Mume mmoja, wake Saba, umejiandaaje na ujio wa SHERIA hiyo ijayo duniani?

Wake wengi aliooa Suleiman ndo sababu ya kumwondoa katika kumcha Mungu na kugeukia miungu.

Wanawake ndo walisababisha Suleiman pamoja na HEKIMA yote Alipewa, yupo kuzimu Hadi sasa tunavyoongea.
Maandiko yapi yanaonyesha kuwa Yuko kuzimu..?kama yeye alifanya uovu huo mbona uzao wake ukabarikiwa..??
 
Maandiko yapi yanaonyesha kuwa Yuko kuzimu..?kama yeye alifanya uovu huo mbona uzao wake ukabarikiwa..??
Mbinguni au kuzimu unaenda individual Si kikundi au Uzao.

Pia kuzimu ni HALISI, washukao huko humkuta.
 
Mkuu duniani wanaume ni wengi zaidi kuliko wanawake ujue
Sensa ya Tanzania, wanawake ni wengi zaidi ya wanaume.

Pia data za Dunia usiziamini sana,Kuna mambo wasingependa ufahamu.

Wanaume na uzao wa mtoto wa kiume unaviziwa upunguzwe na kupotezwa.

Tunza uanaume wako.
 
Alikuwa na wake wawili Ever na Lilith. Pia ADAMU siyo mtu pekee wa kwanza. Aliwakilisha wenzake ktk simulizi ya uumbaji. Waliumbwa binadamu wengi TU Kwa wakati moja. Ndo maana Kaini alipokimbia Toka nyumbani kule alikoenda alijitwalia Mke.
BIBLIA haijasema hivyo, huyo Lilith ni mafundisho ya Mashetani.
 
Watajitolea Mahari wenyewe. Watataka tu kuondolewa Aibu ya kutoolewa.

Hizo ni nyakati ngumu kwakweli.

Mwanaume ataishi kama ndege tu Hana Uchumi, Hana maamuzi, hakutakuwa na dira, Dunia itajiendea kama gari bovu!!
Hatar sana
 
Asili,

Mwanamke aliumbwa kukamilisha na Mwanaume.

Nenda kaangalie ofisi yenye wanawake 7 Mwanaume awe mmoja, hata kama ni mfagiaji uone alivyo na thamani.
Duuh kijana unaishi sayari ya wapi yenye hayo mambo, hivi kwanini wanaume mnatumia nguvu kubwa sana kuwaaminisha wanawake kwamba wao hawana thamani bila wanaume, kwanini msiache hiyo asili ifanye kazi yenyewe badala yake ni propaganda zenu tu ndio yanafanya kazi

Yani nafananisha na zile propaganda za watu weupe kuwaaminisha watu weusi kuwa ni wajinga na hatuwezi kujitawala ili tu waendelee kututawala, na kweli kwa sababu tuna viongozi wapumbavu basi wanatambaa na zile zile propaganda, yani like "si tulisema" wakati kiuhalisia ni wao ndio walijenga hiyo kitu kwa waafrika pale walipotutawala

Kifupi mnatakiwa muwaache wanawake wajitawale wenyewe bila kuwasimanga halafu muone, siyo mnajifanya mmewapa uhuru halafu mnazunguka mnakuja tena kuwatukana kuwa hawawezi, kuharibu kupo tu hata wanaume mmeiharibu hii dunia maana haijaanza kuharibika leo iliharibika tangu enzi za sodoma na gomora ambapo wanaume ndio walikuwa wanatawala
 
Hiyo ya wake saba iruhusu sisi wanawake tuchaguane…. Mbona mume wangu atakoma nitakavyowachukua mashosti zangu wa buza huko waje wawe wake wenzangu… tumkaushe maji, damu , na uroto
Itakapofikia Ratio ya ME 1:7 KE,

Huwezi kuchagua maana watakuwa adimu. Wa kutafuta Kwa tochi.
 
Cc kiranga njoo dhibitisha maneno ya jamaa yetu, cc mr pipa:mi naona ni uongo na kulishana upepo ukitaka kufa haraka we oa mwanamke mmoja afu broo suala la kiuchumi ni mtambuka aka mtambo wa panya ipo hv......naona unataka kubishia hebu sikiliza nikwambie
 
Nimequote hiyo Isaya 4:1 katika andiko.

Hiyo Si propaganda, ni unabii, ni LAZIMA utimie Kwa muda wake
 
... Pamoja na kelele nyingi za kusema kuwa namba ya wanawake ni kubwa kuzidi namba ya wanaume, lakini ukweli unabaki kuwa kwamba kuna balance, kwa asilimia kubwa tu, kati ya wingi wa wanawake na wanaume!

... KINACHOENDA KUIFANYA DUNIA YETU MZINGA WA NYUKI, WENYE MALKIA NA MADUME TEULE WACHACHE, NI KUPUNGUA KWA NGUVU ZA KIUCHUMI KWA WANAUME!

NA KASI INAONGEZWA ZAIDI NA MFUMKO WA UMATI UNAOFANYA HATA HAJA YA KUZAANA KWA KASI IPUNGUE!
MUNGU MTAALAM!
 
Kwanza kabisa kuhusu hilo andiko wengi huwa mnalitafsiri vibaya kwa kuchukua huo mstari mmoja tu, kwa kukusaidia kasome kwanza
Wewe ni Nabii ubishane na unabii bila ufunuo?
 
Hiyo sheria imeanza kutungwa wapi?

Wapi rejea?

Yes biblia imeandika lakini haijasema itatungwa sheria bali wanawake wayajipeleka kwa hiari kuliwa.
 
Unaandikaga uharo sana.

Hiyo sheria imeanza kutungwa wapi?
Wapi?
Wapi rejea?
Yes biblia imeandika lkn haijasema itatungwa sheria bali wanawake wayajipeleka kwa hiari kuliwa
Rudia kusoma tena na tena.

Soma Hadi mwisho, neno Kwa neno kifungu Kwa kifungu, Aya Kwa Aya.

Pia matumizi ya lugha chafu ni kipimo Cha mtu mwoga asiye makini.

Karibu.
 
Nimesikia huko eritrea ni sheria lazima uwe na mke zaidi ya mmoja, sina uhakaika na hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…