Mungu amekataza wanaume kuvaa kofia wanaposali. Kwanini wanaume hawa wanakaidi agizo la Mungu?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Je, ni sahihi kwa mwanaume kuvaa kofia au kufunika kichwa chake anapokuwa katika ibada? Biblia inalo jibu la wazi kabisa.

Katika 1 Wakorintho 11:4, Mtume Paulo anaandika:
“Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake... Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu...”

Hili ni agizo dhahiri kutoka kwa Mungu. Neno hili halipaswi kupuuzwa wala kubadilishwa kwa kufuata mapokeo, utamaduni au mitazamo ya kisasa.

Kwa mujibu wa andiko hili(1 Wakorintho 11:7), mwanaume asalipo, anapokuwa katika ibada, au anapohubiri, akifunika kichwa anamvunjia heshima Yesu Kristo, ambaye ni kichwa chake. Mwanaume anapaswa kuonyesha heshima ya kiroho mbele ya Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo - kwa kutokufunika kichwa. Agizo hili ni kwa wanaume wote. Hata Papa agizo hili linamhusu. Hata Maaskofu na Mapadre, agizo hilo linawahusu, kwa kuwa na wao ni wanaume.

Anayepinga aweke hapa hoja za kimaandiko.
 
Mungu amekataza wanaume kuvaa kofia wanaposali. Kwanini wanaume hawa wanakaidi agizo la Mungu?
Kofia1.png
Kofia2.png
Kofia3.png
 
Wanaume, lichukulieni jambo hili kwa uzito, kama ishara ya kumheshimu Mungu aliye Mkuu.

Vinginevyo siku ile ya mwisho kuna hatari ya kuambiwa:
“Siwajui ninyi, wala mtokako. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!" (Luka 13:27).

Luka 6:46-49
"Kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, lakini hamyatendi nisemayo?"
 
Mbona umeruka kuhusu wanawake kufunika vichwa/nywele zao?

1 Wakorintho 11:4-6
4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.

5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.

6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
 
Hiyo ni mada nyingine. Kwa leo nimeongea na wanaume tu.
 
Je, ni sahihi kwa mwanaume kuvaa kofia au kufunika kichwa chake anapokuwa katika ibada? Biblia inalo jibu la wazi kabisa.

Katika 1 Wakorintho 11:4, Mtume Paulo anaandika:
“Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake... Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu...”

Hili ni agizo dhahiri kutoka kwa Mungu. Neno hili halipaswi kupuuzwa wala kubadilishwa kwa kufuata mapokeo, utamaduni au mitazamo ya kisasa.

Kwa mujibu wa andiko hili(1 Wakorintho 11:7), mwanaume asalipo, anapokuwa katika ibada, au anapohubiri, akifunika kichwa anamvunjia heshima Yesu Kristo, ambaye ni kichwa chake. Mwanaume anapaswa kuonyesha heshima ya kiroho mbele ya Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo - kwa kutokufunika kichwa. Agizo hili ni kwa wanaume wote. Hata Papa agizo hili linamhusu. Hata Maaskofu na Mapadre, agizo hilo linawahusu, kwa kuwa na wao ni wanaume.

Anayepinga aweke hapa hoja za kimaandiko.

Agizo hili lina muktadha wa kitamaduni na kiibada ambao unapaswa kufahamika vizuri kabla ya kutumiwa kama sheria ya hukumu au ukataaji wa watu wengine.

Uitamaduni wa Korintho

Katika jamii ya wakati huo, Korintho ilikuwa jiji lenye mchanganyiko mkubwa wa tamaduni na dini. Kawaida, wanaume wa mataifa walikuwa wakifunika vichwa vyao katika ibada za kipagani. Paulo alitaka Wakristo waepuke tabia za kipagani zilizoleta mkanganyiko au kashfa, ili waoneshe utofauti wa kiimani.

Hivyo, agizo hili lililenga pia kuonyesha utofauti kati ya ibada ya Kikristo na ibada za kipagani., wala si Wokovu au usafi wa kiroho
 
Je, ni sahihi kwa mwanaume kuvaa kofia au kufunika kichwa chake anapokuwa katika ibada? Biblia inalo jibu la wazi kabisa.

Katika 1 Wakorintho 11:4, Mtume Paulo anaandika:
“Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake... Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu...”

