Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Wale raia Wamarekani na Ulaya wanaopenda kuhamia Tanzania, nadhani ni muda mwafaka wa kupewa free pass -- bila masharti yoyote maana wameonesha uzalendo.Hivi kisheria unawezaje kuukana uraia wa nchi yako ili kuepuka kudhalilishwa ?
Tayari tumepigwa.Niliposikia BBC wakitangaza Tanzania imenunua mashine mbili...kilichoendelea nikaishiwa nguvu nikazima redio.Nilikimbilia habari nikitamani kusikia ni mashine mbili za kupima Watanzania ugonjwa wa corona.Pengine wewe unazisikia sauna tu. Mimi nimezitumia miaka mingi tu. Tena kule kwa wenyewe, wenye sauna. Tatizo la hiki ''kituko'' cha Muhimbili ni kuwa wao wanapigia debe inatibu corona wakati wenye sauna wanazitumia kwa burudani. Ingekuwa sauna inasaidia kwenye corona basi nchi zenye sauna karibu kila nyumba kama Finland wasingehangaika.
Du kumbe zimenunuliwa? Mbona kutengeneza sauna ni kitu rahisi sana hata fundi wa mtaani anaweza kufanya kama ana ujuzi? All in all. Awamu hii imenifanya nijue ni kwa nini waafrika hatuendelea. Kumbe hata wasomi ''tumbo'' linawafanya wageuzwe nyuma mbele bila kujielewa.Tayari tumepigwa.Niliposikia BBC wakitangaza Tanzania imenunua mashine mbili...kilichoendelea nikaishiwa nguvu nikazima redio.Nilikimbilia habari nikitamani kusikia ni mashine mbili za kupima Watanzania ugonjwa wa corona.
Bahati mbaya hawajasema zinagharimu kiasi gani labda 1b au na zaidi.Ngoja tutajua tu.Kumwona daktari wa kibanda hiki book 5.Hajasema kwa muda gani.
Hiyo ni mashine au ni kibanda cha mlinzi.Kinagharimu shs.ngapi.Hiyo haisaidii chochote kwenye corona hii ya sasa.Naona waleeeeeee wanakuja taratibu.Hivi ukiingia humo kuna hewa ya kutosha au utazirai,hivi daktari anakupima kwanza kabla hujaingia humo au ikoje.
Ni kina nani hawaruhusiwi kuingia humo.
Naona tunafanya mambo ya ajabu wakati tulishaambiwa hakuna corona Tz.Juzi viongozi wa Dini Rc na KKKT tumewasikia vizuri.Tutatekeleza maelekezo yao. Haya ya shs.5000 mmmm?mmmmmmm?m???mmm?mm
Tunafanya mizaha sana.View attachment 1717207
View attachment 1717208
View attachment 1717209
View attachment 1717216View attachment 1717215
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hii leo imezindua rasmi mashine maalumu ambayo itatumika kutoa huduma za kujifukiza katika hospitali hiyo kuu ya rufaa nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Muhimbili Prof Lawrence Maseru ameeleza kuwa, mgonjwa atatumia dakika tano akivuta mvuke wenye mchanganyiko wa dawa asili.
Hata hivyo, wataalamu wengi wa afya pamoja na shirika la Afya Duniani (WHO) hawakubali matumizi ya mvuke kama tiba ya corona wakionya mvuke unaweza kusababisha madhara makubwa kwenye mfumo wa upuamaji ikiwemo kujaza mapafu maji.
Kuhusu katazo hilo la WHO, Prof Maseru amesema miti shamba imeonesha kuwa na tija.
"Hadi sasa hakuna Tiba ya covid hivyo kila dawa inapaswa kujaribiwa. Matumizi ya miti shamba yaonekana kuwa na faida," amesema Prof Maseru.
Uongozi wa Muhimbili pia umeeleza kuwa kwa sasa idadi ya wagonjwa wenye 'matatizo ya upumuaji' wamepungua hospitalini hapo.
Mashine tatu zaidi zinatarajiwa kufungwa katika hospitali hiyo na nyengine ikitarajiwa kufungwa katika tawi lake la Mloganzila lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mwaka uliopiita rais Magufuli alinukuliwa akisema kwamba wagonja wa virusi vya corona katika hospitali mbali mbali walikuwa wamepungua licha ya serikjali kutotoa takwimu rasmi za viwnago vya maambukizi.
Kiongozi huyo mara kwa mara amesisitiza kwamba watu hawafai kuwa na hofu kuhusu ugonjwa huo.
Serikali ilisitisha utangazaji wa takwimu za ugonjwa huo mara kwa mara mwezi Aprili baada ya rais kulalamika kwamba desturi ya kutangaza idadi ya wagonjwa ilikuwa inaongeza hofu.
Aidha serikali ya Tanzania ilisema ina wasiwasi kwamba kuwafungia watu kwa lengo la kuzuia maambukizi kunaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watu na uchumi, na pia hatua kama hiyo inaweza kuathiri sekta muhimu ya utalii.
Dkt Magufuli pia alitilia shaka usahihi wa matokeo ya vipimo vya corona vilivyokuwa vikifanywa na maabara ya taifa, baada ya sampuli za paipai na mbuzi kuonyesha zilikuwa na virusi.
Ni sawa na ushirikina wa wazungu tunaouita TeknerojiaUshirikina umegeuka kuwa bidhaa awamu hii.
Mitano tena
Safi sana...maana kuwategemea Wazungu wakati nasi tunayo sayansi yetu.TUPENDE VYA KWETU
Ule mvuke si ndo wanasema ni maji sasa vuta picha umevuta ule mvuke Mara mia inamana maji yatajaa mapafuni
Dawa ya kujifukizia wanayotumia hapo [and actually imekua ikiuzwa kwa miezi kadhaa (pia wengine hutumia kwa kunywa)], ni mafuta tete/essential oil ambayo inaitwa Bupiji. Haya mafuta nimeona duka moja wanauza 35,000/-.Kwani dawa ya kujifukizia ambayo india wameifanyia majaribio na ikaonyesha mafanikio ndiyo dawa tunayoitumia sisi kujifukizia?