizwa vichwani mwao kwa miezi kadhaa.

Siku zote dola inapopambana na uhaini mambo mawili huwakuta wahaini hao. Ama wanapigwa risasi wafe au wanakamatwa ili washtakiwe. [Serikali iliamua kuua baadhi na kushitaki waliobaki hai.]

NAJIBU HIVI:

Kuwapiga risasi watuhumiwa wa uhaini ili wafe badala ya luwakamata ili washtakiwe, ni kosa kisheria liitwalo extra-judicial killing. Adhabu yake ni kifo.

UMEANDIKA HIVI:

Samia tulimpigia kura sisi vyama 17 bila ushiriki wa chadema. Ninyi CHADEMA mawakala wa wazungu mnaeleweka kuwa na misimamo ya kupinga kila kitu.

Hamkutaka wakurugenzi wa halmashauri wasimamie uchaguzi mkuu. Hawakuwepo wakurugenzi hao, lakini bado mkapinga.

Kikao cha majadiliano ya kanuni kwa msajili hamkwenda, mkasusa kusaini na mkaishia kuja na kauli mbiu ya 'no reform no election.' Mlidhani mnaikomoa dola kumbe mnajikomoa wenyewe.

NAJIBU HIVI:

Haki ya chama cha siasa kushiriki uchaguzi ni haki ya kikatiba, ilinayotafsiriwa kisheria na kikanuni. Lakini, vifungu vya kanuni haviwezi kufuta vifungu vya sheria, na vifungu vya sheria haviwezi kufuta vifungu vya katiba.

Kwa hiyo INEC haina mamlaka ya kuzuia chama cha siasa kushiriki uchaguzi kama walivyofanya dhidi ya Chadema.

It was impunity, pure and simple.
INEC waliweka masharti kwa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa 2025, kwanini vyama 17 vikubaliane na masharti hayo halafu CHADEMA peke yao walete dharau?. Tangia mapema mlionyesha nia ya kuleta vurugu yale matamko ya Heche kwamba uchaguzi hautafanyika ulikuwa ni upuuzi wa kiwango cha juu sana, mamlaka zikawa zinamuangalia zione atafanya nini.

Kuna polisi waliopigwa risasi Magomeni wakafa wengine maeneo ya Tegeta pia waliuliwa, hawa wanaongelewa vipi na hizi sheria kwa mujibu wa maandiko yako?.

Katika mazingira ya machafuko nani anayefuatilia kwamba sheria ipi na ipi imetekelezwa?. Vita haina macho. Kumbuka kuwa Lissu alihubiri chuki aliposema atakinukisha, aliumba maovu kupitia mdomo wake.
 
Hayakuwa maandamano yale mkuu, licha ya hali kuwa ngumu. Walitaka kutengeneza mazingira ya nchi kutokutawalika, hakuna dola inayoweza kukubaliana na ujinga ule.

Kwamba wao wanapoiba inakuwa ni kawaida tu lakini wanapopigwa risasi ili kuzuia ushenzi usiendelee basi Samia ni muuaji!!.

Hao wanaomuita muuaji wangeichukulia vipi dola ya Tanzania ambayo ingekuwa imeshindwa kujitetea dhidi ya uharamia?.

Wanaleta political blackmailing ambayo ni mbinu inayotumiwa na mataifa makubwa katika kutengeneza mazingira ya kuzibana nchi ndogo za afrika.

..tujiangalie na sisi tumefikaje hapa.

..Hata kama mabeberu wana nia mbaya na sisi hawawezi kutuingilia bila kutumia nyufa zilizoko ktk jamii yetu.

..kwa msingi huo tunatakiwa kuwa macho na kila wakati kuziba nyufa ambazo mabeberu wanaweza kuzitumia kutusambaratisha.

..MUNGU ndio kaishatupa hizo rasilimali. Na mabeberu hawatakoma kuzitamani. Kwa hiyo ni juu yetu sisi kuyaelewa mazingira tunayoishi na namna ya kuyaendea.

NB:

..vibaka na waporaji wako siku zote. Siku ya maandamano FURSA kubwa ilijitokeza na wakaitumia.
 
Kwa bahati mbaya sana wengi wao wakapigwa risasi wakafa. Michakato ya kuandika katiba mpya inaendelea muda huu.

Japo kwangu mimi ni karatasi tu ambalo halitaweza kutujalia ubunifu wa kufaidika vilivyo na wingi wa rasilimali zilizopo.
 
Maandamano yalianza yakiwa ya amani, lakini provocation ya mauaji ya polisi ikayabadilisha kuwa maandamano ya fuja za kujibu mapigo.
Hapa umetupiga Mimi nakaa kimara niliona moshi Kwanza kabla ya risasi vijana walianza vizuri na ni kweli muda huo hata polisi walikuwa wanaangalia Tu pamoja na jeshi. Tatizo sijui kikundi gani (au sijui ndo hao waliolipwa? ) walikotokea haieleweki wakaanza kuchoma .....yaliyotokea wote tumeshuhudia how far dola inaweza kufika pale utapohatarisha usalama wa nchi.
 
Dr. Richard Mbunda lecturer UDSM
  • GenZ na the dead economy
  • uchumi uliokufa dead economy kutokana na viongozi wa kizazi kilichopita kukosa visheni kwa sababu ya umimi na ulafi
  • N.k
    1766934579067.jpeg

Dead economy : uchumi uliokufa dead economy kutokana na viongozi wa kizazi kilichopo na kilichopita kukosa visheni kwa sababu ya umimi na ulafi hadi kukosa uhalali wa kisiasa kuongoza nchi sasa GenZ inataka kuondokana na kaliba ya watawala hao. Sababu za kufeli ni pamoja na hizi :

View: https://m.youtube.com/watch?v=smmeOQ48q78

Articulated economy Tools and machinery specifically for industrial consumers i.e producing things for industries and factories

Disarticulated economy produce what you dont consume and use what you dont produce leading mass unemployment to the youths who are majority in a country's population
 
Hapa umetupiga Mimi nakaa kimara niliona moshi Kwanza kabla ya risasi vijana walianza vizuri na ni kweli muda huo hata polisi walikuwa wanaangalia Tu pamoja na jeshi. Tatizo sijui kikundi gani (au sijui ndo hao waliolipwa? ) walikotokea haieleweki wakaanza kuchoma .....yaliyotokea wote tumeshuhudia how far dola inaweza kufika pale utapohatarisha usalama wa nchi.
Afadhali umemuelezea kilichotokea kuliko yeye anayekuja na nadharia za vitabuni.
 
Kwa bahati mbaya sana wengi wao wakapigwa risasi wakafa. Michakato ya kuandika katiba mpya inaendelea muda huu.

Japo kwangu mimi ni karatasi tu ambalo halitaweza kutujalia ubunifu wa kufaidika vilivyo na wingi wa rasilimali zilizopo.

..Raisi angesimamia kwa uaminifu bila hila zile 4R tungekuwa tumemaliza 97% ya sababu za maandamano ya Oct 29.

..pia asingenasa katika aibu ya kuwa kiongozi mwenye rekodi ya kuuwa Watanzania wengi tangu tupate uhuru.
 
Back
Top Bottom