Nimesoma huu uzi leo. Nilikuwa sijawahi kuuona kwasababu 2025 akaunti yangu ya JF ilikuwa imejaa madodoso (Notifications/Memo)mengi mno. Sasa naomba niseme yafuatayo tu:
MOSI, unavyoandika ushauri wowote ule ni lazima ufahamu kwamba CCM ni chama kikubwa, kiovu na kina watu wajinga na kina watu werevu sana wa mambo. Hivyo mkakati wowote ule au madai yoyote yale utayoyaleta dhidi yao yatajibiwa ipasavyo, na lengo kubwa litakuwa ni kutaka kufilisi heshima ya mawazo yako (To Discredit the depth of your arguments). Nimesoma uzi wako kwa haraka sana, na kuwaza kwamba endapo mtu mwingine akisoma kwa nje tu (Literal Reading) bila kufahamu ulichokuwa unakilenga (The Spirit behind the words) anaweza akaghafirika na kuishia kukuona wewe ni mdini na mzandiki. Binafsi nimejaribu kukuelewa kwenye hayo uliyoyasema na ambayo nayazungumzia kama ifuatavyo kwenye aya inayokuja:
PILI, Elevation of Islamic Law (Mohammedan Law) Over Constitutional and Natural Law: Binafsi nimeelewa vizuri kabisa ulichokuwa unakilenga hapa. Kwamba Islamic Convictions have influenced the President's decision-making processes. Hili linawezekana kabisa, japo hoja yako isingekuwa wazi (Vague and Open-Ended) kama ungetoa mifano dhahiri. Ukikutana na CCM werevu, aina ya Andrew Chenge, Palamagamba Kabudi, Harisson Mwakyembe na Anna Tibaijuka, wataijibu hii hoja kwa kutumia Article 12(1) (c) (ii) of The Judicature and Application of Laws Act (JALA) CAP 358 R.E 2023, kinachosema hivi :
"Customary law shall be applicable to, and courts shall exercise jurisdiction in accordance therewith in, matters of a civil nature......In any other case in which, by reason of the connection of any relevant issue with any customary right or obligation, it is appropriate that the defendant be treated as a member of the community in which such right or obligation obtains and it is fitting and just that the matter be dealt with in accordance with customary law instead of the law that would otherwise be applicable,......Provided that......this subsection shall not preclude any court from applying the rules of Islamic law in matters of marriage, divorce, guardianship, inheritance, wakf and similar matters in relation to members of a community which follows that law"
Hivyo basi, utaambiwa Sharia Law (Mohammedan Law) ni sehemu muhimu ya sheria za Tanzania ilmaradi tu isipingane na katiba au maadila (Mohammedan Law is applicable in Tanzania, provided that it is not repugnant to morality). Lakini pia, inafanya kazi pale tu ambapo waislamu husika hutaka itumike kwenye mambo binafsi, siyo jinai.
Madai haya uliyoyatoa hapa ni mazito na hayajatolewa kwa Samia peke yake, bali hata kipindi cha Mzee Nyerere, mwaka 1963 ambao iliundwa kamati maalumu kuchunguza. Waislamu walilalamika kwamba Baraza ni la Kikatoliki, Mzee Nyerere kukata mzizi wa fitna akaunda kamati kuchunguza, ambapo baadaye ikaja kufahamika kwamba Wakatoliki ndani ya Baraza ni wachache ukilinganisha na dini nyingine. Hivyo hoja ya Waislamu ikapoteza mashiko.
Hoja dhidi ya MFUMO KRISTO ilipata nguvu dhidi ya Mzee Nyerere na WAKATOLIKI miaka ya 1990-2015 baada ya uthibitisho kutolewa. Miaka ya 90's kipindi Prof Malima alipokuwa Waziri wa Elimu, alianzisha utaratibu wa kutumia namba kwenye mitihani ya taifa. Ghafla ufaulu wa waislamu ukapanda. Lile jambo lilizua taharuki kubwa mno ambayo WAKATOLIKI hawakuweza kujitetea nayo. Hapa tunasema "Caught Red Handed". Hili jambo lilikuwa baya mno, watu walikaa na kinyongo dhidi ya Prof Malima hadi anakufa.
