Patra31
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 6,918
- 13,885
Marko 10 :4-12Hebu lete ilo andiko linalosema mke ni mmoja tu ktk biblia
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.
⁵ Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
⁶ Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
⁷ Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
⁸ na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
⁹ Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
¹⁰ Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.
¹¹ Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;
¹² na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.
1 Wakorintho 7:1-3
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
² Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
³ Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
Mwanzo 2:24, Mathayo 19, waefeso 5:31.
Wajuzi zaid watakuja kuelezea zaidi