HakiKwanza_2015
JF-Expert Member
- Nov 16, 2022
- 381
- 557
- Thread starter
-
- #81
Yes na hakuonesha kukerwa.Sawa naomba kukuliza hili swali. Kabla ya kumleta binti, hapo nyumbani Je ulishauriana na mume wako? Alikubali? Ama ulifanya maamuzi mwenyewe ya kumleta bila kumshirikisha mumeo?
Asipate shida ya kumpangia chumba mm naishi hapa jirani na chuo cha huyo binti.Dar Kuna vyumba Hadi vya 10000,mdogo ongea na wazazi wako akae hostel au mpangishieni chumba ,amalize chuo
Mwanamke kutongozwa Ni sunna,na haiepukiki,maamuzi yanakua kwake akubali au akatae,ata umlinde vipi Kama wakuliwa ataliwa tuNamuonea huruma kupanga na mimi sina uwezo wa kumpangia, hana kazi si ndo naenda kumuacha aingie kwenye mtego wa mababa wa mjini, ni mzuri so kusumbuliwa lazima ila akiwa chini yangu nammudu nimemwekea hadi mda wa kurudi. Hata kama anaenda sehemu lazima aage kwangu na kwa shemeji yake. Kama wametongozana nikijua ntapata busara kutokea hapo. Acha Mungu anioneshe najipunguzia stress za kuwaza hayo
Unachokitaka kamwe hutakipata.Kweli kila binadamu ana mapungufu hata yeye mume wangu ukimuuliza atasema mke wangu ana moja mbili tatu. Lakini kilichonileta hapa sio mapungufu ya mume wangu nnachotamani ni kujua au kuelewa nifanyeje ili amuone mdogo wangu kama mwanae.
Haitokua sawa kama akimfanyia mdogo wangu ubaya kwa kuwa mimi ni mbaya japo huwa napenda sana kumuuliza mume wangu kama kuna lolote nimemkosea nirekebishe. So asiposema naona naenda sawa tu
Ikishindikana mtaftie hostels karibu na chuo as long as home wanamudu kulipia hizo huduma haina shida.Umeongea vyema sana kaka angu. Ntatafuta tena neno lenye busara nimwambie kwamba huyu ni mtoto. Amlee tu kama mwanae
Dah. Nimeusoma huu ujumbe kwa maumivu sana. Yani unawekwa katika wakati mgumu wa kuamua kati ya ndoa na ndugu yako wa damu mliopitia matatizo na kuyavuka pamoja. Hivi ikatokea siku mume amekuacha, kwa ndugu yako unarudije sasa kupata msaada na mnakua msha hitilafianaPole sana dear,nimekuelewa
Unakumbuka ulipoolewa uliambiwa ndoa ni uvumilivu?Basi maana yake ni hiyo sasa,uliambiwa unaishi na binadamu na si malaika basi binadamu mwenyewe ndo huyo sasa!
Kwanza kubali kuwa umeolewa na mwanaume mchoyo na mbinafsi na ndo mana wakija ndugu zako anasema hana ela ila wakija ndugu anatoa,hizo ni tabia za ubinafsi!
Kama mwanamke nilie kwenye ndoa nakushauri umtoe huyo mdogo wako hapo as umesema kwenu una uwezo wa kumlipia hostel,usitake kuforce kukaa nae though umesema unampenda mana utaumia tena sana tu huko mbele kadri siku zinavyozidi kwenda na hata huo upendo unaosema unauona kwa mumeo hutauona tena!
Kumbuka kuna kuchoka as wewe pia ni binadamu,na maudhi na maumivu ndo husababisha ndoa nyingi leo kuwa ndoa jina au kusambaratika kabisa!
Mwache aende alafu wewe endelea kumuombea kwa Mungu aguse moyo wake mana uchoyo ni dhambi!
Kuna vitu unaweza kuvumilia kirahisi kwenye ndoa ila sio kuona mwenzio hataki ndugu zako,yani unajiona hata wewe huna thamani kwake ndo mana nakwambia mtoe kwanza huyo hapo ili usijitengenezee maumivu yasiyo ya lazima!
Once again pole sana,
Sasa wewe ni mwanaume. Kumtupa mtoto huko si ntakua katili na kikubwa ntampa tu stress bi mkubwa maana stress za wanae zote huwa ananimwagia mimi nizisort so hawa ni wanguIkishindikana mtaftie hostels karibu na chuo as long as home wanamudu kulipia hizo huduma haina shida.
Mie nina shemeji yangu mmoja ndio ana michongo hio alijaribu kumtwist cousin sis wangu awe kama ananichukia ila niliposanuka nikahama home kwao. Ilikuwa wakati wa chuo hivyo hivyo nikaenda kupanga kwangu nashukuru na mke nilimpata huko huko.
