Mume amfikisha mahakamani mkewe kwa kupeleka mshahara wake kanisani

Ngoja msumeno uume pande zote mbili
1.Kama mdada anapeleka pesa kanisani basi kanisa ndio limuoe ajue kutengenisha kanisa na upendo ndani ya nyumba.Wakina mama wengi ni mateka wa dini za kilokole wakishakolea sana heshima nyumbani inashuka anatumia muda mwingi kuhudumia kanisa kuliko mume wake hata wakati mwingine anaweza kukuambia nachelewa kwenda kwa mchungaji nitakupikia nikirudi.Hili na mimi linanitesa kwa sasa nilikuwa namuachia kadi yangu lakini nimemnyang'anya kwa sasa.Wakina dada ya kaizari mpeni kaizari ya mungu mpe mungu.
2.Na wewe mwanaume acha udikteta huwezi sema mke eti uchukue kadi yake kisa umemlipia mahari mwanamke sio ATM naye ana haki yake.Ungekuwa muislam ungenielewa waislam wao mwanamme huna haki ya kuuliza mshahara au ujira wa mkeo wewe ndio una haki ya kumtunza na kumlisha hela yake ni kujipanda ili akupendezeshe wewe wewe.Mahari sio kununua mtu ni utaratibu tu wa kimila hasa za kiafrica ndio maana wazungu hawana kitu inaitwa mahari.Kumbuka wakati anatoka kwao kulikuwa na ugali hakufuata ugali kwako.Kumbuka kwao kulikuwa na mashamba hakuja kukulimia wewe
 
Kama mmeamua kuishi pamoja kama ndoa ni vizuri rasilimali za familia zikawa wazi na kutumika ipasavyo.

Ndio maana hata mume anapochepuka hupelekea kupotea Kwa rasilimali fedha za familia.

Kwa hiyo mwenza kuingilia kati ni Sawa tu
 
Hata kodi zetu zinazoliwa na hawa mafisadi hatuwapi mkononi bali tunaingiza kwenye accounts za serikali lakini mafisadi wanazifikia na kuzitafuna.

Mchungaji hakabidhiwi pesa mkononi lakini tunajua zinamfikia na anazitafuna vizuri tu. Hivyo hoja yako ni dhaifu sana
 
Anayetakiwa kujua pesa za sadaka zinaliwa na mchungaji ni wewe wa nje au waumini wanaotoa sadaka?
 
hakuna ndoa hapo......mume 31, mke 32...........nna hakika isiyo na uthibitisho....mke kapata mchepuko barafu.........na mmewe ni bwege.....sidhani kama alishawahi piga PULI.......
 
Hayo ni matatizo ya kifamilia mahakamani Hakuna ufumbuzi wake
 
Sababu za kikinga sana za kuacha ndoa, je sisi wenye watu wenye tabia ngumu still tunadunda miaka.
Kuna wanandoa Wana magumu yasiyovumilika lakini still wanapita.
Kama utaki changamoto oa malaika.
 
Kugombea umiliki/utawala ndio chanzo cha migogoro 90% ya ndoa. Mwanamke anataka awe sterling, mume nae hawezi kubali pokonywa sterling. KILA mmoja akiitambua mipaka yake inaishia wapi ndoa ni paradiso.
 
Huu msemo wa pesa ya mke ni ya mke na za mume ni zetu umewaharibu Sana wanawake saikolojia, wao ndio wanufaika wakuu pindi watoto wanapofanikiwa huku wanaume wakibakia kama bulldozer linatengeneza barabara ikishakamilika sio ruhusa kutumia barabara.
 
Ama kweli huyo afande kadhihirisha jeshi letu linamapungufu alitakiwa kumpiga na kitu kizito anavokuja kukumbuka miaka ishapita
 
Cha muhimu jamaa angemuomba mama amsaidie baadhi ya majukumu maisha yamebana sana
 
Kuwa hakimu, jaji ni kazi ngumu, mara watu wagombanie kadi za benk, mara zumaridi ajiite Mungu na kupoteza watu, mara wanaoshindwa kuelewana kitandani hawa wote mizigo inapelekwa mahakamani dah, mara mke asiende kwa shoo ya diamond apigwe chuma aiseee
 
sio mda risas zitarindima.kumbuka ni askar huyo
 
Ila huko kanisani wakiitaka hiyo atm kadi ataitoa kilainiiii[emoji23][emoji23]
 
Mafeminist mna taabu ninyi si mnataka 50/50 ila kwenye majukumu ya kifamilia hapana[emoji23] halafu hakimu ahukumu kwa mujibu wa sheria au ampendelee mwanamke kwenye hukumu kisa ni mwanamke mwenzake[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…