Mume anataka kumuacha mke kisa kumpeleka mtoto shule na ex wake

Hiyo ni kwa imani yako, sasa msimamo wa imani yako siyo msimamo wa dunia acha ujinga, kwa imani yangu hakuna mtoto haramu, wala mtoto wa zinaa mtoto ni mtoto tu ilimradi kazaliwa.
Kwa hiyo wewe unaweza kuzaa na mamako, dadako, shangazi yako?
 
Kazi kweli kweli
Hata mimi siwezi kuendelea kuwa na wewe kama mke wangu sababu hauheshimu kile nachokwambia usikifanye

Video call haiwezi kuniaminisha kuwa umelala mwenyewe

Kwa uchache na kwa ufupi sana bado upo kwenye mahusiano na huyo X wako(BADO MNAKULANA)
Lakini wanaume na sisi ni wapumbavu sana. Mtu ulimshindwa akapata pa.kujistiri na amekuwa mke wa mtu, unahangaika naye nini? Hivi haya mauaji ya wivu wa mapenzi hayatustui?
 
Kwa hiyo wewe unaweza kuzaa na mamako, dadako, shangazi yako?
Kwani huyo bwana katika story yake kasema kazaa na mama yake au dadake au shangazi yake?

Halafu dini yako yenyewe ni matokeo ya mtoto wa nje ya ndoa kwa hiyo nayo ni haramu?

Lakini pia nyie si dini yenu inaruhusu kuoa binamu ,mtoto wa baba mdogo.
 
wadau huyu Dada tumshauri nn?
Mume wangu anataka kuniacha kwa kumpeleka Mtoto shule Mimi na X ambaye tulizaa kabla ya ndoa!

Mimi ni mama wa watoto 3. Mtoto wangu wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa kwenye mahusiano lakini alikuja kuoa mwanamke mwingine. Mwanzo mimi na yeye hatukuwa tunaongea kabisa kwani aliniacha vibaya, baadaye nilikutana na huyu mume wangu wa sasa. Katika mahusiano alikuwa ni mwanaume mzuri mpaka nikasahau kama nilishawahi kuumizwa.

Mpaka tunafunga ndoa, nilikuwa sifikirii kabisa kuhusu baba wa mtoto wangu, kwani huyu mume wangu alikuwa ananihudumia mimi na mwanangu kwa kila kitu. Kuna kipindi baba wa mtoto alirudi na kuomba msamaha, akasema anataka kuwa sehemu ya maisha ya mtoto na kulipa ada na mambo mengine.

Nilimkubalia na kwa kuwa ni mtoto wangu sikuona haja ya kuomba ruhusa kutoka kwa mume wangu, hivyo akaanza kulipa ada. Baadaye nililazimika kumwambia mume wangu kuwa ada inalipwa na baba yake mtoto, kwani kuna kipindi walilipa ada mara mbili shuleni.

Mume wangu alilipa ada ya mtoto bila kuniambia, wakati huo baba yake alikuwa tayari ameshalipa. Alikasirika kwa nini sikumwambia, lakini nilimwambia ni mwanangu na yule ni baba yake, hivyo ana haki zote. Tuliongea, yakasahaulika kwani watu waliniambia hata kama yeye si baba wa mtoto, kwa heshima nilitakiwa kumwambia kwani alibeba majukumu wakati baba wa mtoto kanitelekeza. Niliomba msamaha, yakamalizika, tukarudi kwenye hali nzuri.

Mtoto wangu amemaliza darasa la saba mwaka huu, na kuna shule mimi na baba yake tulipanga kumpeleka ili afanye usaili, ambayo ipo mkoani. Nilipoongea na mume wangu kumwambia kuwa tunataka kumpeleka mtoto, aliniambia hapendi hicho kitu, kwamba kama ni kumpeleka, nimpeleke mimi mwenyewe au baba yake ampeleke mwenyewe lakini si kuongozana kwenye gari moja mpaka mkoani, alikataa kabisa.

Nilijaribu kumuelewesha kuwa yule tumeshatengana naye, ni mzazi mwenza wangu tu, lakini hata hakujali. Aliniambia, "kama vipi nitakupeleka mimi, ila siwezi kukuruhusu kupanda gari moja na X wako." Nilimwambia hapana, yule ni baba yake mtoto na ana haki hivyo huwezi kunipangia. Aliniambia, "kama ukienda, ukirudi rudi huko huko." Mimi namjua mume wangu, ni mtu wa kunitishia-tishia kwani anahisi hajiamini, kwa kuwa huyo baba wa mtoto ana pesa zaidi, anaona kama ana hofu. Hivyo nilimwambia hapana.