Sasa mtu kudai mashuka ambayo nimempa mdogo wangu alalie anasema abaki na pair moja nayo ni kujiona victim. Hata mimi nilidhani hivyo lakini kuna matukio naona kabisa ni changamoto na wala sii u victim.Shida imeanzia pale, kutokuwa na mahusiano mazuri sana na baba yenu. Kisaikolojia wote mmevaa vazi la victim wewe na wadogo zako, hvyo hakuna mwanaume yeyote mtamwona ni mzuri kwenu kwa sasa include mmeo. Zaidi kila kitu atakachoongea mme wako utaona ni manyanyaso tu mnanyanyaswa, sometimes labda anaongea kikawaida tu, ila litakuzwa hilo jambo katika sura ya manyanyaso.... nazifahamu hz mambo,.. Anza wewe kuitoa hyo conflict kwanz ndan yako dhidi ya Baba Mzazi.. Utanishkuru
Dah. Nimeusoma huu ujumbe kwa maumivu sana. Yani unawekwa katika wakati mgumu wa kuamua kati ya ndoa na ndugu yako wa damu mliopitia matatizo na kuyavuka pamoja. Hivi ikatokea siku mume amekuacha, kwa ndugu yako unarudije sasa kupata msaada na mnakua msha hitilafiana
Ndoa bado changa ila watapatikana tuWewe na mume wako mmebahatika kupata watoto?
Ukisema nahamishia ndugu ni wangapi sasa, ungekua mume na una ndugu anatakiwa kuja kukaa hapa ningesema maneno haya ungeniona wa kawaida? Kiafrika utaepuka kusaidia ndugu hata mmoja? Maana sijawahamishia wengine. Wengine wanakaa hostel na hapa hata hawaji.Nimesoma maelezo
Nimejaribu kusoma na kukusoma wewe nimegundua wewe ni aina ya watu wanaopenda kujenga himaya ya undugu zaidi walipoolewa.
Jambo hili sio jema.
Jitahidi muwe na mahusiano mazuri pande zote lakini usihamishie ndg zako kwako utaivunja ndoa hivi hivi.
Hapa umejitahidi sana kuuonyesha udhaifu wa mume zaidi lkn mdhaifu zaidi ni wewe.
Si kila jema ulitendalo ni JEMA...laweza kuwa uharibifu kwasababu unapolifanyia sio sehemu sahihi.
Facts 😁😁😁😁😁Pole sn mkuu. Hilo ni tatizo tena ni kubwa sana.
Nakushauri mtoe mdogo wake mrudishe nyumbani.
Pengine mumeo anaomba kugegeda mdogo wako.
Lakini ni ngumu kukueleza sababu ya kuvunja ndoa yako.Hapo Kuna jambo. Chukuwa hatua.
Mkuu, mume wako ana roho masikini…period!Ukisema hanipendi nanyong’onyea maana ananijali yani kuna vitu ananifanyia naridhika so nikimuhukumu kwa hili ntakua nakosea. Roho ya kimaskini siwezi Kupinga ila naikemea tu kwa jina la Muumba. Na ntafanyeje sasa ndo mume wangu wa ndoa
Asante kwa ushauri. Nishamwambia mara nyingi niambieMkuu, mume wako ana roho masikini…period!
Si ajabu kukutana na watu wenye roho masikini, cha msingi na kama unampenda mumeo, ni jukumu lako kumfundisha kuwa na roho tajiri kama vile ulivomfundisha some manners za maisha!
Wewe kama wewe huwezi jitenga na ndugu zako na Pia mkumbushe alipokuoa hakukukuta unaishi mwenyewe bila ndugu.
Una maneno mengi huwezi kushaurika zaidi kuna vitu unataka usapotiwe uhalalishe mawazo yako.Ukisema nahamishia ndugu ni wangapi sasa, ungekua mume na una ndugu anatakiwa kuja kukaa hapa ningesema maneno haya ungeniona wa kawaida? Kiafrika utaepuka kusaidia ndugu hata mmoja? Maana sijawahamishia wengine. Wengine wanakaa hostel na hapa hata hawaji.
Kwenye comment nyingi nimeshaelezea sana kuhusu mapungufu. Wala sijaja kumuongelea mume mapungufu yake nimeleta hilo tu niombe ushauri kwa wenye ndoa zenye miaka mingi wameishije.
Kingine nishaurini mtaishi peke yenu miaka mingapi na hao watoto mnawaleaje kwa maisha haya ya kiafrika?