Mume mmoja, wake Saba, umejiandaaje na ujio wa SHERIA hiyo ijayo duniani?

Mume mmoja, wake Saba, umejiandaaje na ujio wa SHERIA hiyo ijayo duniani?

Wake wengi aliooa Suleiman ndo sababu ya kumwondoa katika kumcha Mungu na kugeukia miungu.

Wanawake ndo walisababisha Suleiman pamoja na HEKIMA yote Alipewa, yupo kuzimu Hadi sasa tunavyoongea.
Maandiko yapi yanaonyesha kuwa Yuko kuzimu..?kama yeye alifanya uovu huo mbona uzao wake ukabarikiwa..??
 
Maandiko yapi yanaonyesha kuwa Yuko kuzimu..?kama yeye alifanya uovu huo mbona uzao wake ukabarikiwa..??
Mbinguni au kuzimu unaenda individual Si kikundi au Uzao.

Pia kuzimu ni HALISI, washukao huko humkuta.
 
Mkuu duniani wanaume ni wengi zaidi kuliko wanawake ujue
Sensa ya Tanzania, wanawake ni wengi zaidi ya wanaume.

Pia data za Dunia usiziamini sana,Kuna mambo wasingependa ufahamu.

Wanaume na uzao wa mtoto wa kiume unaviziwa upunguzwe na kupotezwa.

Tunza uanaume wako.
 
Alikuwa na wake wawili Ever na Lilith. Pia ADAMU siyo mtu pekee wa kwanza. Aliwakilisha wenzake ktk simulizi ya uumbaji. Waliumbwa binadamu wengi TU Kwa wakati moja. Ndo maana Kaini alipokimbia Toka nyumbani kule alikoenda alijitwalia Mke.
BIBLIA haijasema hivyo, huyo Lilith ni mafundisho ya Mashetani.
 
Watajitolea Mahari wenyewe. Watataka tu kuondolewa Aibu ya kutoolewa.

Hizo ni nyakati ngumu kwakweli.

Mwanaume ataishi kama ndege tu Hana Uchumi, Hana maamuzi, hakutakuwa na dira, Dunia itajiendea kama gari bovu!!
Hatar sana
 
Asili,

Mwanamke aliumbwa kukamilisha na Mwanaume.

Nenda kaangalie ofisi yenye wanawake 7 Mwanaume awe mmoja, hata kama ni mfagiaji uone alivyo na thamani.
Duuh kijana unaishi sayari ya wapi yenye hayo mambo, hivi kwanini wanaume mnatumia nguvu kubwa sana kuwaaminisha wanawake kwamba wao hawana thamani bila wanaume, kwanini msiache hiyo asili ifanye kazi yenyewe badala yake ni propaganda zenu tu ndio yanafanya kazi

Yani nafananisha na zile propaganda za watu weupe kuwaaminisha watu weusi kuwa ni wajinga na hatuwezi kujitawala ili tu waendelee kututawala, na kweli kwa sababu tuna viongozi wapumbavu basi wanatambaa na zile zile propaganda, yani like "si tulisema" wakati kiuhalisia ni wao ndio walijenga hiyo kitu kwa waafrika pale walipotutawala

Kifupi mnatakiwa muwaache wanawake wajitawale wenyewe bila kuwasimanga halafu muone, siyo mnajifanya mmewapa uhuru halafu mnazunguka mnakuja tena kuwatukana kuwa hawawezi, kuharibu kupo tu hata wanaume mmeiharibu hii dunia maana haijaanza kuharibika leo iliharibika tangu enzi za sodoma na gomora ambapo wanaume ndio walikuwa wanatawala
 
Hiyo ya wake saba iruhusu sisi wanawake tuchaguane…. Mbona mume wangu atakoma nitakavyowachukua mashosti zangu wa buza huko waje wawe wake wenzangu… tumkaushe maji, damu , na uroto
Itakapofikia Ratio ya ME 1:7 KE,

Huwezi kuchagua maana watakuwa adimu. Wa kutafuta Kwa tochi.
 
Cc kiranga njoo dhibitisha maneno ya jamaa yetu, cc mr pipa:mi naona ni uongo na kulishana upepo ukitaka kufa haraka we oa mwanamke mmoja afu broo suala la kiuchumi ni mtambuka aka mtambo wa panya ipo hv......naona unataka kubishia hebu sikiliza nikwambie
 
Duuh kijana unaishi sayari ya wapi yenye hayo mambo, hivi kwanini wanaume mnatumia nguvu kubwa sana kuwaaminisha wanawake kwamba wao hawana thamani bila wanaume, kwanini msiache hiyo asili ifanye kazi yenyewe badala yake ni propaganda zenu tu ndio yanafanya kazi

Yani nafananisha na zile propaganda za watu weupe kuwaaminisha watu weusi kuwa ni wajinga na hatuwezi kujitawala ili tu waendelee kututawala, na kweli kwa sababu tuna viongozi wapumbavu basi wanatambaa na zile zile propaganda, yani like "si tulisema" wakati kiuhalisia ni wao ndio walijenga hiyo kitu kwa waafrika pale walipotutawala

Kifupi mnatakiwa muwaache wanawake wajitawale wenyewe bila kuwasimanga halafu muone, siyo mnajifanya mmewapa uhuru halafu mnazunguka mnakuja tena kuwatukana kuwa hawawezi, kuharibu kupo tu hata wanaume mmeiharibu hii dunia maana haijaanza kuharibika leo iliharibika tangu enzi za sodoma na gomora ambapo wanaume ndio walikuwa wanatawala
Nimequote hiyo Isaya 4:1 katika andiko.