Upande mwingine ni lile lililotokea kipindi Prof Joyce Ndalichako ni Waziri wa Elimu. Waislamu walilalamika kwamba wanafelishwa serikali ikasema haiwafelishi. Kina Jakaya Kikwete wakaamuru mitihani isahiishwe upya kwenye baadhi ya masomo ya kiislamu, na ghafla mtoto anatoka kwenye kupata "D" hadi "B". Hapo unajiteteaje labda ??? "Caught Red Handed"
Mfano mwingine ni huu wa mwaka 2010: Jakaya Kikwete alishindwa uchaguzi na Dr Wilbroad Slaa, na ushahidi ukawa wazi kwamba CCM inakufa. Ikajengwa hoja ya UDINI, kwamba WAKATOLIKI ndiyo wameratibu haya yote. NEC ikahamia msikitini, na Prof Lipumba akaamua kumpa kura zake Jakaya Kikwete kwasababu Masheikh walitaka iwe hivyo. Hili hadi Prof Lipumba alilisema wazi.
Mfano wa mwisho: Kinachoendelea sasa hivi kisheria tunasema ni UDINI unaofadhiliwa na serikali (Government is complicit to Religious Extremism). Anachokifanya huyo muhuni Mwaipopo ni jambo la hatari mno ambalo litakuja kuleta matatizo huko mbele. Tulitegemea mpaka sasa serikali iamke imkanye Mwaipopo, BAKWATA waamke wamkee na Samia mwenyewe aamke na kusema wazi kwamba haungi mkono maneno ya chuki na kigaidi ya muhumi anayeitwa Mwaipopo anayetanabaisha kuongoza kikosi cha mgambo kinyume cha sheria.
Hoja yako naikubali na naelewa umeoiongelea kwa upande gani. Lakini bila mifano hai, yenye uzito, huwezi kukwepa watu kusema wewe ni mdini.
======================================================================================
TATU, on the displacement of indigenous people: Hili nalo inabidi uwe nalo makini mno. Kisheria watu wa asili "Indigenous People" ni watu ambao wamekuwepo kwenye hilo eneo kiasilia kwa miaka mingi kuliko jamii nyingine yoyote. Kwamba hii jamii ina utamaduni wake yenyewe ambao bila huo jamii hiyo itapotea kabisa. Lakini pia, tamaduni hizo huunganishwa na ardhi ya eneo hilo, ambapo wakiondolewa kwenye hiyo ardhi basi watafutika duniani.
Hii hoja imeanza kutumika na wanaharakati wa haki za binadamu hasahasa kwenye maeneo kama Marekani "Red Indians/Polynesian People", Australia "Aboriginals", New-Zealand "Maori" kuelezea kwamba watu hawa wamekuwepo kwenye maeneo yao na wana haki kuliko wazungu (Caucasian Settlers) waliovamia.
Hii hoja kwenye maeneo kama Tanzania INAWEZA kukosa mashiko kwasababu zifuatazo. Kwanza kabisa, sera ya Tanzania ni kwamba hakuna watu asilia "Indigenous People" nchini kwetu. Watanzania wote ni watu asilia kwasababa wote tumekuwepo hapa kwa miaka maelfu. Hii ndiyo ilikuwa sera ya Tanzania tangia kipindi cha TANU. Mwaka 1961, Mzee Nyerere aliwashambulia kina John Mwakangale kuhusu suala la Wahindi/Waarabu waliozaliwa Tanganyika, kwasababu wengi walisema wao siyo wazawa na watakuja kutuuza huko mbeleni. Mzee Nyerere akatishia kuacha madaraka. Hivyo hiyo ndiyo imekuwa sera ya Tanzania, hadi kipindi anawahamisha watu kimabavu ili kujenge vijiji vya ujamaa.
Mwaka 2019, kwenye UNITED NATIONS- Human Rights Council-Universal Periodic Review (UPR), serikali ya Tanzania ilirudia kusisitiza msimamo wake kwamba nchini kwetu hakuna kabisa, Indigenous People kwasababu nchi yetu siyo nchi ambayo imetokana koloni la walowezi/nchi ya walowezi (Settler Economy) kama Australia, Marekani, New-Zealand, Israel, Canada, Hawaii n.k ambako wageni walivamia na kunyang'anya ardhi za wazawa kimabavu.
Hoja hapa utaambiwa, wamassai wanaondolewa kisheria na anayewaondoa ni Raisi wao ili kupisha wawekezaji. Hapa inahitaji akili ya ziada kuweza kupangua hoja ya namna hii ambayo iko hadi kwenye kumbukumbu mbalimbali za UN (Travaux Preparetoires). Kuna nyenzo nyingi za kuzungumzia kufukuzwa kwa wamassai kwenye maeneo yao, lakini siyo hii ya INDIGENOUS PEOPLE. Sheria za kimataifa, neno Indigenous People lina maana zaidi ya sisi tunavyoweza kulielewa.
