Mume amemtuma mtoto wetu wa miaka mitano dukani usiku ni sahihi?

Kwanini yeye hakwenda kununua mpaka amtume mtoto mdogo hivyo tena mtoto mpaka anamwambia baba yake kuwa anaogopa daa inasikitisha sana
Huu ndio ukatili kwa watoto

Nikisema sisi kwa dini na maadili tunakatazwa kabisa kumtoa mtoto nje pindi jua likizama na wote wanakuwa wamerudi ndani
Ila kila mmoja na Imani yake na hapa kuna watakaobeza na kusema mbona kawaida ila akipatwa kitu chochote atalaumiwa mzazi au wazazi kwa kumtoa nje usiku

Utakuta baba alikuwa kwenye simu maana ndio wengi wamerogewa siku hizi
Kweli maisha yamekuwa tofauti sana nowadays
 
Angekuwa ni mtoto wa kiume tungesema ana mwelekeza the real world ila Kwa mtoto wa kike inaonekana kabisa bibi yake anataka leta ubushi mjini,Kaa na huyo ma mkwe mweleweshe kuwa Nyerere alishakufa na Miaka hii sio Ile ya 47'na Wala usimuogope maana madhara yakimkuta mtoto wataanza kukuangalia ww
 
mama yake ❌️

mama mkwe ✅️
Na tatizo limeanzia hapa.

Mleta mada unaonekana hu-appreciate mama wa mumeo kuwa mama yake (kama umenielewa vizuri yaani baada ya wewe kuolewa nae unataka kukaa nafasi zote mke/mama yake).huyo ni mama mkwe wako ulivyokataa asiongozane na mjukuu wake dukani ulijuaje kama baada ya kitu kununuliwa asingeenda na safari zake angesubiri hadi amuone amekaribia nyumbani ndiyo aondoke?

Hapa hutasema,lakini zipo dalili ameziona mumeo za wewe kutokumuheshimu mama yake au hupendi uwepo wake hapo kwenu na amefanya hivyo kutokana na panic labda nilichokiandika hapo juu mama mkwe wako alikuwa ameshamwambia mumeo wewe ukam-crush as if ni mtoto mwenzako,mambo ya familia yanataka sana hekima hapo mumeo amekupa kitu kama adhabu (well,amekosea) lakini ndiyo imeshatokea wewe next time kuwa na subira.
 
Naishi nae vizuri...hio point ya kusema amenipa kama adhabu na mimi nahisi hivyo...naona kama amejaribu kunionesha nmemkosoa mama mkwe na ma mkwe yupo sahihi
Mimi sidhan kama kuangalia zaidi usalama wa mtoto ni kumkosea heshima na nilisema kwa ustaarab
 
Angekuwa ni mtoto wa kiume tungesema ana mwelekeza the real world ila Kwa mtoto wa kike inaonekana kabisa bibi yake anataka leta ubushi mjini,Kaa na huyo ma mkwe mweleweshe kuwa Nyerere alishakufa na Miaka hii sio Ile ya 47'na Wala usimuogope maana madhara yakimkuta mtoto wataanza kukuangalia ww
Maisha hayapo hivi bro,unazungumzia ya Nyerere hata wewe ukija kufikia umri wa kuitwa mkwe wa mtu kuna vitu utataka viende sawa na dunia uliyopo na uoni unaouona wewe,sisi ni Waafrika siyo wazungu tumezoea kuishi kwa umoja wa kifamilia ukiendekeza uzungu kizazi chako kitakatwa na laana ya mzazi wako.

Hii changamoto nilishawahi kukutana nayo ktk familia yangu mama na mke wangu walikuwa wanakaa hata miezi sita hawapigiani simu sababu mama alipokuja mjini kupumzika alimkera wife kitu fulani ikawa ugomvi,nilikaa na wife nikamwambia yule ni mama yangu hakuna namna utasema asije kwetu au wewe usimsalimie ukijua wazi yupo mbali na ana maradhi yake cha kufanya jishushe chochote atakachokwambia as long as hakikudhuru vumilia likiwa zito sana niambie mimi nitakaa nae chini tusahihishane.

Alinielewa maisha yanaenda.
 
Naishi nae vizuri...hio point ya kusema amenipa kama adhabu na mimi nahisi hivyo...naona kama amejaribu kunionesha nmemkosoa mama mkwe na ma mkwe yupo sahihi
Mimi sidhan kama kuangalia zaidi usalama wa mtoto ni kumkosea heshima na nilisema kwa ustaarab
Ulipomwambia mumeo akae nje akimchungulia je alifanya hivyo au hakufanya hivyo?
 
