Hajawahi kufanya hivyo ni mara ya kwanza. Ilikua hivi mama yake ambae kwa sasa tupo nae aligundua kuna kitu kimepelea jikoni akamwambia mtoto wetu wa kike (ambae mara nyingi muda huo wa saa tatu na nusu usiku anakua ameshalala kasoro hii leo ) waongozane yeye kuna sehem anaenda mara moja wapitie dukan wanunue hicho kiungo ampe arudi mwenyewe .
Mimi kusikia hivyo nikamwambia sasa hiv usiku na kuna giza huko nje japo duka halipo mbali. Dada wa kazi akimaliza anachofanya au mimi nitaenda kuchukua . Mama mkwe akajibu sawa akaondoka, baada ya kama dakk 5 mume wangu akasema kwann mtoto asiende dukan yeye anamtuma. Nikamwambia sio sawa ni usiku sana mimi nitaenda akalazimisha .
Mtoto akatoka nje alivyofika mbal na eneo la nyumbani akarudi kumuomba baba ake akae nje awe anamuangalia kwa kua anaogopa. Mimi sijapenda hichi kitendo kwa kua hakukua na ulazima wq mtoto kwenda. Je ni sahihi na mimi nina overreact? Ushauri tafadhali ili nijue namna nzuri ya kuhandle hii situation ikitokea tena.
Kuna issue 2:
1. Mama Mkwe yupo, hayo mazingira kum challenge mme, kuwa nayo makini especially kwenye issue ambayo Mama mkwe is involved.
2. Kwa nini wewe usinge voluntary amua kwenda instead ya mtoto au kumsindikiza mtoto, halafu bada ya hiyo issue ukateta na Mume wako?
3. Kwa nini Dada wa kazi aende dukan saa 3 mwenyewe? Ninaye Dada wa kazi ana miaka 19, ikifika saa 1 lazima asindikizwe dukani.
Maoni yangu:
- Kwa sababu mume kaona ume mu attack mbele ya Mama ya kum challenge mbele ya Mama yake, akaona akaze, ila amefanya jambo la kipumbavu sana.
- Kwa nini mtoto amwambie Baba yake amuangalie, asikuambie wewe au kwa nini wewe usingeenda na Mama? Inaonekana wewe ni mvivu ana sio kimbilio la mtoto.
Ushauri:
- Usimtume Dada mtoto wa watu usiku.
- Usi challenge mme wako akiwa na Mama yake.
- Jitoe kwa hiyari kusaidia jambo kama unaona mtoto si salama.
Bado nawaza:
Inawezekanaje Baba na Mama wapo ndani, mtoto wa miaka 5 aende dukani, Mume ni mshenzy na wewe ni mtu wa hovyo maana ungeweza inuka ukaenda.
Acha mdomo, the fact kwamba umeleta hii issue humu, ina maana bado unq ligi nayo, acha ligi na Mume, hili ni jambo dogo sana na kueleweshana.
Kuwa makini na huyo Mama Mkwe, hilo jibu lake la sawa sio zuri na ndo limeleta reaction yote hiyo, sasa na mume alivyo wa hovyo akataka mwonyesha Mama yeye ana msimamo