Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Hivi hizi pesa wanawake tunazotafuta kama haziwezi kusaidia familia zetu ni za nini sasa[emoji2297][emoji2297][emoji2297]

Na hawa wachungaji jamani sijui ni madawa au ni kitu gani!! Wamewashika watu ufahamu hawasikii wala hawaambiliki.
Wewe Ni superwoman 💐 Una akili Sana.
 
Ni aibu dume Zima kung'ang'ania fedha za mkeo. Sio kazi yake kuhudumia familia. Kidume ng'ang'ana !!! Akikunyima chini ya kitovu hapo nenda mahakamani... Lakini sio kadi yake ya benki.!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Mkuu hujaelewa Nini hapo?
Mke kahama kanisa lao na kujiunga na walokole, kwa ambao hawawajui Hawa walokole anaweza asielewe hili.
Kuna jamaa yangu kakuta kadi ya mchango kwenye biblia mkewe mlokole kaficha humo anajua mume hafunguagi biblia, mke anakumbushwa kuhusu ahadi ya million moja shilling alizoahidi kutoa kanisani kununua vyombo vya mziki wakati Kila mwezi mke anamlilia aongeze hela za matumizi.
Kumuuliza hiyo kadi kulizuka bonge la ugomvi.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu wa shule ya Sekondari Jijini Mbeya, Julieth Kabuja (32) ameieleza Mahakama ya mwanzo Mkoani hapo kuwa ni bora ndoa yake ivunjike kuliko kumkabidhi mumewe kadi yake ya benki.

Ameyazungumza hayo mbele ya Mahakama ya mwanzo jijini hapo baada ya mumewe Charles Meshack (31) kufungua shauri la madai ya talaka akitaka kuachana na mkewe kwa kuhama dhehebu la katoliki na kuhamia la kilokole.

Aidha Meshack ambaye ni Askari Magereza amedai mkewe baada ya kuhamia katika ulokole fedha zake amekuwa akizipeleka kanisani kitendo kinachosababisha yeye kuzidiwa na majukumu ya familia.

“Naumia sana na majukumu, kodi ya nyumba nilipe mimi, ada za Watoto na chakula vyote mimi, halafu yeye mshahara wake apeleke kanisani, bora tuachane” alisema Meshack.
Hata hivyo Julieth aliiambia Mahakama kuwa yeye na mume wake wote ni wafanyakazi, lakini anashangaa anataka kumiliki kadi zote.

“Siku moja aliniamsha usiku na kuniambia nisipokubali kumkabidhi kadi yangu ya benki bora tuachane kwa kisingizio yeye alinilipia mahari hivyo mimi na kila kitu changu kipo chini yake, yaani kazi nifanye mimi halafu mshahara nimuachie huyu bwana, nipo tayari kuachika lakini siyo kuacha kadi yangu” alidai Julieth

Baada ya Hakimu Hafsa Shelimo kusikiliza pande zote mbili, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 12, mwaka huu kwaajili ya hukumu.

Chanzo: Swahili Times

Suala la kutunza mke ni suala la mme kisheria,na sheria inaenda mbali zaid inasema endapo pesa ya matumiz itakosa ndan mwanamke ana haki ya kuuza vitu vya ndani ili apate pesa ya chakula
 
Hapo hoja ya mume ni pesa inakwenda kanisani alafu nyumbani mke hajitutumui kutoa support kwa damu yake, nadhani kama ingekuwa haiendi kanisani sidhani kama mume ange-mind yaani hata ingekuwa inapotelea kusikojulikana
Yah huo ni ujinga mkubwa yan bora angekuwa na mke hana kaz angejua moja. Ila hela yote unafanyia kanisa sasa si ukaolewe na kanisa.
Hawa watumishi wa Mungu wengne n mashetan wanajifanya watu. Kwa hali ya kawaida tu hata huyo mchungaji mke wake angefanya hvyo pangechmbika
 
Huyu mwamba miaka 31
Mke miaka 32
So anazidiwa ujanja na bibie kwa namna fulani. Maafande jela jela hapo Mbeya mwiteni mwamba mpeni somo la UBAHARIA kuna issue unafinyia ndan kwa ndani mpaka somo linaeleweka
 
Hilo gari lilikuwa la mkewe.Likwelile akawa analazimisha kulitumia kwa mambo ya ufuska na wanawake wengine
Mke akaona Mateso mengi ndani akaokoka na akaona kuliko hilo gari lake limtumikie shetani heri atoe litumike kwa kazi ya Mungu kuliko mumewe awe analitumia kwenda kwa malaya na kubeba malaya wake

Mwanaume aka mind kukosea hiyo gari
Kitu hujui uliza! Huyo efatha alikuwa si Mchepuko wake?
 
Mama abakie hapo hapo.
Anaitaka ATM aisee

Mwanamke kweli umkabidhi mime ATM? That is too much

Wanawake vizuri kuomba Mungu kutopata kidume kilofa kama hicho hopeless kabisa kiofisa magereza

Kinadhalilisha jeshi la magereza wanawake wenye kazi zao watakatakaa kuolewa na Askari magereza kuwa watawapokonya ATM
Bora mwanamke huyo aache kazi nimuhudumie kuliko mwanamke anafanya kazi halafu hela zake hazifanyi kazi kwenye familia.
 
Hakuna cha kutuangusha wala nini mi naona mwamba katuwakilisha vyema, achague kutoa ATM CARD au ASEPE TU, huwezi fanya kazi mshahara mzima unaupeleka kwa mpigaji mmoja kwa kisingizio cha mchungaji,
Mwamba kasanuka,kumbe anaibiwa Mali zake na Mchungaji!!
 
Mwambie huyo afisa magereza amlete mkewe niwe namhurumia,aachane na issue ya ATM kadi ya mkewe.
 
Mwanamke mpumbavu sana huyo, si bora basi angemjengea mama yake kajumba...unachukua mshahara wote unaprleka kanisani, hizo ni akili kweli...upimbi wa baadhi ya wanawake ni shida sana.

Sisemi kidume alalamike kutosaidiwa majukumu ya nyumbani, ila mtu kuchukua mshahara wote kupeleka church huku home kuna pressing issues na bado mnaishi umasikini ni upumbavu wa hali ya juu.
 
Hata kama mwanaume ni kichwa cha familia ila namsapoti huyo mwamba kutaka ndoa ivunjike huo ni upimbi. Unafanya kazi kwa bidii mnaishi kwa tabu ila hela ya mwenzio ingekua hata anajenga kwao au anajinunulia nguo ni sawa ila anampa fala mmoja tu huko anayejiita mtume huo ni ufala wa hali ya juu.

Huyo mwanamke kudai mume anataka Kadi ya benki ni uongo asilimia 900. Ampe talaka tu akalitumikie kanisa vyema.
Ila baba mchungaji akitaka kadi ya benki anapewa
 
Back
Top Bottom