Huyo mama mkwe ni mpumbavu at all grounds haijalishi wewe na yeye hamuelewani. Hii ni aina nyingine ya ukatili kwa watoto. Muafrika hajafikia pointi ya ustaarabu. Ni suala nitaendelea kulisisitiza siku zote za maisha yangu.
Usimuite mama wa mtu hivi please mkuu.

Tuna namna nyingi na nzuri za kukosoa watu hata kama hatuwajui,kila mtu anampenda mzazi wake tujaribu kuheshimu hisia zao.hili nimezidi kulijua na kuliamini juzi mwezi august jamaa yangu aged 52 alifiwa na mama yake akalia kama mtoto mdogo,miaka 52 tayari ameigawa karne lakini bado ana mapenzi makubwa kwa mama yake.

My point is,jamaa akiona ulichoandika hapa na jinsi anavyomthamini mama yake asingekuelewa hata kidogo.
 
Maisha hayapo hivi bro,unazungumzia ya Nyerere hata wewe ukija kufikia umri wa kuitwa mkwe wa mtu kuna vitu utataka viende sawa na dunia uliyopo na uoni unaouona wewe,sisi ni Waafrika siyo wazungu tumezoea kuishi kwa umoja wa kifamilia ukiendekeza uzungu kizazi chako kitakatwa na laana ya mzazi wako.

Hii changamoto nilishawahi kukutana nayo ktk familia yangu mama na mke wangu walikuwa wanakaa hata miezi sita hawapigiani simu sababu mama alipokuja mjini kupumzika alimkera wife kitu fulani ikawa ugomvi,nilikaa na wife nikamwambia yule ni mama yangu hakuna namna utasema asije kwetu au wewe usimsalimie ukijua wazi yupo mbali na ana maradhi yake cha kufanya jishushe chochote atakachokwambia as long as hakikudhuru vumilia likiwa zito sana niambie mimi nitakaa nae chini tusahihishane.

Alinielewa maisha yanaenda.
Hizo tamaduni zibaki tu,na kama laana ije ila Kwa Dunia ya Sasa siwezi muacha mtoto wa kike atembee mwenyewe usiku,hata wa kiume na Sio uzungu mkuu nyakati zimebadilika.
 
Hajawahi kufanya hivyo ni mara ya kwanza. Ilikua hivi mama yake ambae kwa sasa tupo nae aligundua kuna kitu kimepelea jikoni akamwambia mtoto wetu wa kike (ambae mara nyingi muda huo wa saa tatu na nusu usiku anakua ameshalala kasoro hii leo ) waongozane yeye kuna sehem anaenda mara moja wapitie dukan wanunue hicho kiungo ampe arudi mwenyewe .

Mimi kusikia hivyo nikamwambia sasa hiv usiku na kuna giza huko nje japo duka halipo mbali. Dada wa kazi akimaliza anachofanya au mimi nitaenda kuchukua . Mama mkwe akajibu sawa akaondoka, baada ya kama dakk 5 mume wangu akasema kwann mtoto asiende dukan yeye anamtuma. Nikamwambia sio sawa ni usiku sana mimi nitaenda akalazimisha .

Mtoto akatoka nje alivyofika mbal na eneo la nyumbani akarudi kumuomba baba ake akae nje awe anamuangalia kwa kua anaogopa. Mimi sijapenda hichi kitendo kwa kua hakukua na ulazima wq mtoto kwenda. Je ni sahihi na mimi nina overreact? Ushauri tafadhali ili nijue namna nzuri ya kuhandle hii situation ikitokea tena.
Hii nayo ya kufungulia uzi!!!??? Aisee!
 
Hizo tamaduni zibaki tu,na kama laana ije ila Kwa Dunia ya Sasa siwezi muacha mtoto wa kike atembee mwenyewe usiku,hata wa kiume na Sio uzungu mkuu nyakati zimebadilika.
Una point za msingi sana lakini wazee wanaangalia mambo kwa angle tofauti na sisi vijana.

Ndiyo nikasema hata wao hatari wanazijua tena Bibi na mjukuu jinsi wanavyowajali sometimes ni hata kukuzidi wewe mzazi lakini kwa case hapa duka haliko mbali,hatujui Bibi aliwaza nini kwenda na mtoto obviously itakuwa alikuwa anunue kitu amkabidhi kisha amuangalie mpaka akiingia nyumbani ndiyo aondoke ila mama mtoto aka-panic.
 
Back
Top Bottom