Wewe Ni superwoman 💐 Una akili Sana.Hivi hizi pesa wanawake tunazotafuta kama haziwezi kusaidia familia zetu ni za nini sasa[emoji2297][emoji2297][emoji2297]
Na hawa wachungaji jamani sijui ni madawa au ni kitu gani!! Wamewashika watu ufahamu hawasikii wala hawaambiliki.
Mkuu hujaelewa Nini hapo?Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Mwalimu wa shule ya Sekondari Jijini Mbeya, Julieth Kabuja (32) ameieleza Mahakama ya mwanzo Mkoani hapo kuwa ni bora ndoa yake ivunjike kuliko kumkabidhi mumewe kadi yake ya benki.
Ameyazungumza hayo mbele ya Mahakama ya mwanzo jijini hapo baada ya mumewe Charles Meshack (31) kufungua shauri la madai ya talaka akitaka kuachana na mkewe kwa kuhama dhehebu la katoliki na kuhamia la kilokole.
Aidha Meshack ambaye ni Askari Magereza amedai mkewe baada ya kuhamia katika ulokole fedha zake amekuwa akizipeleka kanisani kitendo kinachosababisha yeye kuzidiwa na majukumu ya familia.
“Naumia sana na majukumu, kodi ya nyumba nilipe mimi, ada za Watoto na chakula vyote mimi, halafu yeye mshahara wake apeleke kanisani, bora tuachane” alisema Meshack.
Hata hivyo Julieth aliiambia Mahakama kuwa yeye na mume wake wote ni wafanyakazi, lakini anashangaa anataka kumiliki kadi zote.
“Siku moja aliniamsha usiku na kuniambia nisipokubali kumkabidhi kadi yangu ya benki bora tuachane kwa kisingizio yeye alinilipia mahari hivyo mimi na kila kitu changu kipo chini yake, yaani kazi nifanye mimi halafu mshahara nimuachie huyu bwana, nipo tayari kuachika lakini siyo kuacha kadi yangu” alidai Julieth
Baada ya Hakimu Hafsa Shelimo kusikiliza pande zote mbili, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 12, mwaka huu kwaajili ya hukumu.
Chanzo: Swahili Times
Yah huo ni ujinga mkubwa yan bora angekuwa na mke hana kaz angejua moja. Ila hela yote unafanyia kanisa sasa si ukaolewe na kanisa.Hapo hoja ya mume ni pesa inakwenda kanisani alafu nyumbani mke hajitutumui kutoa support kwa damu yake, nadhani kama ingekuwa haiendi kanisani sidhani kama mume ange-mind yaani hata ingekuwa inapotelea kusikojulikana
Kitu hujui uliza! Huyo efatha alikuwa si Mchepuko wake?Hilo gari lilikuwa la mkewe.Likwelile akawa analazimisha kulitumia kwa mambo ya ufuska na wanawake wengine
Mke akaona Mateso mengi ndani akaokoka na akaona kuliko hilo gari lake limtumikie shetani heri atoe litumike kwa kazi ya Mungu kuliko mumewe awe analitumia kwenda kwa malaya na kubeba malaya wake
Mwanaume aka mind kukosea hiyo gari
Mimi lofa tuu lakini natoa miongozo vipi hapo.Mwanaume lofa hawezi toa miongozo kwa mwanamke mwenye kazi yake ma pesa kumzidi
Huo ndio ukweli, ukitaka ndoa ife chukua hela ya mwanamke uiweke kwenye matumizi ya familiaWanaume tafuteni pesa, pesa ya mwanamke ni yake, ila ya mume ni yenu.
Acha kutetea ujinga, bora pesa ibaki kwa familia ili isaidie hata Watoto kuliko hiyo pesa iliwe na Mchungaji huko kanisani!!Huo ndio ukweli, ukitaka ndoa ife chukua hela ya mwanamke uiweke kwenye matumizi ya familia
Bora mwanamke huyo aache kazi nimuhudumie kuliko mwanamke anafanya kazi halafu hela zake hazifanyi kazi kwenye familia.Mama abakie hapo hapo.
Anaitaka ATM aisee
Mwanamke kweli umkabidhi mime ATM? That is too much
Wanawake vizuri kuomba Mungu kutopata kidume kilofa kama hicho hopeless kabisa kiofisa magereza
Kinadhalilisha jeshi la magereza wanawake wenye kazi zao watakatakaa kuolewa na Askari magereza kuwa watawapokonya ATM
Kwa hiyo unataka kusema kua hata Mumewe na Rais wetu hawezi toa miongozo kwa Mkewe kisa Mkewe ana pesa kumzidi yeye!? Ebu acha kufikiri kwa kutumia tumbo,wenzako huwa tunafikiria kwa kutumia kichwa na si tumbo au masaburi!!Mwanaume lofa hawezi toa miongozo kwa mwanamke mwenye kazi yake ma pesa kumzidi
Mkiendelea kuota hizo ndoto na mjiandae kuwa wengi.Nakuoa halafu naoa tena.Sijui umeelewa?Wanaume tafuteni pesa, pesa ya mwanamke ni yake, ila ya mume ni yenu.
Mwamba kasanuka,kumbe anaibiwa Mali zake na Mchungaji!!Hakuna cha kutuangusha wala nini mi naona mwamba katuwakilisha vyema, achague kutoa ATM CARD au ASEPE TU, huwezi fanya kazi mshahara mzima unaupeleka kwa mpigaji mmoja kwa kisingizio cha mchungaji,
Ila baba mchungaji akitaka kadi ya benki anapewaHata kama mwanaume ni kichwa cha familia ila namsapoti huyo mwamba kutaka ndoa ivunjike huo ni upimbi. Unafanya kazi kwa bidii mnaishi kwa tabu ila hela ya mwenzio ingekua hata anajenga kwao au anajinunulia nguo ni sawa ila anampa fala mmoja tu huko anayejiita mtume huo ni ufala wa hali ya juu.
Huyo mwanamke kudai mume anataka Kadi ya benki ni uongo asilimia 900. Ampe talaka tu akalitumikie kanisa vyema.