Mungu alitumia na anatumia nguvu nyingi sana kupambana na Ibilisi ila anafeli

Mungu alitumia na anatumia nguvu nyingi sana kupambana na Ibilisi ila anafeli

Siku zote tunawaambia humu habari za Mungu na Shetani ni fictional characters waliotungwa na wajinga wa kale na hazina nafasi katika Dunia ya Kisasa hawaelewi
Ona jinsi watakavyoishiwa hoja kukujibu mtoa mada
Hasa hasa wenye kilanga ni wafuasi wa Mungu
Hua wanatia huruma Sana kumtetea ingali Shetani hua hatetewi ila Kazi zake hua zinadhihirika wazi Bila jasho
Mifano mnayo wadau!
😁😁😁😁😁🔥
 
Siku zote tunawaambia humu habari za Mungu na Shetani ni fictional characters waliotungwa na wajinga wa kale na hazina nafasi katika Dunia ya Kisasa hawaelewi
Ona jinsi watakavyoishiwa hoja kukujibu mtoa mada
Hasa hasa wenye kilanga ni wafuasi wa Mungu
Hua wanatia huruma Sana kumtetea ingali Shetani hua hatetewi ila Kazi zake hua zinadhihirika wazi Bila jasho
Mifano mnayo wadau!
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji91]

pumba, nawe uko jamii intelligence
 
Mungu amemuacha dhaifu(Shetani) atambe. Wamegawana vipindi. Shetani anashinda Ulimwenguni, anakura hasara Mbinguni(Ulimwengu ujao). Mungu anatoa Sare Ulimwenguni, anakabidhi ushindi Mbinguni. Mungu ndiye anaeruhusu huo ushindi unaouona kwa shetani hapa duniani.
 
Kuna mambo mengine yanafikilisha sana, kuna movement kibao zimeanzishwa ili kumpiga vita Ibilisi ila cha kushangaza Ibilisi huyo bado yupo na anadunda vizuri tu.

Ukiangalia movement ambazo Mungu ameanzisha ili aweze kujitangaza na kumpiga vita Ibilisi ni nyingi sana ukilinganisha na zile ambazo Ibilisi anazitumia kujitangaza na kumpiga vita Mungu.

Mungu alishafanya kafara nyingi sana ili aweze kupambana na Ibilisi lakini wapi Ibilisi bado anadunda tu. Mfano ilifikia hatua Mungu aliteketeza watu wa Nuhu na aliteketeza watu wa Sodoma na Gomora ili liwe fundisho kwa watu wengine ili waachane na Ibilisi ila mission ilifeli vibaya sana ndio kwanza Ibilisi anazidi kupeta tu.

Mitume kibao wameletwa ili wapambane na Ibilisi ila hakuna hata mmoja aliyefanikiwa wote walifeli vibaya sana na Ibilisi bado anadunda vizuri tu.

Mungu alishatuma vitabu kibao vije duniani kupambana na Ibilisi. Mfano wa vitabu nivyo ni:-
i/The Bible kwa wakristo
ii/The Vedas,The Upanishads, The Mahabharata na The Ramayana kwa Hinduism.
iii/ The Qur'an kwa waislam.
iv/ The Jaina Sutras kwa Jainism
v/ The Law and The Prophets, The Psalms na The Talmud kwa Judaism.
vi/The Katab-l-Aqdas, na The Katab-l-Iqan kwa Baha'i Faith.
vii/The Kojiki na The Nihongi kwa washinto.
viii/The Shri Guru Granth Sahib kwa Sikhism.
ix/ The Toa-te-Ching kwa Taoism.
x The Zend Avesta na Pahlavi Text kwa Zoroastrianism.

Pamoja na vitabu vyote hivi vinavyompinga Ibilisi (evils) katika kila jamii lakini bado Ibilisi yupo na anadunda tu.

Mpaka mwisho wa siku Mungu akaamua kuja yeye mwenyewe dunia kwa umbo la binadami kuja kupambana na Ibilisi kilichompata nadhani tunakijua. Aliishia kutundikwa msarabani na kufa palepale. Na ikabidi waibuke watetezi na kusema yule hakuwa yeye bali ni mwanae na watetezi wengine wakasema alifufuka siku ya tatu na akapaa ipo siku atarudi.

Mission zote na harakati zote zilizoletwa na Mungu kwa lengo la kupambana na Ibilisi zilifeli totally. Hakuna hata moja iliyofanikiwa ndio maana mpaka leo Ibilisi yupo na anadunda vizuri tu.

Sasa sijui hali ingekuwaje kwa Mungu kama na Ibilisi nayeye angeamua kuwekeza kwa namna hii ili apambane na Mungu?

Ibilisi anapata wapi nguvu hizo za kupambana na na Mungu kwa kiasi hicho?

Daaah kuna Mungu na Ibilisi kweli?

Au ndiyo tuamini kwamba washauri wa Mungu (Malaika) hawamshauri vizuri namna gani ya kupambana na Ibilisi?

Hi nchi uhuru umezidi sasa.
 
Kuna siku nilikua nipo kwenye kikao cha mirathi (wote waislamu) sasa kuna vipengele vikaleta ugumu kidogo

1. Mtoto wa kiume kupata zaidi ya mtoto wa kike
2. Mtoto wa nje ya ndoa kutopewa urithi
3. Mjukuu asipate urithi kwa sababu mzazi wake alikimbia mirathi ( mzazi wa mjukuu alikufa kabla ya babu)

Sasa kwa sababu kwenye familia kulikua na watoto ambao baadhi yao hivyo vipengele hapo juu vinawabana na vikifuatwa baadhi hawatopata kabisa mirathi,mgogoro ukaanza.

Njia pekee ya kuleta amani ilikua ni kuachana na sheria za dini.

Hivyo dini ikawekwa pembeni watu wakagawana sawa kwa sawa na amani ikawepo .

Hapo ndipo nilipogundua hizi dini tunalazimishwa tu lkn wakati mwingine hatuzihitaji.

Je hapo napo shetani alishinda?[emoji2297]
Aisee
 
Cha kushangaza mungu vs shetani tangu nmezaliwa sikuwahi kuwasikia wakisema woote wanasemewa tu..
Ujinga mzigo wa kuni yaaniiiiiii mtu unatishwa na maandishi,maandishi jaman enheeee.
 
Acha wanaoamini waende njia yao , na wasiyoamini pia waende njia yao. Tunacheleweshana sana, kwa kila mtu kujiona ni bora sana.
 
Back
Top Bottom