Muhimbili, kulikuwa na haja gani ya upasuaji kutenganisha watoto mapacha?

Mkuu wewe unatumia vizuri ubongo wako
 
Ilipangwa tu tusiwalaumu madaktari wana kazi nzito na ngumu sana!!
 
Haaa! Leo umeamua kuja kwa staili ya maswali tupu?
 
Kwenye operesheni kama hiyo hata kwa mabeberu chance of survival huwa ni ndogo sana
Kwa beberu na kwetu wapi chance ya survival ni kubwa zaidi na kwa kiwango kipi? Kweli ukweli usisemwe kuwa bongo Nyoso?

Wapumzike kwa amani malaika hawa they deserved more kama binadamu. Ndiyo maana huwa kuna guinea pigs au siyo?
 
Uzuri walifanikiwa watenganisha na wakaishi kwa siku kadhaa
 
Ni bora basi wangebaki vilevile kama wangefariki mbeleni natural death kama wale mapacha basi ni sawa kuliko hivi ilivyotokea.
Kubaki vile ni mateso
Kumbuka wale mabinti mapacha wa Iran walikuwa wameungana kichwani, walifika umri wa miaka 22. Waliomba watenganishwe licha kuambiwa uwezekano wa kuishi ni mdogo lakini waliomba wafanyiwe. Operation ilifanyika na wote wawili walikufa
 
Wakuu hawa mapacha wakuungana(conjoined twins) matibabu yao ni magumu sana,
Tafiti zinaonesha ni asilimia 60 tu ndiyo wanafanikiwa kuishi baada ya operation yaani kama wakifanyiwa operation watu 10 kati yao wataishi watu 6 tu...
Angalia hapa
 
Sasa hapo kipi ni bora mkuu?
Kuishi wakiwa vile au kufa mapema
 

Je, walivyofanyiwa Op walikufa hapo hapo?? --> Kwa vile walifanyiwa operation wakiwa hai, vifo vyao ni yatokanayo na operation hiyo.

Je, wangeweza kuishi kwa kuungana kule kwa muda gani? --> kwa vile walikuwa hai ni wazi wangekuwa hai leo. Hivyo ni sahihi kusema wangeishi kwingi zaidi (hata kwa saa moja zaidi) wakiwa wameungana kuliko yalivyotokea baada ya kutenganishwa.

Je, waliungana nini? --> hili waulize waliowatenganisha.

Je, nini chanzo cha vifo vyao? --> kwenye mada imeombwa tupewe maelezo ya kina kutokea hapo Mhimbili. Swali lako hili ni letu pia.

Je, hao Mabeberu Op zao zote hua zinafanikiwa hawajawahi kushindwa? --> beberu Wana facilities, resources, weledi, ubobezi, uzoefu nk uliopindukia kuliko mno yetu. Ndiyo maana kina Ayubu na wale raia daraja la kwanza wanakotibiwa. Huko failure rates zipo ila ni negligible na kwa hakika katu si kama kwetu.

Je, umejuaje kama kwenye hiyo Op mabeberu hawakuwepo au kutia Muongozo? --> Habari ya operation hii ilikuwa sana kwenye media. Neno kujimwambafy uliliona kwenye mada? Hatukujuzwa uwepo wao bali umwamba wetu. Hata hivyo kwanini kina Ayubu wao hawatibiwi hapa kwa usaidizi au mwongozo wa hao mabeberu?

Au wewe waonaje ndugu mjumbe?
 
Mapacha walioungana hata ulaya wapo , kuna wanaotenganishwa na kuna wanaoachwa wazeeke bila kuwagusa .
A human life is placed at very high value to take one , come with it very bold decision
Huko first class world operation kama hizi haziwei authorised na madaktari wa hopspitali moja .
 
Kwenye operesheni kama hiyo hata kwa mabeberu chance of survival huwa ni ndogo sana
Huwa hawafanyi kama chances za ku survive ni ndogo,
Hao mapacha walioungana wapo wengi tu wametenganishwa na wapo wa kutosha wanazeeka wakiwa wameungana
 
Reactions: Tsh
Mkuu, Mm naona Tununue vifaa, tukachukue ujuzi na tuwe makini. Hatuwezi kuanza moja kwa kupita njia waliyopita wengine kwa gharama za maisha. Huwezi sema naachana na ndege za mabeberu naanza moja kutest za kwangu kwa kutoa kafara abiria.
 
Mkuu, Mm naona Tununue vifaa, tukachukue ujuzi na tuwe makini. Hatuwezi kuanza moja kwa kupita njia waliyopita wengine kwa gharama za maisha. Huwezi sema naachana na ndege za mabeberu naanza moja kutest za kwangu kwa kutoa kafara abiria.
They must understand the principle of standing on others' shoulders. Hiyo reasoning yao kwenye masuala ya uhai ni immoral, evil, na criminal.
 
Reactions: Tsh
They must understand the principle of standing on others' shoulders. Hiyo reasoning yao kwenye masuala ya uhai ni immoral, evil, na criminal.
Nakubaliana na wewe 100% Jasmoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…