Mungu alitumia na anatumia nguvu nyingi sana kupambana na Ibilisi ila anafeli

Mungu alitumia na anatumia nguvu nyingi sana kupambana na Ibilisi ila anafeli

GRAMAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,241
Reaction score
3,800
Kuna mambo mengine yanafikilisha sana, kuna movement kibao zimeanzishwa ili kumpiga vita Ibilisi ila cha kushangaza Ibilisi huyo bado yupo na anadunda vizuri tu.

Ukiangalia movement ambazo Mungu ameanzisha ili aweze kujitangaza na kumpiga vita Ibilisi ni nyingi sana ukilinganisha na zile ambazo Ibilisi anazitumia kujitangaza na kumpiga vita Mungu.

Mungu alishafanya kafara nyingi sana ili aweze kupambana na Ibilisi lakini wapi Ibilisi bado anadunda tu. Mfano ilifikia hatua Mungu aliteketeza watu wa Nuhu na aliteketeza watu wa Sodoma na Gomora ili liwe fundisho kwa watu wengine ili waachane na Ibilisi ila mission ilifeli vibaya sana ndio kwanza Ibilisi anazidi kupeta tu.

Mitume kibao wameletwa ili wapambane na Ibilisi ila hakuna hata mmoja aliyefanikiwa wote walifeli vibaya sana na Ibilisi bado anadunda vizuri tu.

Mungu alishatuma vitabu kibao vije duniani kupambana na Ibilisi. Mfano wa vitabu nivyo ni:-
i/The Bible kwa wakristo
ii/The Vedas,The Upanishads, The Mahabharata na The Ramayana kwa Hinduism.
iii/ The Qur'an kwa waislam.
iv/ The Jaina Sutras kwa Jainism
v/ The Law and The Prophets, The Psalms na The Talmud kwa Judaism.
vi/The Katab-l-Aqdas, na The Katab-l-Iqan kwa Baha'i Faith.
vii/The Kojiki na The Nihongi kwa washinto.
viii/The Shri Guru Granth Sahib kwa Sikhism.
ix/ The Toa-te-Ching kwa Taoism.
x The Zend Avesta na Pahlavi Text kwa Zoroastrianism.

Pamoja na vitabu vyote hivi vinavyompinga Ibilisi (evils) katika kila jamii lakini bado Ibilisi yupo na anadunda tu.

Mpaka mwisho wa siku Mungu akaamua kuja yeye mwenyewe dunia kwa umbo la binadami kuja kupambana na Ibilisi kilichompata nadhani tunakijua. Aliishia kutundikwa msarabani na kufa palepale. Na ikabidi waibuke watetezi na kusema yule hakuwa yeye bali ni mwanae na watetezi wengine wakasema alifufuka siku ya tatu na akapaa ipo siku atarudi.

Mission zote na harakati zote zilizoletwa na Mungu kwa lengo la kupambana na Ibilisi zilifeli totally. Hakuna hata moja iliyofanikiwa ndio maana mpaka leo Ibilisi yupo na anadunda vizuri tu.

Sasa sijui hali ingekuwaje kwa Mungu kama na Ibilisi nayeye angeamua kuwekeza kwa namna hii ili apambane na Mungu?

Ibilisi anapata wapi nguvu hizo za kupambana na na Mungu kwa kiasi hicho?

Daaah kuna Mungu na Ibilisi kweli?

Au ndiyo tuamini kwamba washauri wa Mungu (Malaika) hawamshauri vizuri namna gani ya kupambana na Ibilisi?
 
Mungu ni timeless, alikuepo kabla hajaumba muda, zama au nyakati. Hana pupa wala haraka, anajua mwisho kila kitu kipo katika umiliki wake.



Shet'ani atasema baada ya kutolewa hukumu "Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu." Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu.

Quran; Surah Ibrahim (14): Ayah 22.
 
Kwani watu wengi duniani wanaendeshwa Na Mungu au shetani?

Mfano nyimbo Za gospel Na Za bongo fleva zipi zinabamba?
Kuzini Na kuoa kipi kinabamba?
Meza ya bwana Na Meza ya pombe ipi inabamba?
Tunajua tumetokana na Mungu ila ulimwengu mzima unatawaliwa na yule mwovu shetani 1 yohana 5:19
 
Kwahyo Kwa juhudi zote Hizo Mungu ameshindwa kutawala ulimwengu aliouumba? Sad
Nisikilizeni ninyi mlio na moyo mkaidi, ninyi mlio mbali sana na uadilifu.
Nimeuleta karibu uadilifu wangu, hauko mbali sana *na wokovu wangu hautakawia. Isaya 46:12
 
Kuna siku nilikua nipo kwenye kikao cha mirathi (wote waislamu) sasa kuna vipengele vikaleta ugumu kidogo

1. Mtoto wa kiume kupata zaidi ya mtoto wa kike
2. Mtoto wa nje ya ndoa kutopewa urithi
3. Mjukuu asipate urithi kwa sababu mzazi wake alikimbia mirathi ( mzazi wa mjukuu alikufa kabla ya babu)

Sasa kwa sababu kwenye familia kulikua na watoto ambao baadhi yao hivyo vipengele hapo juu vinawabana na vikifuatwa baadhi hawatopata kabisa mirathi,mgogoro ukaanza.

Njia pekee ya kuleta amani ilikua ni kuachana na sheria za dini.

Hivyo dini ikawekwa pembeni watu wakagawana sawa kwa sawa na amani ikawepo .

Hapo ndipo nilipogundua hizi dini tunalazimishwa tu lkn wakati mwingine hatuzihitaji.

Je hapo napo shetani alishinda?[emoji2297]
 
Back
Top Bottom