Pole sana dear,nimekuelewa
Unakumbuka ulipoolewa uliambiwa ndoa ni uvumilivu?Basi maana yake ni hiyo sasa,uliambiwa unaishi na binadamu na si malaika basi binadamu mwenyewe ndo huyo sasa!
Kwanza kubali kuwa umeolewa na mwanaume mchoyo na mbinafsi na ndo mana wakija ndugu zako anasema hana ela ila wakija ndugu anatoa,hizo ni tabia za ubinafsi!
Kama mwanamke nilie kwenye ndoa nakushauri umtoe huyo mdogo wako hapo as umesema kwenu una uwezo wa kumlipia hostel,usitake kuforce kukaa nae though umesema unampenda mana utaumia tena sana tu huko mbele kadri siku zinavyozidi kwenda na hata huo upendo unaosema unauona kwa mumeo hutauona tena!
Kumbuka kuna kuchoka as wewe pia ni binadamu,na maudhi na maumivu ndo husababisha ndoa nyingi leo kuwa ndoa jina au kusambaratika kabisa!
Mwache aende alafu wewe endelea kumuombea kwa Mungu aguse moyo wake mana uchoyo ni dhambi!
Kuna vitu unaweza kuvumilia kirahisi kwenye ndoa ila sio kuona mwenzio hataki ndugu zako,yani unajiona hata wewe huna thamani kwake ndo mana nakwambia mtoe kwanza huyo hapo ili usijitengenezee maumivu yasiyo ya lazima!
Once again pole sana,