Tulipanga na baba wa mtoto tukampeleka mtoto huko mkoani, nilimuaga lakini hakunijibu chochote. Nilienda na sikufanya chochote, hata usiku nilimpigia video call ili aone kuwa sipo chumba kimoja na huyo mwanaume, lakini hakupokea. Baada ya interview, nilirudi nyumbani ila kufika niliambiwa kuwa baba ameondoka. Nilimpigia simu kumtafuta, akaniambia "nimekuachia nyumba utakaa na watoto, mimi sidhani kama naweza kuendelea kuwa mume wako tena."

Sikufanya chochote, nilikaa kimya nikijua kuwa hasira zikiisha atarudi, lakini juzi nimepewa wito wa kuitwa Baraza la usuluhishi kwani mume wangu amefungua madai ya talaka. Kaka, sijui nifanye nini. Ndoa yangu bado naipenda, sina mahusiano na baba wa mtoto; nilimpeleka tu mtoto, nashindwa kuelewa kama huyu mwanaume ananipenda kweli au la. Sikulala na X wangu na nimemwambia aongee naye, lakini hataki kabisa. Naomba ushauri wako, kaka, sijui nifanye nini?

HUPANGIWI JIPANGIE MWENYEWE SASA

Mwanaume; Mwanamke hahitaji amani! ukiwa na busara sana huwezi kuishi na mwanamke hasa hawa Wakitanzania. Wanahitaji kashkash na kupigwa matukio ndiyo akili iwakae sawa!

Kama huyu atasimama kwenye mitandao na kusema wanaume wote ni mbwa!! Na atapata wafuasi
 
Ukweli wanawake ni wabinafsi sana; wanaume wana upendo hasa. Imagine una lea mtoto wa mwanaume mwenzio halafu mwanamke wako wala haoni kama kuna jambo lilikua linafanyika. Mwamba ana haki zote za kuomba muachane; wewe bado una uhusiano na X wako
Ngoja sasa mke wa X nae ajue kuwa kumbe wanapelekaga mtoto pamoja!
 
Kuna wanaume wazuri sana ila wanayokutana nayo ndo yanawabadilisha. Kila utendalo wewe dada, mama, mwanamke, binti...ni mbegu. Itazaa tu, iwe kilo moja au kilo mia maana mbegu zinatofautiana. God teach me how to fear you, kama moto upo kuna watu watakuwa kuni kwa staili hii. Kama ni story ya kweli pole kwa huyo kaka, tumemsikitikia wananzengo.
 
wadau huyu Dada tumshauri nn?
Mume wangu anataka kuniacha kwa kumpeleka Mtoto shule Mimi na X ambaye tulizaa kabla ya ndoa!

Mimi ni mama wa watoto 3. Mtoto wangu wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa kwenye mahusiano lakini alikuja kuoa mwanamke mwingine. Mwanzo mimi na yeye hatukuwa tunaongea kabisa kwani aliniacha vibaya, baadaye nilikutana na huyu mume wangu wa sasa. Katika mahusiano alikuwa ni mwanaume mzuri mpaka nikasahau kama nilishawahi kuumizwa.

Mpaka tunafunga ndoa, nilikuwa sifikirii kabisa kuhusu baba wa mtoto wangu, kwani huyu mume wangu alikuwa ananihudumia mimi na mwanangu kwa kila kitu. Kuna kipindi baba wa mtoto alirudi na kuomba msamaha, akasema anataka kuwa sehemu ya maisha ya mtoto na kulipa ada na mambo mengine.

Nilimkubalia na kwa kuwa ni mtoto wangu sikuona haja ya kuomba ruhusa kutoka kwa mume wangu, hivyo akaanza kulipa ada. Baadaye nililazimika kumwambia mume wangu kuwa ada inalipwa na baba yake mtoto, kwani kuna kipindi walilipa ada mara mbili shuleni.

Mume wangu alilipa ada ya mtoto bila kuniambia, wakati huo baba yake alikuwa tayari ameshalipa. Alikasirika kwa nini sikumwambia, lakini nilimwambia ni mwanangu na yule ni baba yake, hivyo ana haki zote. Tuliongea, yakasahaulika kwani watu waliniambia hata kama yeye si baba wa mtoto, kwa heshima nilitakiwa kumwambia kwani alibeba majukumu wakati baba wa mtoto kanitelekeza. Niliomba msamaha, yakamalizika, tukarudi kwenye hali nzuri.