Hivyo basi unapojenga hoja kama hizi, hakikisha unazifunga kabisa na kufuri la chuma na kuzijengea wigo na maboma, ili wahuni wa CCM wale wenye werevu mkubwa washindwe kuzipangua kirahisi. Unatakiwa ufanye kama anavyofanya Mheshimiwa TUNDU LISSU, JOSEPH WARIOBA na JENERALI ULIMWENGU, ambao huwagusa CCM panapouma kwa kuwapa mifano hai kabisa kiasi cha kuwabana mbavu na kusababisha wapige jalamba.
====================================================================================
NNE, politicization of the military: Hili kweli lipo hapa nchini kwetu na naelewa wewe unazungumza kutokea upande gani. Binafsi nafahamu kinachoendelea ndiyo maana imekuwa rahisi kukuelewa. Japo ni rahisi mno kupindisha maneno yako. CCM waerevu, ambao wanafahamu fika historia ya nchi, wanaweza kusema mbona siasa iko jeshini tangu kipindi cha Mzee Nyerere. Tena wanaweza kwenda mbali na kusema kwamba siku hizi imepungua, maana zamani jeshi lilikuwa na nafasi za KAMISA (Commissars) ambazo zimefutwa. Wanajeshi/Polisi/Maafisa Usalama walikuwa wanaingia kwenye NEC-CCM na vikao vyake. Hapa utawajibuje ??? (It's very tricky)
Kuhusu masuala ya tenda kutolewa na Angela Kizigha, wahuni wa CCM watakujibu, mbona hadi watu kutoka familia ya Mzee Nyerere kama Jack Gotham walikuwa wanapewa tenda za usalama nchini. AU mbona kina Manji walikuwa wanapewa tenda za kuuza uniform kipindi cha Jakaya. AU mbona Mzee Nyerere na Mwinyi waliwatumia kina Sabodo, Mullah, Tako, na waarabu/wahindi wengine kufanya tenda za kijeshi kipindi nchi iko kwenye vita vya Kagera na mdororo wa kiuchumi. Kwanini unamsema Angela Kizigha au Saidi Lughumi peke yao ???
Mambo kama haya unaweza ukakutana nayo, siku umeingia kwenye vikao vya ndani na MIZEE YA COLD-WAR, na itakutishia na ukaishia kuonekana mjinga. Inahitaji tafakuri za kina kuweza kupambana na CCM. Mle ndani kuna watu wana uelewa mzuri sana tu, sema ndiyo wameamua kuharibu nchi kwa maksudi kwasababu wanaamini wananufaika na mfumo uliopo.
=======================================================================================
Kuna mtaalamu alitoka Harvard University na kwenda kufanya kazi IKULU YA KIKWETE. Alikuwa na mawazo mazito mno ya kuleta mabadiliko. Bahati mbaya hakufahamu kwamba mle ndani ni UKOO WA SHETANI, watu wamo mle ndani kwa mtandao maalumu. Basi kila akileta wazo jipya wanamwambia mbona hilo lipo lishaandikwa na fulani, basi anatumwa karani kuleta faili na mwishowe inagundulika kweli kile kitu siyo kipya, tayari kina Prof/Dr fulani washakiandika.
Lengo lilikuwa kumtumia ujumbe kwamba wewe ni wa kawaida na huwezi kutufundisha sisi jambo jipya. Kiufupi hauna maajabu. CCM ndiyo iko hivyo. Unapoamua kupambana nayo kwa hoja, hakikisha kwamba umezifungia kufuri la chuma na kuziweka wigo mpana.
========================================================================================
Nimesoma hoja zako na nafahamu unaandika kutokea upande upi, kwasababu kweli hiki ndicho kinachoendelea hapa nchini. Lakini siyo wote watakuwa na ufahamu ambao sisi wengine tunao, na hoja zako zikaishia kutafasiriwa ndivyo-sivyo na mamluki au waumini wa dini husika.
NDIYO MAANA HUWA NASEMA KUNA NJIA MOJA TU YA KUSHUGHULIKA NA CCM. NAYO SIYO YA KIMJADALA, ila huwa hamtaki mnaishia kusema mimi MNAZI (A Radical Extremist)