Hili ni agizo dhahiri kutoka kwa Mungu. Neno hili halipaswi kupuuzwa wala kubadilishwa kwa kufuata mapokeo, utamaduni au mitazamo ya kisasa.

Kwa mujibu wa andiko hili(1 Wakorintho 11:7), mwanaume asalipo, anapokuwa katika ibada, au anapohubiri, akifunika kichwa anamvunjia heshima Yesu Kristo, ambaye ni kichwa chake. Mwanaume anapaswa kuonyesha heshima ya kiroho mbele ya Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo - kwa kutokufunika kichwa. Agizo hili ni kwa wanaume wote. Hata Papa agizo hili linamhusu. Hata Maaskofu na Mapadre, agizo hilo linawahusu, kwa kuwa na wao ni wanaume.

Anayepinga aweke hapa hoja za kimaandiko.
Hapo vipi...👇👇

Wakorinto 14:34-38 “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
 
Je, ni sahihi kwa mwanaume kuvaa kofia au kufunika kichwa chake anapokuwa katika ibada? Biblia inalo jibu la wazi kabisa.

Katika 1 Wakorintho 11:4, Mtume Paulo anaandika:
“Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake... Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu...”

Hili ni agizo dhahiri kutoka kwa Mungu. Neno hili halipaswi kupuuzwa wala kubadilishwa kwa kufuata mapokeo, utamaduni au mitazamo ya kisasa.

Kwa mujibu wa andiko hili(1 Wakorintho 11:7), mwanaume asalipo, anapokuwa katika ibada, au anapohubiri, akifunika kichwa anamvunjia heshima Yesu Kristo, ambaye ni kichwa chake. Mwanaume anapaswa kuonyesha heshima ya kiroho mbele ya Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo - kwa kutokufunika kichwa. Agizo hili ni kwa wanaume wote. Hata Papa agizo hili linamhusu. Hata Maaskofu na Mapadre, agizo hilo linawahusu, kwa kuwa na wao ni wanaume.

Anayepinga aweke hapa hoja za kimaandiko.
Wewe huyo ni Paulo sio Mungu
Mungu hakuwahi kusema hivyo usimsingizie
 
Vipi nikitia mkilemba kama Ayatollah?! Kilemba ni tofauti na kofia ujue?
 
Wanaume, lichukulieni jambo hili kwa uzito, kama ishara ya kumheshimu Mungu aliye Mkuu.

Vinginevyo siku ile ya mwisho kuna hatari ya kuambiwa:
“Siwajui ninyi, wala mtokako. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!" (Luka 13:27).

Luka 6:46-49
"Kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, lakini hamyatendi nisemayo?"
Tofautisha kati ya Kristo na Paulo

Halafu sio kila neno lililomo kwenye bible ni la Mungu, maana kuna vitabu kama Ruthu, Wafalme, Mhubiri, Mithali n.k ukivisoma vizuri unaona hizi ni historia na maneno ya hekima ya wazee wa Kiyahudi sio vitabu vya Mungu
 
Je, ni sahihi kwa mwanaume kuvaa kofia au kufunika kichwa chake anapokuwa katika ibada? Biblia inalo jibu la wazi kabisa.

Katika 1 Wakorintho 11:4, Mtume Paulo anaandika:
“Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake... Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu...”

Hili ni agizo dhahiri kutoka kwa Mungu. Neno hili halipaswi kupuuzwa wala kubadilishwa kwa kufuata mapokeo, utamaduni au mitazamo ya kisasa.

Kwa mujibu wa andiko hili(1 Wakorintho 11:7), mwanaume asalipo, anapokuwa katika ibada, au anapohubiri, akifunika kichwa anamvunjia heshima Yesu Kristo, ambaye ni kichwa chake. Mwanaume anapaswa kuonyesha heshima ya kiroho mbele ya Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo - kwa kutokufunika kichwa. Agizo hili ni kwa wanaume wote. Hata Papa agizo hili linamhusu. Hata Maaskofu na Mapadre, agizo hilo linawahusu, kwa kuwa na wao ni wanaume.

Anayepinga aweke hapa hoja za kimaandiko.
Barua ya Mtume Paulo kwa Wakorintho. Hayo yalikuwa ya kwake wala siyo ya Mungu
 
Back
Top Bottom