Kama hujajifunza
principles of effective communication na
message clarity, ngoja nikumegee kidogo points mbili:
1.
Principle of Clarity (Uwazi wa Ujumbe)
Communication theory inasisitiza kuwa ujumbe mzuri unapaswa kuwa wazi na rahisi kueleweka. Kuongea mada moja inasaidia kuepuka mkanganyiko kwa wasomaji na kufanya ujumbe ueleweke haraka.
2.
Information Overload Avoidance
Katika Shannon-Weaver Communication Model, kuna kipengele cha "noise" (kelele au usumbufu) kinachoweza kuathiri upokeaji wa ujumbe. Kuongea mada moja hupunguza "semantic noise" — yaani, usumbufu unaotokana na kuchanganya mada nyingi bila mpangilio.
Sura ya 11 ya 1 Wakorintho ina mada nyingi sana. Kwa mfano:
- Umuhimu wa kumfuata Paulo kama anavyomfuata Kristo
- Sifa kwa Wakorintho kwa kushika mafundisho
- Mpangilio wa mamlaka: Mungu - Kristo - Mwanaume - Mwanamke
- Umuhimu wa kufunika kichwa mwanaume
- Kwanini mwanamke ana nywele ndefu
- Kwanini mwanamke anapaswa kufunika kichwa
- Kama mwanamke hapendi kufunika kichwa afanyeje
- Tunapohutubu na kuomba tuwe katika hali gani
- Uwezekano wa kukusanyika kanisani kwa hasara
- Utaratibu wa kula chakula cha Bwana
- Madhara ya kula chakula cha Bwana isivyostahili
Sasa wewe unataka niongee mada zote hizo kwenye uzi mmoja tu, wakati unajua wazi kwamba JF ina watu wengi wavivu wa kusoma nyuzi?