Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya

Beka ranger namjuwa tokea skiwa fundi maredio mara nasikia kaingia kwenye mipango,anyway kwa kino na migomigo hyo kawaida tu
Sema yule alikamatwa kwa kuvitwa,FBI hao hao walikuwa wanamsaka...kuna watu waliwakamsta nje huko ndy wakamtaje beka
Ona sasa wazungu walivyokuwa na akili wakikutaka,hawana haraka si walikuwa wanafanya naye biashara na kumpa pesa
Dili moja wakanuambia kwann usije huku uchukue tu pesa yako na kuna mpango mkubwa zaidi,beka si akaenda kichwakichwa ndy akanasa 😄

Ova
Hiyo story Yako ni nyingine Kuna mwamba mwingine alinaswa hapa hapa enzi za mkwele,
 
Chonchi alikamatwa kipindi cha JK akiwa ndio anakaribia kuondoka madarakani, hata shikuba alikamatwa kipindi cha JK pia
Yeah, 2014.Serikali karibu zote duniani zinajihusisha na hii biashara kwa namna moja ama nyingine na huwatumia watu fulani kisha baadaye wanawapoteza!

Yaani unakuta jamaa ni maarufu kwa kuuza madawa lakini hakamatwi! Kumbe yupo kwenye mfumo!Ingia wewe uone!

Yule jamaa mchoraji huwa nahisi anatumika na mfumo! Naona dalili za kuchokwa zimeanza, unafikiri Mwijaku alijitungia? Au wahenga wenzangu mnasemaje??
 
Joji white marehemu yule
Kama joji unamfahamu na mimi utakuwa unanifahamu sisi na kina joji ndio tulikuwa tunaishi kwenye hicho kighorofa Cha chonchi kabla hajainunua mwamba kabla hajaijenga hiyo ghorofa aliwaamisha wapangaji wa hiyo nyumba kwa kuwalipa Kodi Kila mpangaji nadhani Kodi ya mwaka au miezi 6 waende wakapange kwingine...!

 
Ndiyo na ana mdogo wake anaitwa Abuu
Abuu itakuwa ni WA mwisho huyo Mimi nilikuwa namfahamu George na Rose...last time nilisikia jamaa amezamia...!

Huyo mwamba Mimi nimekuwa nae nyumba moja hapo kwa chonchi enzi hizo Kuna uwanja usawa wa hiyo sheli ukivuka barabara watu walikuwa wanacheza mpira Cha ndimu mnaita🤣🤣🤣

Nimekumbuka mbali sana mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi😭😭😭​
 
Abuu itakuwa ni WA mwisho huyo Mimi nilikuwa namfahamu George na Rose...last time nilisikia jamaa amezamia...!

Huyo mwamba Mimi nimekuwa nae nyumba moja hapo kwa chonchi enzi hizo Kuna uwanja usawa wa hiyo sheli ukivuka barabara watu walikuwa wanacheza mpira Cha ndimu mnaita🤣🤣🤣

Nimekumbuka mbali​
Mzumbe hapo ndo tunachezaga cha ndimu, jamaa alifia nje ya nchi
 
Chonji ni Tajiri maarufu kule Nagomeni MwembeChai ni The Doni hasa.
Tangu mwaka 2010 alikuwa akiwika kama tajiri anayeibuka kwa kasi.

Kesi hii imekaa muda mrefu sana..
Hongera Dr Samia kwa kusimamia ukweli kuliko wale wenzako walioshindwa kazi wakaishia kubambikia watu madawa kwa chuki tu.
Kwani hukumu si imetolewa na mahakama?
 
Mzumbe hapo ndo tunachezaga cha ndimu, jamaa alifia nje ya nchi
Harafu nahisi mzumbe huko unapo sema ni mbali sana...hapo barabarani kulikuwa na uwanja inatizamana na hiyo Sheli...

Uwanja ulikuwa mbele ya nyumba ya warabu Kuna kibinti kimoja kilikuwa kinaitwa SAFAA...ila siku hizi nahisi atakuwa mshangazi🤣🤣🤣

Naizungumzia magomeni ya 1999 ujue​
 
Unamfahamu Nzinza...au nziii hapo kwenye hiyo nyumba ya mtama mchungu enzi hizo Kuna Mzee alikuwa anafuga MBWA...!
Kabla hicho kighorofa hakijajengwa...!
Ulikiwepo enzi hizo...?​
😂😂😂 mimi ni ile generation ya tatu hapo Makanya, nilikuwa nakaa nyumba ya chini baada ya kina Joji(Kwa Bi Manywele)
 
Huyu kama sijakosea ametangulia mbele za haki.(Naomba kusahihishwa) Alizamia South.
Ni Namibia nadhani harafu ndio akaenda huko south ni muhuni wa mwishoni mwishoni hivi dah...!

Enzi za uhuni magomeni vijana wengi walizamia na wengine Hadi Leo wapo nchi za mbali..!

Vijana wa magomeni wamesababisha wazazi wetu wahofie sana safari za nje...ilinichukua miaka 4 kumuaga mama kuwa nataka nikatafute maisha nchi za mbali miaka yote hiyo mama haku wahi kunikubalia...!

Chanzo ni vijana wa magomeni ambako mama yangu aliishi sana hapo na vijana wengi walio zamia wa hapo ama wengine walifungwa huko au waliuawa😭😭😭​
 
Back
Top Bottom