Uchaguzi 2020 Mufti Mkuu wa Waislamu Sheikh Zuberi leo Korogwe mbele ya Rais Magufuli

Uchaguzi 2020 Mufti Mkuu wa Waislamu Sheikh Zuberi leo Korogwe mbele ya Rais Magufuli

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Mufti Mkuu leo amepewa heshima ya kufungua kwa Dua mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa CCM na kabla ya kuanza dua amesema ana mambo mawili;

1. Kukanusha kile kinachodaiwa kuwa Waumini wa Dini ya Kiislam wana udini. ( hili linahitaji mjadala wake)

2. Amemuomba Dkt.Magufuli ajenge barabara ya kwao kwani imezidi kuwa mbaya na yenye vumbi.

Sasa najenga hoja yangu maajabu ya Mufti ni yapi?

Kama kweli huyu Mufti ni sheikh kweli kwa fursa aliyoipata leo kama mufti wa waislamu, leo ndio ilikuwa siku ya masheikh wa Uamsho kuachiwa huru.

Ombi hili angelitoa pale hadharani Mufti angesikilizwa na Rais, lakini kwakuwa Bakwata si chombo cha kutetea waislamu Mufti ametoa ombi la kujengewa barabara ya kwenda kijijini kwao.

Huyu ndio kiongozi mkuu wa Waislamu, huu ni msiba mzito.
 
Wewe ni Mufti wa Tanzania lakini pia hapo hapo Wewe ni Kiongozi Mkuu wa Kiimani nchini Tanzania bila kujali hata Sisi akina Gentamycine ambaye ni Mkristo tena wa 'Dhehebu' la Katoliki kabisa. Nakuheshimu Wewe ( japo ni Muislamu ) kama vile ninavyomuamini Kadinali wangu wa Ukatoliki nchini. Na nimesikitika pia kuona Watu wako wa Karibu 'hawakukushauri' katika hili.

Kitendo chako Mufti cha kupewa nafasi ya Kuzungumza mbele ya Mkuu wa nchi huko Tanga kisha 'Ukakemea' Kauli za 'Udini' zilizooneshwa Juzi na Jana na Kiongozi Mmoja wa Kiislamu Sheikh Ponda kisha hapo hapo na Wewe ukaanza Kuomba Msaada wa Ujenzi wa Barabara huko Mkoani Tanga huku ukiwananga wasiompenda Mgombea Urais wa CCM na Kumsifia ni Kosa Kubwa.

Gentamycine sikatai Wewe ( Nyie ) Viongozi Wakuu tena wa Kitaifa wa hizi 'Dini' Kuu mbili hapa Tanzania za Uislamu na Ukristo kuwa na 'Itikadi' zenu za 'Kisiasa' ila kuziweka hadharani sidhani kama ni Jambo jema kwani linaweza 'Kuwagawa' Watu wenu na hata kuanzisha 'Mitafaruku' mingine ya Kiimani ( Kidini ) nchini. Acheni kupenda 'Kuwalamba' Miguu 'Wanasiasa' Mungu hakuwatumeni muwe hivyo.

Nimesikitika sana kwa ulichokifanya japo Mimi ni mwana CCM na ninamkubali sana Mgombea wangu Ndugu Dkt. John Pombe Magufuli ila kuonyesha Kwako wazi wazi kuwa 'Unamkubali' hadi Kumpigia 'Chapuo' vile sikubaliani nacho na kama wana CCM Wenzangu hapa JamiiForums 'mtanichukia' Gentamycine kwa hili naamini Mwenyezi Mungu juu Mbinguni atanipenda zaidi.

Kila Siku nyie Viongozi Wakuu wa Kidini nchini Tanzania huwa 'mnatukanya' Watanzania kuingiza 'Udini' katika 'Siasa' ila cha 'Kushangaza;' nyie Viongozi Wakuu wa Kidini ndiyo mnakuwa wa Kwanza 'Kuvuruga' huu ( huo ) utaratibu na Kutuonyesha ( Kututhibitishia ) kuwa si tu mna 'Unafiki' uliotukuka bali pia hamlitakii 'mema' kabisa Taifa hili na Ustawi wake wa Amani yake.

Ili Mufti Mkuu wa Tanzania nikuone na nikuamini kuwa Wewe si Mufti Mkuu wa Tanzania na Chama changu Cha Mapinduzi ( CCM ) nakuomba Kesho nikuone pia katika Mkutano wa Mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu, nikuone pia katika Mikutano ya Wagombea akina Lipumba wa CUF na wa Seif Sharrif Hamad wa ACT-Wazalendo hadi na Wagombea wengineo wote.

Kukipenda mno Chama changu cha CCM na Mgombea wake Urais JPM haimaanishi nikiona Jambo la 'Kipumbavu' basi nilinyamazie tu. Nimekereka!
 
images(6).png

Hafai kusikilizwa na Muislamu Yoyote yule
 
Bwashee, Uamsho hawako chini ya Bakwata!
Kisheria Mufti ni kiongozi wa waislamu wote Tanzania.

Uamsho ni movement tu ndani uislamu.

Ni kama wanakarismati au wanamaombi ndani ya kanisa Katoliki.

Huu ni ushahidi tosha ccm bado hamyajui madai wala matatizo ya Waislamu.

Kwa hili la leo umma wa kiislamu Tanzania utazidi kumuunga mkono Sheikh Ponda kwa sababu hasimami kwenye batili bali haki.
 
Wewe subiri tu mikutano ya CCM mwisho itafunguliwa na wachawi, si unajua manyani wakianza kufa, waganga wamewamaliza, mashee na mapadire ndio hao bado wachawi.

CCM jambo dogo hili la kuwa wameshapoteza upendo kwa wananchi wanajifanya hawalielewi wala kuliona.
 
Kisheria Mufti ni kiongozi wa waislamu wote Tanzania.

Uamsho ni movement tu ndani uislamu.

Ni kama wanakarismati au wanamaombi ndani ya kanisa katoliki.

Huu ni ushahidi tosha ccm bado hamyajui madai wala matatizo ya waislamu.

Kwa hili la leo umma wa kiislamu Tanzania utazidi kumuunga mkono Sheikh Ponda kwa sababu hasimami kwenye batili bali haki.
Zanzibar kuna Bakwata?
 
Wewe subiri tu mikutano ya CCM mwisho itafunguliwa na wachawi,si unajua manyani wakianza kufa,waganga wamewamaliza ,mashee na mapadire ndio hao bado wachawi.
CCM jambo dogo hili la kuwa wameshapoteza upendo kwa wananchi wanajifanya hawalielewi wala kuliona.
Mufti ni mtu mkubwa mzito kama angekuwa anajitambuwa, kila mkoa kuna masheikh wa kufanya hizo duwa za mikutano, lakini ushabiki wa mufti mzima kutoka Dar mpaka Tanga kwa ajili ya duwa inayoweza kusomwa hata na Ustaadhi tu madrasa inafikirisha sana.

Sasa natamka rasmi si maaskofu wala Masheikh watakaouona ufalme wa Mungu

Ni rahisi kuwakuta walevi na mafirauni peponi kuliko hawa tunaowaita viongozi wa dini Tanzania hamna kitu, dini zote mbili.

Ukiwachekecha kupata cream ya viongozi halisi wa kidini wapo wachache mno.
 
Back
Top Bottom