Hiyo Si propaganda, ni unabii, ni LAZIMA utimie Kwa muda wake
 
... Pamoja na kelele nyingi za kusema kuwa namba ya wanawake ni kubwa kuzidi namba ya wanaume, lakini ukweli unabaki kuwa kwamba kuna balance, kwa asilimia kubwa tu, kati ya wingi wa wanawake na wanaume!

... KINACHOENDA KUIFANYA DUNIA YETU MZINGA WA NYUKI, WENYE MALKIA NA MADUME TEULE WACHACHE, NI KUPUNGUA KWA NGUVU ZA KIUCHUMI KWA WANAUME!

NA KASI INAONGEZWA ZAIDI NA MFUMKO WA UMATI UNAOFANYA HATA HAJA YA KUZAANA KWA KASI IPUNGUE!
MUNGU MTAALAM!
 
Kwanza kabisa kuhusu hilo andiko wengi huwa mnalitafsiri vibaya kwa kuchukua huo mstari mmoja tu, kwa kukusaidia kasome kwanza
Wewe ni Nabii ubishane na unabii bila ufunuo?
 
Hiyo sheria imeanza kutungwa wapi?

Wapi rejea?

Yes biblia imeandika lakini haijasema itatungwa sheria bali wanawake wayajipeleka kwa hiari kuliwa.
 
Unaandikaga uharo sana.

Hiyo sheria imeanza kutungwa wapi?
Wapi?
Wapi rejea?
Yes biblia imeandika lkn haijasema itatungwa sheria bali wanawake wayajipeleka kwa hiari kuliwa
Rudia kusoma tena na tena.

Soma Hadi mwisho, neno Kwa neno kifungu Kwa kifungu, Aya Kwa Aya.

Pia matumizi ya lugha chafu ni kipimo Cha mtu mwoga asiye makini.

Karibu.
 
Salaam, Shalom!!!

(Isaya 4:1)

NA SIKU HIYO, WANAWAKE SABA WATAMSHIKA MTU MUME MMOJA WAKISEMA, TUTAKULA CHAKULA CHETU, NA KUVAA NGUO ZETU WENYEWE, LAKINI TUITWE TU KWA JINA LAKO, UTUONDOLEE AIBU YETU.

Maneno ya unabii huo yanakwenda kutimia, inakwenda kutungwa SHERIA kabisa kuruhusu wanawake wengi Kuolewa na mwanamume mmoja.

Tangu 2021, Dunia iliingia msimu mpya, yapo mengi sana yanakwenda kubadilika, hivyo kuleta mgawanyiko wa watu katika makundi mawili makubwa,

Kundi moja, litakuwa wanaomcha Mungu, na kundi la pili, kundi la waovu.


KWANINI WAKE SABA MUME MMOJA?

1. Idadi ya wanaume waoaji imepungua na ITAENDELEA kupungua sana. Maisha magumu na misongo ya mawazo inakwenda kupunguza sana wanaume na uzao wa watoto wa kiume.

2. Mifumo ya kidunia inazidi kuwainua wanawake na kiwashusha chini wanaume Ili kuipindua juu chini Dunia iende kinyume na mapenzi ya Mungu. Mungu aliagiza mume mmoja aoe mke mmoja. Mwanaume awe KICHWA, kiongozi, nw MAPINDUZI yameendekea kukua na kumwachia Mwanaume akitaabika.

3. USHOGA, usagaji na vitendo vya kubadili JINSIA,ni mambo ambayo ya akwenda kupunguza sana idadi ya wanaume duniani.

4. Magonjwa, vita na vifo vitapunguza sana idadi ya wanaume duniani na kuwafanya wawe bidhaa adimu.

5. Nchi nyingi walitunga sera za kupanga uzazi ambazo zimeondoa nguvu KAZI Kwa kiasi kikubwa, na tunakoelekea, Africa itastawi sana kiuchumi sababu ya kutofuata sera hizo.

Yote hayo hapo juu, yanakwenda kutimiza unabii huo.

Wanaume, watakosa nguvu ya kiuchumi na kutawaliwa na wanawake, Nchi zilizoendelea, Hadi tunavyoongea Mwanaume tayari ni mtumwa wa mwanamke.


LINI UNABII HUO UTATIMIA?

Kwa kuanza, mwaka huu 2024- 2030, zitatungwa SHERIA za kuruhusu wanawake kuruhusiwa Kuolewa na mwanamume mmoja, na itakuwa SHERIA kabisa.

HITIMISHO.

Imeandikwa, mwovu na azidi kuwa mwovu, na mtakatifu na azidi kujitakasa. Tunaelekea katika nyakati ngumu na za taabu sana ULIMWENGUNI.

Uyaonapo haya Kutokea, jua kuwa Yesu Yu karibu kurudi. Chagua kuwa moto au baridi.

Ikiwa hujaokoka, fuatisha Sala hii;

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN
Nimesikia huko eritrea ni sheria lazima uwe na mke zaidi ya mmoja, sina uhakaika na hilo.
 
Back
Top Bottom