Mufti anapata faida gani kusema uongo kuhusiana na mwandamo wa mwezi?

Mufti anapata faida gani kusema uongo kuhusiana na mwandamo wa mwezi?

BAKWATA ina back up ya serikali. Yeyote atakaethubutu kwenda kinyume atashughulikiwa na serikali. Hili hasa ndilo linalompa kiburi huyo mzee.

Rejea misukosuko ya Sheikh Ponda.

Uongozi wa BAKWATA wenyewe umejawa uchafu wa rushwa, dhulma na umalaya tele. Mfano Katibu Mkuu wake tu ana kazi ya kuzalisha mahawara na kuwapangia majumbo kwa jeuri ya pesa ya Baraza.

Sasa watu kama hao unadhani watapata wapi moral grounds za kusimamia maadilii ama ukweli.
Waislam wakiamua wanawaza wakawa na chombo cha kuwaanganisha lakini siyo hii BAKWATA
 
Hivi mnataka aende kinyume na mamlaka alafu ule mshahara anaolipwa na Serikali aupate wapi

Vipi na ule ulinzi pamoja na gari zuri analotembelea, mafuta mtampa nyie 😎

Madaraka matamu eti
 
wataisajilia wapi? Labda wakaisajili maka kuliko na chimbuko la uislam kama ilivyo vatican kwa waislam, huwezi kughairisha kilichnpangwa vatican. Ndio mjue dini utashi tu wa mtu kuamua aamini na kuabudu vipi mungu wake
Binafsi naona waislam wengi karibia wote wanakula Eid
Hawana habari na maujinga ya BAKWATA.
Ina maana waislam wameipuuza BAKWATA
Kwaiyo BAKWATA haipo Kwa ajili ya umma wa waislam
 
Hivi mnataka aende kinyume na mamlaka alafu ule mshahara anaolipwa na Serikali aupate wapi

Vipi na ule ulinzi pamoja na gari zuri analotembelea, mafuta mtampa nyie 😎

Madaraka matamu eti
Sasa aseme wazi kuwa hayupo Kwa maslahi ya uislam
 
Waislam wakiamua wanawaza wakawa na chombo cha kuwaanganisha lakini siyo hii BAKWATA
hicho chombo kitasajiliwa wapi kama BAKWATA ipo? Kuna chombo cha kina sheikh Ponda kinaitwa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, sidhani chombo hicho kama kina usajili au serikali imeamua tu kukiacha kifanye shughuli zake bila kukiingilia na kupata uhalali wake. Hicho chombo kina bifu na BAKWATA, hujioma wao ndio waislam wa ukweli na wengine ni magumashi tu
 
Dini zenu ni utapeli

Mtu ana ghairisha sikukuu ya allah , halafu Allah nayeye yupo kimya tu ana mtazama


Halafu sio mara Moja ! Hii inafikirisha sana Kwa mtu mwenye Akili timamu kisawa sawa
Kwa hiyo ulitaka Allah adondoke kutoka mbinguni ili aje kumtisha Mufti?kama amefanya makosa ataadhibiwa siku ya kiama.
Na kitu kingine wenye elimu zao hawamfuatishi yeye wanasheherekea leo.
Kitu kingine yule Mufti ameajiriwa tu na serikali ya CCM haimaanishi kwamba yeye ndio kama nabii au mtukufu kwenye dini ya kiislamu ingekuwa tuko Iran hapo sawa sauti ya Mufti ina uzito.
 
hicho chombo kitasajiliwa wapi kama BAKWATA ipo? Kuna chombo cha kina sheikh Ponda kinaitwa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, sidhani chombo hicho kama kina usajili au serikali imeamua tu kukiacha kifanye shughuli zake bila kukiingilia na kupata uhalali wake. Hicho chombo kina bifu na BAKWATA, hujioma wao ndio waislam wa ukweli na wengine ni magumashi tu
Sasa nimekuelewa sana mkuu
Nadhani waislam wapo kama yatima
BAKWATA ni kama imewauza, inatumika
Nilishangaa walivotoka kutetea mauaji ya oktoba 29 na kuwapinga TEC
 
Binafsi naona waislam wengi karibia wote wanakula Eid
Hawana habari na maujinga ya BAKWATA.
Ina maana waislam wameipuuza BAKWATA
Kwaiyo BAKWATA haipo Kwa ajili ya umma wa waislam
hawa wanaokula iddi leo ni wachache na serikali haitambui kama leo ni iddi. Wengi watakula iddi kesho na serikali inatambua. Salamu za iddi zitatolewa kesho, sio leo
 
wachambuzi watuletee listi ya nchi zinazosherehekea leo na kesho

na sababu ya hiyo tofauti, alafu waumini wataamua nani yupo sahihi au wote wapo sahihi
Eid ni Leo mkuu
Quran inasema ' ikifinga siku ya 30 katika mfungo hata msipoona mwezi basi laZima iwe Eid '
Sasa siku 30 zilitimia Jana kwaiyo automatically Leo ni Eid
 
Kutoka hapo sio rahisi, wameshagawanywa (kuna watu wa mfumo mule wamejazwa)

Infact sio rahisi kupambana na system, angalia anachopitia Lissu na ukumbuke kilichowakuta masheikh wa uamsho
Sahihi nadhani waislam waungane na Chadema tupate katiba mpya, tufanye uchaguzi huru na haki tuitoe CCM madarakani,
Waislam nao wapate taasisi Yao ya kuwawakilisha
 
Back
Top Bottom