NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Ngoja msumeno uume pande zote mbiliMwalimu wa shule ya Sekondari Jijini Mbeya, Julieth Kabuja (32) ameieleza Mahakama ya mwanzo Mkoani hapo kuwa ni bora ndoa yake ivunjike kuliko kumkabidhi mumewe kadi yake ya benki.
Ameyazungumza hayo mbele ya Mahakama ya mwanzo jijini hapo baada ya mumewe Charles Meshack (31) kufungua shauri la madai ya talaka akitaka kuachana na mkewe kwa kuhama dhehebu la katoliki na kuhamia la kilokole.
Aidha Meshack ambaye ni Askari Magereza amedai mkewe baada ya kuhamia katika ulokole fedha zake amekuwa akizipeleka kanisani kitendo kinachosababisha yeye kuzidiwa na majukumu ya familia.
“Naumia sana na majukumu, kodi ya nyumba nilipe mimi, ada za Watoto na chakula vyote mimi, halafu yeye mshahara wake apeleke kanisani, bora tuachane” alisema Meshack.
Hata hivyo Julieth aliiambia Mahakama kuwa yeye na mume wake wote ni wafanyakazi, lakini anashangaa anataka kumiliki kadi zote.
“Siku moja aliniamsha usiku na kuniambia nisipokubali kumkabidhi kadi yangu ya benki bora tuachane kwa kisingizio yeye alinilipia mahari hivyo mimi na kila kitu changu kipo chini yake, yaani kazi nifanye mimi halafu mshahara nimuachie huyu bwana, nipo tayari kuachika lakini siyo kuacha kadi yangu” alidai Julieth
Baada ya Hakimu Hafsa Shelimo kusikiliza pande zote mbili, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 12, mwaka huu kwaajili ya hukumu.
Chanzo: Swahili Times
1.Kama mdada anapeleka pesa kanisani basi kanisa ndio limuoe ajue kutengenisha kanisa na upendo ndani ya nyumba.Wakina mama wengi ni mateka wa dini za kilokole wakishakolea sana heshima nyumbani inashuka anatumia muda mwingi kuhudumia kanisa kuliko mume wake hata wakati mwingine anaweza kukuambia nachelewa kwenda kwa mchungaji nitakupikia nikirudi.Hili na mimi linanitesa kwa sasa nilikuwa namuachia kadi yangu lakini nimemnyang'anya kwa sasa.Wakina dada ya kaizari mpeni kaizari ya mungu mpe mungu.
2.Na wewe mwanaume acha udikteta huwezi sema mke eti uchukue kadi yake kisa umemlipia mahari mwanamke sio ATM naye ana haki yake.Ungekuwa muislam ungenielewa waislam wao mwanamme huna haki ya kuuliza mshahara au ujira wa mkeo wewe ndio una haki ya kumtunza na kumlisha hela yake ni kujipanda ili akupendezeshe wewe wewe.Mahari sio kununua mtu ni utaratibu tu wa kimila hasa za kiafrica ndio maana wazungu hawana kitu inaitwa mahari.Kumbuka wakati anatoka kwao kulikuwa na ugali hakufuata ugali kwako.Kumbuka kwao kulikuwa na mashamba hakuja kukulimia wewe