Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Wanaume wenzetu wa Mwanza mnakwama wapi aisee huyu mbona ilikuwa wa kumuacha tuu usiku huo huo?

Wanaume wa dar huwa mnatuponda lakini ukweli unatakiwa utumie sana maarifa kuliko nguvu kwa wanawake wa sasa.
Inawezekana, jamaa wa nje anapesa ndefu
 
Muheshimu mwanaume wako acha mbwembwe na kujiona una akili sana, mbona mnapoomba matumiz hamtaki tukae mezan? Endelea na akili zako za kitoto hizo muwaache watoto yatima, hasira za mwanaume ni hatari sana, shauri yako.
Kama umemuoa TEGEMEZI basi jua ni sehemu ya MKATABA WA NDOA KUMUHUDUMIA....

usitake kumwekea vikwazo baada ya kumwoa!!!!!

Umemchoka ni bora mkaachana...
 
Na inakuwaje mwanamke anakuwa comfortable na mwanaume Aina hii?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sio wote wapo hivyo kuna saa maji yanazidi unga..., Kuna msemo The last Straw which broke the Camels Back...

Yaani unaweza ukawa unamuwekea ngamia mzigo kidogo kidogo ila mwishoni kumuongezea kafimbo tu mgongo ukavunjika, point ni kwamba sio hio fimbo iliyovunja bali ni ule mzigo kuanzia mwanzo uliomuwekea..., kwahio life is not black or white kuna a lot of grey areas....

Ila kwa wanaopenda wakijua tu kwamba kupendwa leo mpaka mtu anakuona kwenye gilasi sio kwamba na kesho atakupenda vilevile au hatamuona mwingine kwenye sahani

Difference between now na hapo kale mabibi zetu walikuwa wavumilivu na walikuwa hawana options sasa hivi kina mama wana option kwahio tegemea drama kama hizi mara kwa mara
 
Juzi tu IGP kasema usimuue mtu kama hamuendani muache.. achaneni.. there is always second chance
 
Haya mambo yanachangiwa na mkusanyiko wa matukio mbali mbali yanayopelekea maumivu na ghazabu.....hivyo kukosekana busara, uvumilivu, kuzuia hisia ama kuchukua hatua ya kujiondoa labda kutokana na sababu kadhaa ndio huleta matokeo haya.
 
Majuto yalimuandama akaona nae ajimalize, na hii ishu ya umiliki wa silaha naona vibali vinatolewa kifamba sana kuna watu hawastahili kupewa silaha, watu wana historia mbovu then unakuja mmilikisha silaha
Hivi kwani bunduki tu ndiyo zinahamasisha kudhuru au kujidhuru
Kwani angekuwa hana bunduki kuna visu mapanga hata kamba zipo
tutumie njia gani kudhibiti kamba na silaha nyingi watu wanazotumia kujidhuru

Kama hakuna njia ya kudhibiti hizi silaha nyingine hakuna sababu ya kuzuia watu kumiliki bunduki
 
Yalikua maamuzi sahihi.
Imagine umemkataza hajasikia na kaondoka show hua ni usiku mnene...unabaki na mawazo ya kinachoendelea .
Mara nyingi ukipiga cm hapokei au anazima cm kabisa.


Hasira zake akirudi usipime kabisa
 
Sure
 
Kitu ambacho wanaume tunasahau nikwamba utiifu wa mke unapaswa kupaliliwa kila muda.

Sio wewe ni nunda husikilizi la mtu wewe ni wewe alafu unataka binti wa watu awe anakusiliza tu. (Kwa watoto wasasa hapo imekula kwako)

Ni wanawake wachache sana ambao waume zao sio watu wakutoka alafu yeye mke awe anatoka. Hapa hii ni familia ya kula bata ila inaonekana mwanaume amekua na ubabe mwingi bata zake hapangiwi wala wife hana mamlaka ya kutia neno ila bata za wife yeye anatia ngumu.

Nimejaribu tu kuwaza kwa sauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…