Mufti Zubeir: Serikali inunue chombo cha kutazamia mwezi
Swali, Je ni jukumu la Serikali kufanya masuala ya dini?

===
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amekemea ufisadi, akihimiza jamii kulinda maadili, umoja na mshikamano, huku akiwaomba viongozi wa Serikali na wadau kusaidia upatikanaji wa darubini ya kukusanya taarifa za mwandamo wa mwezi ili kumarisha uhakika wa taarifa.

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi ambacho waumini wa Kislamu duniani hufunga kwa siku 30 kabla ya kusherehekea siku hiyo kupitia taarifa rasmi va mwandamo wa mwezi huo.

Hata hivyo, kabla ya kusherehekea, kifaa hicho (moon sighting machine) ndio hutumika kupata uhakika wa mwandamo wa mwezi huo kimani ili kuondoa utata au mabishano miongoni mwa waumini hao.

Sheikh Zubeir amesema hayo leo Jumanne Aprili 22, 2023 katika swala ya Eid EI- Fitr iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Wilaya ya Kinondoni, jijini hapa, ikihudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mabalozi, mawaziri na watu mashuhuri.

Chanzo: Mwananchi
Tunakoelekea, kubaya sana na haya ya serikali kutakiwa kununua kifaa cha kutazamia mwezi na mara mishahara iwahi kisa kuna Eid..!!
By the way, huo mwezi utakaokuwa unatazamwa ni upi, wa SUNI au wale wengine?
 
Tunakoelekea, kubaya sana na haya ya serikali kutakiwa kununua kifaa cha kutazamia mwezi na mara mishahara iwahi kisa kuna Eid..!! Huo mwezi utakaokuwa unatazamwa ni upe wa SUNI au wale wengine?
Aaahahaha

Utakuwa ni mwezi wa Bakwata
 
Pumbavu zao Bakwata,wametukosesha Bata la siku nne mfululizo Kwa ukilaza wao

Kumbae yawezekanq hata mwezi uliandama ***** ila Kwa sababu ya umasikini wao na ukosefu wa teknolojia ndo maana wanakosa ujasiri wa kutangaza Iddi Kwa usahihi

Bladifulu Bakwata
Ombeni ule utaratibu wa kufidia sikukuu zinazoangukia weekend urudi kama enzi ya Mzee Rukhsa.
 
Swali, Je ni jukumu la Serikali kufanya masuala ya dini?

===
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amekemea ufisadi, akihimiza jamii kulinda maadili, umoja na mshikamano, huku akiwaomba viongozi wa Serikali na wadau kusaidia upatikanaji wa darubini ya kukusanya taarifa za mwandamo wa mwezi ili kumarisha uhakika wa taarifa.

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi ambacho waumini wa Kislamu duniani hufunga kwa siku 30 kabla ya kusherehekea siku hiyo kupitia taarifa rasmi va mwandamo wa mwezi huo.

Hata hivyo, kabla ya kusherehekea, kifaa hicho (moon sighting machine) ndio hutumika kupata uhakika wa mwandamo wa mwezi huo kimani ili kuondoa utata au mabishano miongoni mwa waumini hao.

Sheikh Zubeir amesema hayo leo Jumanne Aprili 22, 2023 katika swala ya Eid EI- Fitr iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Wilaya ya Kinondoni, jijini hapa, ikihudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mabalozi, mawaziri na watu mashuhuri.

Chanzo: Mwananchi
Mbona hiyo ipo tayari, Zanzibar walipewa zawadi.

Utata haupo kwenye kuuona mwezi pekee, Utata pia upo ni wapi umeonekana.

Hii ihtilafu ni heri iachwe kama ilivyo, inaongeza ilm.
 
Back
Top Bottom