Mtoto wangu amemaliza darasa la saba mwaka huu, na kuna shule mimi na baba yake tulipanga kumpeleka ili afanye usaili, ambayo ipo mkoani. Nilipoongea na mume wangu kumwambia kuwa tunataka kumpeleka mtoto, aliniambia hapendi hicho kitu, kwamba kama ni kumpeleka, nimpeleke mimi mwenyewe au baba yake ampeleke mwenyewe lakini si kuongozana kwenye gari moja mpaka mkoani, alikataa kabisa.

Nilijaribu kumuelewesha kuwa yule tumeshatengana naye, ni mzazi mwenza wangu tu, lakini hata hakujali. Aliniambia, "kama vipi nitakupeleka mimi, ila siwezi kukuruhusu kupanda gari moja na X wako." Nilimwambia hapana, yule ni baba yake mtoto na ana haki hivyo huwezi kunipangia. Aliniambia, "kama ukienda, ukirudi rudi huko huko." Mimi namjua mume wangu, ni mtu wa kunitishia-tishia kwani anahisi hajiamini, kwa kuwa huyo baba wa mtoto ana pesa zaidi, anaona kama ana hofu. Hivyo nilimwambia hapana.

Tulipanga na baba wa mtoto tukampeleka mtoto huko mkoani, nilimuaga lakini hakunijibu chochote. Nilienda na sikufanya chochote, hata usiku nilimpigia video call ili aone kuwa sipo chumba kimoja na huyo mwanaume, lakini hakupokea. Baada ya interview, nilirudi nyumbani ila kufika niliambiwa kuwa baba ameondoka. Nilimpigia simu kumtafuta, akaniambia "nimekuachia nyumba utakaa na watoto, mimi sidhani kama naweza kuendelea kuwa mume wako tena."

Sikufanya chochote, nilikaa kimya nikijua kuwa hasira zikiisha atarudi, lakini juzi nimepewa wito wa kuitwa Baraza la usuluhishi kwani mume wangu amefungua madai ya talaka. Kaka, sijui nifanye nini. Ndoa yangu bado naipenda, sina mahusiano na baba wa mtoto; nilimpeleka tu mtoto, nashindwa kuelewa kama huyu mwanaume ananipenda kweli au la. Sikulala na X wangu na nimemwambia aongee naye, lakini hataki kabisa. Naomba ushauri wako, kaka, sijui nifanye nini?

HUPANGIWI JIPANGIE MWENYEWE SASA

View: https://web.facebook.com/reel/473221525712495
 
Ngoja sasa mke wa X nae ajue kuwa kumbe wanapelekaga mtoto pamoja!
Ndio wanako elekea sasa though wanawake wasanii sana; kama huyo X ana hela, mkewe hatamuacha; watapigiana kelele za hapa na pale and finally usishangae mkewe akataka huyo mtoto achukuliwe ili wamlee wote. Ogopa sana hawa dada/mama zetu. Kila ushauri anaokupa, kuna HILA ndani yake
 
ubishi na ujuaji mwingi ni kitu mbaya sana. hakunaga baba wawili kwa mtoto moja.

hayupo mwanamue wa kukubali kufanyika kwa jambo hilo namna hiyo nyakati zilizopita na wala nyakati hizi.

Yaani kijana, alale pazuri, avishwe vizuri, apate matunzo na usalama wa kutosha tangu akiwa mchanga, kisha baba mwingine aje ajitokeze, aelekeze au ndio aje aamue ampeleke kijana shule gani? ni dharau sana hiyo.

kwa usalama wa ndoa yako ilifaa huyo kijana aende au umpeleke na atokomea huko kwa babake na asomeshwe huko huko.

there is no way uje useme eti humkufanya jambo lolote na mzazi mwenzio mlipokua mkimpeleka huko shule. Yes inawezekana hamkufanya jambo lolote , but Lazima mtakua mmezungumzia jambo hilo.

Na kwa nature ya binadamu ilivyo, Lazima ipo siku mtalifanya tu jambo hilo kwa kisingizio cha kumuhudumia mtoto..

hii iwe fundisho,
kwamba hakuna mwamaume anaependelea familia au ndoa yake iingiliwe na mwamaume mwingine kwa namna yoyote ile.

kwa kuhitimisha,
yote hayo umeyataka mwenyewe. Na huyo mwanaume asingeweza kuacha kuchukua hatua hizo 🐒
Umeeleza vizuri mno ila sijaelewa kwanini umemalizia na picha ya tumbili sijui ni nyani, au ndo huyo single mother?
 
Back
Top Bottom